Kamati Teule ya Bunge Iundwe kuhusu Kashfa ya Rada

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Ili tuweze kuwachukulia serious watawala wetu na hasa wabunge wetu kwenye suala la rada wakati umefika kwa Wabunge wote kukubaliana kuunda Kamati Teule ya Bunge ambayo itafanya uchunguzi wa wazi na huru kuhusu nini kilitokea. Hii itakuwa ni hatua ya kwanza ya kutufanya tuamini kuwa serikali yetu kweli iko makini na imeguswa. Hadi hivi sasa walioonekana kufuatilia ni Waingereza tu. Kamati Teule iundwe mara moja kabla ya kuendelea na kudai fedha zaidi.

Kamati Teule ikishaundwa na kupewa TOR za kueleweka tutakuwa tayari sisi wengine kuwasaidia ushahidi utakaowasaidia. Tutatoa ushirikiano kama kwenye Kamati Teule ya Richmond. Tunajua mengi kweli. Hatuitaji mjadala wa Rada uwe hivi hivi, mjadala utakuwa na maana kama kutoka hapo itaundwa kamati teule.
 
you cant be serious....kaka its 2011 bado una advocate kamati tuu?

dont u think we've passed that point?

dawa ni kukomaa na hii katiba mpya bila hiyo huku kwingine tunapoteza muda tuu
 
Mkuu Mwanakijiji hoja yako ni nzuri sana lakini uzoefu unaonesha kuwa ripoti za tume nyingi zilizoundwa kipindi cha nyuma zimeishia kwenye makabati na hazijawahi kufanyiwa kazi. Viongozi wetu hawapendi ukweli na ni werevu katika kuchakachua mambo na kufanya yaonekane jinsi watakavyo wao. Kuna haja ya kutafuta njia mbadala ya kupambana na hawa viongozi wetu ambao kwa lugha nyepesi tunaweza kuwaita kuwa ni WABAKAJI WA HAKI na WAPENZI WA MAOVU NA MAJONZI KWA JAMII.
 
gademu.. somebody hit me.. nani kataja tume humu!!? Jamani hata watu hawajui Kamati Teule ni kitu gani? Hivi ripoti ya mwakyembe ilikuwa siri? Kamati Teule ndio chombo pekee ambacho kinaweza kuwaita hawa watu kwa lazima, wakahojiwa hadharani na ikasomwa Bungeni kama ilivyosomwa ya Mwakyembe.. wanaogopa nini?
 
you cant be serious....kaka its 2011 bado una advocate kamati tuu?

dont u think we've passed that point?

dawa ni kukomaa na hii katiba mpya bila hiyo huku kwingine tunapoteza muda tuu
sikubaliani na wewe hata kidogo
Kamati itawezesha kujua namna viongozi wengine wa kitaifa walivyoshiriki huu mchezo.
Muhimu ni namna JESHI LA ULINZI TANZANIA LILIVYOSHIRIKI as JESHI limejaa uchafu sana kwa visingizio vya kijinga.
Maofisa wa JESHI ni too corrupt, wanakul;a kama mchwa hawakaguliwi kwa hiyo ni muhimu tujue ushiriki wao
 
Hata ikiwa ni Kamati bado wanaweza kuiunda na kuifanya ifanye kazi kulingana na matakwa yao. Katika hali yoyote naona uchakachuaji wa mambo lazima utakuwepo hasa ukiangalia jinsi wabunge wanaojiita kuwa wako wengi bungeni wanavyopitisha na kushabikia hoja za kijinga na za kipuuzi ndani ya bunge.
 
jamani basi mjifunze kidogo juu ya kamati teule zinavyofanya kazi. Itasaidia maana tukianza kutoa elimu hii ya "Kamati Teule" na nguvu zake ambazo ni sawa na za mahakama itakuwa vurugu kwa kweli.
 
Kama serikal inadai hakna alye na ushahdi km Chenge ni fisadi kamati itawezaje kpata ukwel, me nawashaul wawaone Mwanaharisi wana nyaraka zote.
 
Kamati ya nini, hapo ni kuzidi kutafuna kodi zetu tu, sijaona kamati iliyoleta matunda, ni bla bla tu.
 
Kamati ya nini, hapo ni kuzidi kutafuna kodi zetu tu, sijaona kamati iliyoleta matunda, ni bla bla tu.
angalau sisi wananchi wa tanzania tutajua ukweli wa nani alishiriki na ushiriki wake, hiyo ni faida kubwa kuliko kazi hii wakiachiwa pccb
 
Mwanakijiji,

Nahisi wanajua what does "kamati teule" mean. Matokeo ya hizo kamati kila mtu anajua na hata wewe unajua. Hivi kuna potential outcomes gani ya kamati ya mwakyembe zaidi ya kugawana vyep au kushushwa hadhi kwa akina Sitta? Achilia mbali kifo cha CCJ?

Well, they will buy your idea and chair of that committee is Edward Lowassa (or his type), other members are Jan Makamba, Kigwangallah, Serukamba, Augustine Mrema, Leticia Nyerere Mageni, Juma Nkamia, Pro. Stephene aka Maji marefu, and Zambi. Predict the outcome.

Tumechoka, waache tu. Weldone Tundu Lissu. Jana umeweka historia na maneno yako na sura yako viliendana mana Chenge/ Chikawe au mzushi yeyote angekuwa karibu yako ngumi au kichwa ilikuwa halali yako.
 
Ni wazo jema, lakini kwa yale yalipita bado nadhani 'sirikali' chini ya wezi wenyewe haitafanya la maana sana.
 
jamani basi mjifunze kidogo juu ya kamati teule zinavyofanya kazi. Itasaidia maana tukianza kutoa elimu hii ya "Kamati Teule" na nguvu zake ambazo ni sawa na za mahakama itakuwa vurugu kwa kweli.
Mi sina hata hamu na hizo kamati za bunge unazozizungumzia, kwani bunge lina kamti ngapi? Na hizo kamati zimefanya nini ambacho watanzania tunajivunia? Au na wewe ni gamba? Hizo hizo kamati zinageuka kuwa mafisadi wa kuhujumu uchumi. Mfano kamati ya madini si juzi tu wanalalamikiwa kupokea mlungula ili wapitishe bajeti ya wizara ya nishati na madini! Au we unazungumzia kamati iundwe na kina nani?
 
Ili tuweze kuwachukulia serious watawala wetu na hasa wabunge wetu kwenye suala la rada wakati umefika kwa Wabunge wote kukubaliana kuunda Kamati Teule ya Bunge ambayo itafanya uchunguzi wa wazi na huru kuhusu nini kilitokea. Hii itakuwa ni hatua ya kwanza ya kutufanya tuamini kuwa serikali yetu kweli iko makini na imeguswa. Hadi hivi sasa walioonekana kufuatilia ni Waingereza tu. Kamati Teule iundwe mara moja kabla ya kuendelea na kudai fedha zaidi.

Kamati Teule ikishaundwa na kupewa TOR za kueleweka tutakuwa tayari sisi wengine kuwasaidia ushahidi utakaowasaidia. Tutatoa ushirikiano kama kwenye Kamati Teule ya Richmond. Tunajua mengi kweli. Hatuitaji mjadala wa Rada uwe hivi hivi, mjadala utakuwa na maana kama kutoka hapo itaundwa kamati teule.

Nakubaliana na wewe kabisa katika hili.
Tatizo langu lipo katika UHURU wa Bunge, KUFIKIRIA WAZO HILO, KUUNDA KAMATI na hatimaye KUJADILI TAARIFA YA KAMATI HIYO na KUTOA MAPENDEKEZO, kumbuka hizi si zama za Mzee SITTA.

ToR
1. Iongozwo na mbunge mwanasheria asiyetoka chama tawala;
2. Wakusanye ushahidi utakaowatia hatiani wahusika wa mkataba huu
3. Kamati ikikamisha kukusanya ushahidi wawapeleke wahusika mahakami bila kupitia kwa DPP
4. Mwenendo wa kesi uwekwe wazi kwa umma (PublicT
 
Ndiyo ni kweli m/kijiji, lakini kamati ingefanya kazi kama tungekuwa na spika wa aina ya sitta au utayari wa wabunge wetu..msiibeze kamati ya mwakyembe kuna watu wamejeruhiwa mle hawatapona hata kwa kikombe cha babu,vile vile ni mwiba ambao ccm wameshindwa kuutoa ambao unatabiriwa kuipeleka ccm chini 2015;kwani kila dalili za kumsimamisha lowasa zinadhihiri na ndipo ulipo msiba wakujitakia wa babu kabwela aliyezeeka
 
Jamani ili swala la rada ushahidi upo wazi, kinachotakiwa watu wapelekwe mahakamani! Barua kutoka SFO kwenda AG-URT inatamka wazi kabisa maofisa wa serikali ya tz waliohusika ktk sakata hili, uchunguzi mwingine wa nn?! Mengine yatabumbuluka ukouko makamani.
 
gademu.. somebody hit me.. nani kataja tume humu!!? Jamani hata watu hawajui Kamati Teule ni kitu gani? Hivi ripoti ya mwakyembe ilikuwa siri? Kamati Teule ndio chombo pekee ambacho kinaweza kuwaita hawa watu kwa lazima, wakahojiwa hadharani na ikasomwa Bungeni kama ilivyosomwa ya Mwakyembe.. wanaogopa nini?

hilo litazimwa kwa kisingizio kuwa kesi ilishapelekwa mahakamani.
 
Nakubaliana na wewe kabisa katika hili.
Tatizo langu lipo katika UHURU wa Bunge, KUFIKIRIA WAZO HILO, KUUNDA KAMATI na hatimaye KUJADILI TAARIFA YA KAMATI HIYO na KUTOA MAPENDEKEZO, kumbuka hizi si zama za Mzee SITTA.

makinda hana jeuri hiyo, si umeona mzee wa vijisent alivyofanya mbinu za kugombea uspika ili tukose sote?? sasa unatarajia kamati teule iwe na sura gani? labda mwenyekiti wa hiyo kamati awe mzee wa vijisenti.
 
Back
Top Bottom