#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:


a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Tume ya hovyooooo kuwahi kutokea tz,watakuwa walitumwa hawaaaaaa.sisi Hatuna corona tuna Mungu.
 
Maswali yako yote ya kidwanzi tu. Ndio tatizo la baadhi yetu humu - kujifanya tunajua kumbe hovyo tu!! Wasio na utaalamu ndio wanaotoa tatuzi za kitaalamu na kuuliza vitu vya ajabu!

Fact ni hii - toka tarehe 26/04/2020 Rais alizuia kupima wala kutoa takwimu za maambukizi na vifo. Tukaambiwa corona imekwisha Tanzania!! Unataka tume ukupe taarifa ambazo serikali ilizuia kuzitoa??? Unajua hata kwanini Dr. Ndugulile alitumbuliwa?? Tanzania hii ya leo anayepimwa ni msafiri wa nje ya nchi tu - hata mgonjwa hospitali hapimwi!! Mnabeza barakoa halafu mnataka kujua madhara yake msipozivaa??

Takwimu hukusanywa kwanza kabla ya kufanyiwa upembuzi kuhojiwa!!

Tushukuru sana Mungu mkuu - ugonjwa huu unafikia kuua asilimia ndogo sana ya watu!!!
Sawa mtaalamu maswali yangu ni kiduwanzi.

Sasa kama ni hivyo ilikuwa na haja gani kuunda tume na kutuambia inafanya utafiti kwa kipindi chote kile? waliyokuja kutoa mapendekezo ni mambo ambayo yanajulikana na tulishawahi kuyafanya huko mwanzoni tulikuwa tunapima na kutoa takwimu na kuchukua tahadhari mbalimbali labda kipya ni hizo chanjo ambazo zilikuwa bado kipindi kile, sasa hayo yanahitaji Maprofesa kukaa muda wote ule ndio kuja kutueleza hayo?

Kuna watu humu walikuwa wanasema madaktari huko wanajua ukweli kuhusu corona ila wamezuiliwa kusema ukweli na tuhuma za serikali kuficha ukweli wa kuhusu hili janga ni mambo ambayo yamezungumziwa sana, sasa nilidhani hiyo kamati ingeanzia huko ila yenyewe imekusanya Maprofesa na kuja na mapendekezo ya mambo ambayo wote tunayajua.
 
Unataka kuniambia hawa watu wangu wa mtaani hapa ambao hawavai hata barakoa wala kunawa mikono achilia kuepuka mikusanyiko ndio chanjo zikija wataenda kuchanjwa kwa hiari yao kabisa? mimi nafikiri kunahitajika kulazimishana, wewe hebu angalia muitiko wa kuvaa barakoa yani pamoja na watu kumuona Rais anavaa barakoa ila watu hata haijawashtua ndio hao watu watachanjwa kweli kwa hiari?

Hapa ni kulazimisha au kutafuta njia ya kuwatisha kinyume na hivyo tusiongopeana watakaochanjwa watahesabika.
BRO BLACK SKIN NI NOMA SANA SISI! KWENYE SWALA LA NAMA HYO KUKATAA CHANJO ISSUE NDUGU
 
Watu mshirikishe ubongo kidogo !
VP wakati akiwa Waziri wa Mapene alitandikwa hii kitu.....Meko kama angechomoa .....angeweza kuwa na mtazamo mwingine .......SHS anashauriwa kwa karibu na VP ambaye ni muhanga ...kusoma hamjui picha nazo hamzioni ......Hivi ulishajiuliza kwa nini kuna mabadiriko ya ghafla juu ya mtazamo wa Corona baada ya mwendazake!
Hivi kati ya wewe na watu wa serikali nani anajua kipi kilipita na mwendazake kati ya Korona na Umeme katika mfumo wa moyo ?
Lakini pia kama vijana hamtaki chanjo acha ije kwa ajili ya wazee over 60 yrs na others in risk! Kwani hawana cha kupoteza!
 
Ndio sio lazima, sasa kwanini umekuwa ukitaja hizo chanjo zengine pamoja na tiba zengine kisa wanapinga hizi chanjo za corona?
Kwa sababu mna potosha kwamba chanjo ya Covid pekee ndio ina side effects wakati kuna tiba za radiology ambazo zina madhara kwa watumiaji 38% ila sijawahi sikia mkizikosoa au kudai wazungu wanatuua.

Embu nikuulize tu kivp tiba 90% zimetoka kwa beberu ila hamzipingi but ikija chanjo tu ndio wanataka kutuua?? Double standards ni kwa faida ya nani
 
Kwa sababu mna potosha kwamba chanjo ya Covid pekee ndio ina side effects wakati kuna tiba za radiology ambazo zina madhara kwa watumiaji 38% ila sijawahi sikia mkizikosoa au kudai wazungu wanatuua.

Embu nikuulize tu kivp tiba 90% zimetoka kwa beberu ila hamzipingi but ikija chanjo tu ndio wanataka kutuua?? Double standards ni kwa faida ya nani
Hata humu hujawahi kuona nyuzi watu wakipinga ARV na kukataa kuwa hakuna virusi vya ukimwi?
 
Hapa ni kulazimisha au kutafuta njia ya kuwatisha kinyume na hivyo tusiongopeana watakaochanjwa watahesabika.
Mbona Uganda chanjo ni optional kama zilivyo tu za Yellow fever..... Hutaki unaacha. Sasa wapi wamesema ni lazima mchanjwe mamilion?

Hata humu hujawahi kuona nyuzi watu wakipinga ARV na kukataa kuwa hakuna virusi vya ukimwi?
Wanaopinga ARV hawazidi 100 ila chanjo ya Covid kelele ni zaidi ya mamilion ya wa-TZ ambao walipotoshwa na JPM.

Sasa najiuliza wakati mnapotosha hao Millions of illiterate Tanzanians kwanni hamkuwaambia tiba ya kansa inaua hta kuliko kansa yenyewe? Kwanni hamkuwaambia wenye wagonjwa wa Ukimwi kwamba ARV zitawaletea madhara mengi kwenye organs zao baada ya matumizi ya dawa kwa miaka mingi?? Hizo taarifa mmeficha ila kwa Covid ndio mnageuka mko concerned na afya zao.
 
Unataka kuniambia hawa watu wangu wa mtaani hapa ambao hawavai hata barakoa wala kunawa mikono achilia kuepuka mikusanyiko ndio chanjo zikija wataenda kuchanjwa kwa hiari yao kabisa? mimi nafikiri kunahitajika kulazimishana, wewe hebu angalia muitiko wa kuvaa barakoa yani pamoja na watu kumuona Rais anavaa barakoa ila watu hata haijawashtua ndio hao watu watachanjwa kweli kwa hiari?

Hapa ni kulazimisha au kutafuta njia ya kuwatisha kinyume na hivyo tusiongopeana watakaochanjwa watahesabika.
Kwa nini tulazimishane ? Kila mtu na maamuzi yake vinginevyo itakuwa ni udikteta
 
Mbona Uganda chanjo ni optional kama zilivyo tu za Yellow fever..... Hutaki unaacha. Sasa wapi wamesema ni lazima mchanjwe mamilion?


Wanaopinga ARV hawazidi 100 ila chanjo ya Covid kelele ni zaidi ya mamilion ya wa-TZ ambao walipotoshwa na JPM.

Sasa najiuliza wakati mnapotosha hao Millions of illiterate Tanzanians kwanni hamkuwaambia tiba ya kansa inaua hta kuliko kansa yenyewe? Kwanni hamkuwaambia wenye wagonjwa wa Ukimwi kwamba ARV zitawaletea madhara mengi kwenye organs zao baada ya matumizi ya dawa kwa miaka mingi?? Hizo taarifa mmeficha ila kwa Covid ndio mnageuka mko concerned na afya zao.
Usiseme wanapotosha, nimekupa huo mfano wa ARV ili kuonesha kuwa wapo wenye mtazamo tofauti na kuhusu huo uchache wao ni kutokana hakuna uhuru kwa mtu kuweza kueleza ubaya wa ARV na kupinga uwepo wa virusi vya ukimwi hadharani kisha akaachwa tu.
Mimi binafsi nilikuwa natamani kweli Magufuli afike huko kwenye ARV.

Sasa Tanzania suala la hiari ya kuchanjwa chanjo za corona zoezi litadoda kwa sababu watu hawaoni sababu za kuchanjwa na hawana iman na hizo chanjo.
 
Kamati ya corona majina yalifanywa siri kana kwamba ni kamati ya roho mbaya! Hata walipoibuka kwenye kamera walikuwa wamevaa kininja ili kuficha nyuso kwa kisingizio cha corona!! Kwa maigizo Tanzania hatujambo!!
 
Hizo chanjo wakajichanje wao na mama zao. Hatutaki upuuzi wa kudungana masumu ya ajabu ajabu.

Ati ooh tuko kwenye hatari ya maambukizii! Hatari gani?

Watu tunadunda tu kila siku, hakuna cha corona wala baba yake corona.

Msitutibue vichwa kabisa na hayo machanjo yenu ya kihuni.
 
Back
Top Bottom