#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

kinachonifurahisha ni kwamba barakoa zinavaliwa kipindi cha kukabidhi na picha za kitaifa baada ya hapo wahusika maisha yao ya kawaida hawavai barakoa na wananchi wanaoongea nao hawaoni haja ya kuwapa barakoa japo katika kipindi cha kuongea nao ila hawaoni tabu kuwapa mlo.
bora mlo 7000 lakini sio barakoa ya 700/- kweli!
 
hii issue ya corona inamajibu mengi sana lakini wacha tutunze vibwaya vyetu tusubiri ngoma tucheze japo sina uhakika tutacheza tutakavyo bali wapiga ngoma watakavyo!
 
Taifa linakwenda kuanguka.. tulikuwa tumejizoea mfumo huu.. sasa malengo yao ya kuitia dunia hofu yamekamilika... Siku tu idadi ikianza kutangazwa nchi itaingia kwenye tahaharuki ya kudondoka mtu..

Ni kwel tunahitaji chanjo?? Au tunahitaji kuingia kwenye Muunganiko wa kuana?? Who knows after kinanachoitwa chanjo??

Kama ni Kinga kwel y India imepiga balaa?? Hiv kwel thinktank ya kamati ndo hayo tu mapendekezo? Au yalikuwa maelekezo? Mbona Kama yalijulikana before?? No anynews!!!

Anyway ngoja tutiane hofu ili malengo yafikiwe..
The deal is done, the report poses as a covert defense amid the citizens cold backlash
 
Taifa linakwenda kuanguka.. tulikuwa tumejizoea mfumo huu.. sasa malengo yao ya kuitia dunia hofu yamekamilika... Siku tu idadi ikianza kutangazwa nchi itaingia kwenye tahaharuki ya kudondoka mtu..

Ni kwel tunahitaji chanjo?? Au tunahitaji kuingia kwenye Muunganiko wa kuana?? Who knows after kinanachoitwa chanjo??

Kama ni Kinga kwel y India imepiga balaa?? Hiv kwel thinktank ya kamati ndo hayo tu mapendekezo? Au yalikuwa maelekezo? Mbona Kama yalijulikana before?? No anynews!!!

Anyway ngoja tutiane hofu ili malengo yafikiwe
Kaka hakuna anakuzuia kujielimisha.
1. Ndiyo, chanjo ni kinga. Si 100% lakini kama 80-90%. Imethibitishwa na wataalamu China, Afrika Kusini, Urusi, Uhindi, Marekani, Ulaya, Australia ...

2. Wewe huhitaji chanjo kama hutaki. Ila ukubali wengine wanafanya maazimio yao kwa hiyo usitegemee kuhiji Makka, kufanya biashara China, kusoma Ulaya au Marekani. Ni azimio lako. Pamoja na kutoingia katika nchi jirani zitakazoweka mashariti ya kuonyesha kadi ya chanjo wakati ujao.

3. Tatizo la Uhindi ni: A) hadi sasa walifikia asilimia ndogo mno wa watu wao, hata kama wamshapiga mamilioni lakini wako zaidi ya biloni. B) baada ya kupita vema awamu ya kwanza sisas yao ililegea. Waziri Mkuu Modi anatafuta kura za wafzasi wa Uhindi, hivyo hakutaka kutamka maonyo au kutangaza mashariti wakati wa sikuu kubwa ya Kinhidu ambako mamilioni walihiji na kuktana; pia walikuwa na kampeni za uchaguzi katika majimbo kadhaa bila mashariti yoyote kwenye miktano ya hadhara. Sasa wanavuna matokeo.

Katika yote nahofia Tanzania imeshapitiwa na wakati kupata chanjo karibuni. Nchi kadhaa zilichangia pesa ili Afrika ipate kiasi cha chanjo; akiba hii inakwisha sasa. Uhindi walipata mlipuko ho hivyo hao, ilhali ni watengenezaji wakuu wa madawa duniani, wamapiga marufuku kuuza dawa la chanjo nje ya Uhindi hadi waendelee kufikia watu wao wenyewe.
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:


a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Kwa taarifa hii, waziri wa afya na naibu waziri wa afya wawajibike kwa kujiizulu. Pia walimdanganya JPM
 
Ndo wameandika hayo mavitabu yote au wamekopi tu maandishi ya wengine na kuyakusanya na kuyaweka yaonekane kama mavitabu?

Halafu sidhani kama Samia atayasoma 🤣.

Sidhani kama ni mtu wa kusoma mavitabu kama hayo.

Yeye ni mitandao tu 🤣🤣.
Wasukuma bado mna madukuduku,
Hapo ndipo tutajua tuna zaidi ya dhaifu Ikulu pale anajilembua.
Mtheenge ww,, acha dharau kwa Rais
 
Taifa linakwenda kuanguka.. tulikuwa tumejizoea mfumo huu.. sasa malengo yao ya kuitia dunia hofu yamekamilika... Siku tu idadi ikianza kutangazwa nchi itaingia kwenye tahaharuki ya kudondoka mtu..

Ni kwel tunahitaji chanjo?? Au tunahitaji kuingia kwenye Muunganiko wa kuana?? Who knows after kinanachoitwa chanjo??

Kama ni Kinga kwel y India imepiga balaa?? Hiv kwel thinktank ya kamati ndo hayo tu mapendekezo? Au yalikuwa maelekezo? Mbona Kama yalijulikana before?? No anynews!!!

Anyway ngoja tutiane hofu ili malengo yafikiwe
Acha ujinga wewe bwege. Kwa taarifa yako ni kuwa yule hayati kama angekuwa anazingatia kuwa Corona ni hatari asingekufa na wala yale mavifo ya ajabu ajabu yasingekuwepo. Ulizoea kuishi hivyo wewe na nani wakati mwenzako ameshafariki?

Hivi unajua kuwa India walifanya mzaha kama wewe unachotaka tufanye unaona madhara yake? Emb funga up! Hujui Corona imeigharimu nchi kiasi gani. Au kwa vile wewe hujafa?
 
Utakayekataa Chanjo utajikosesha kusafir nchi kadhaaa.hii itakuja kuwa km ya yellow kadi . Mama ana maono sema kumuelewa unahitaj usiwe na mihemko.over.
 
Twafaaaaaa jamani hao wazee wanaotaka chanjo wajichanje wenyewe watuache vijana manake wao wanataka kuharakia kufa sisi vijana watuache tuendeleze taifa manake nasikia chanjo mbeleni huko miaka 30 hivi ijayo genes zetu zinaweza badilika chanjo ni mbaya wazungu wenyewe hawaitaki
Umasikini wa kifikra ni kitu kibaya sana
 
Bado natafakari sana, kamati ya wataalam awamu ya sita ni kina nani na kamati ya watalaam awamu ya tano ni kina?....kwanini kamati awamu ya tani ilishauli vile na kamati awamu ya sita imeshauli hivi?
 
Taifa linakwenda kuanguka.. tulikuwa tumejizoea mfumo huu.. sasa malengo yao ya kuitia dunia hofu yamekamilika... Siku tu idadi ikianza kutangazwa nchi itaingia kwenye tahaharuki ya kudondoka mtu..

Ni kwel tunahitaji chanjo?? Au tunahitaji kuingia kwenye Muunganiko wa kuana?? Who knows after kinanachoitwa chanjo??

Kama ni Kinga kwel y India imepiga balaa?? Hiv kwel thinktank ya kamati ndo hayo tu mapendekezo? Au yalikuwa maelekezo? Mbona Kama yalijulikana before?? No anynews!!!

Anyway ngoja tutiane hofu ili malengo yafikiwe..
Soon, rais ataambiwa TZ mulichelewa, kopa pesa kwa ajili ya COVID. Naanza kuona anguko letu ili wasema JPM alituponza.
 
Bado natafakari sana, kamati ya wataalam awamu ya sita ni kina nani na kamati ya watalaam awamu ya tano ni kina?....kwanini kamati awamu ya tani ilishauli vile na kamati awamu ya sita imeshauli hivi?
Uzuri wa kamati za marais wetu hushauri kutegemea ufahamu wa aliyeiunda.
 
Jamani kuna jipya kwenye mapendekezo yatakayoletwa kutoka kwenye kamato ya RJMT ya COVID-19 au ni kuigilizia yale ya USA na ulaya?
 
Back
Top Bottom