Kamata kamata ya TANROADS, tuoneeni huruma

cmoney

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
3,603
Reaction score
5,588
Nmeingia kwe kasherehe ka ndugu yangu nikaacha kamkweche kangu nje parking ya ukumbi mbali na Barabara.

Wamekuja vijana wa TANROAD hawasikii la muadhini wala nini, wanasema nimepaki kwenye hifadhi ya barabara faini laki 2, jamani tuoneane huruma, kweli kwa uchumi huu hii fedha ni ya kutafuta mwezi nzima.

Sheria zipi? Sikatai ila zisiwe sheria za kuumizana maana badala ya kufundisha zinaleta chuki tu kati ya wananchi na haya mashirika.

Naomba waliangalie hili na kutupa mwelekezo badala ya kutengenezeana mazingira ya kuumizana.
 
tii sheria bila shurti! nachukiaga napoonaga watu wanafanya makosa alafu wanabaki kulialia waonewe huruma
 
Unajua
Haaa!? Umetisha sana. Ukiendelea na moyo huo utakuwa mbeba viatu wa Kiongozi wa Malaika Mbinguni.
Unajua kitu ambacho watu wanashindwa elewa ni kua ukiongea kero yoyote unaokena unapinga ufalme uliopo...hv ni kwa sheria gani umepaki nje ya barabara hata pavement zake hujazigusa faini laki2 sasa ukigonga yale mawe so ndo watataifisha gari kabisa...hii sheria haipo wazi na ya kionevu
 
Sheria ni zetu na Barabara ni zetu pia.
Vyote ni vya kwetu, tusianzishe ili kukomoana.
Wewe utoe laki 2 kirahisi rahisi tu? Unaitoa fungu gani?

Hebu Tanroads kuweni na akili, faini hata ingekua elfu 20 inatosha.

Mnazidi kuichonganisha serikali kwa wananchi jamani. Mnajenga chuki nyie mlopewa mamlaka tumieni mamlaka yenu vizuri
 
Nmeingia kwe kasherehe ka ndugu yangu nikaacha kamkweche kangu nje parking ya ukumbi mbali na Barabara.

Wamekuja vijana wa TANROAD hawasikii la muadhini wala nini, wanasema nimepaki kwenye hifadhi ya barabara faini laki 200, jamani tuoneane huruma, kweli kwa uchumi huu hii fedha ni ya kutafuta mwezi nzima.

Sheria zipi? Sikatai ila zisiwe sheria za kuumizana maana badala ya kufundisha zinaleta chuki tu kati ya wananchi na haya mashirika.

Naomba waliangalie hili na kutupa mwelekezo badala ya kutengenezeana mazingira ya kuumizana.
Wapi huko!?
 
Karibu kwy ulimwengu wa magari. Uku kwy magari ukinunua Gari unatakiwa, uache kama million 2 kwa ajili ya kuzoe majanga yatakayotokea kwa iyo Gari. Izo ndio principal za kumiliki Gari au chombo cha motto. Ukiziweza izo principles uwezi kuja kulia lia apa kwa Jamii Forum.
Inapendeza ukawa na asilimia 10 ya pesa uliyonunulia Gari iyo. Ndio maana unakuta MTU ana pesa nyingi unakuta ananunua Gari ya million 16. Unakuta pembeni kaweka kama million zake za kubadilisha vitu, kama matairi na vinginevyo
 
Sheria ni zetu na Barabara ni zetu pia.
Vyote ni vya kwetu, tusianzishe ili kukomoana.
Wewe utoe laki 2 kirahisi rahisi tu? Unaitoa fungu gani?

Hebu Tanroads kuweni na akili, faini hata ingekua elfu 20 inatosha.

Mnazidi kuichonganisha serikali kwa wananchi jamani. Mnajenga chuki nyie mlopewa mamlaka tumieni mamlaka yenu vizuri
Najiuliza sana kuwa awamu hii viongozi
WAMETOKEA NCHI GANI?
MBONA AWALI hatukushuhudia UBABE HUU?
 
Sheria ni zetu na Barabara ni zetu pia.
Vyote ni vya kwetu, tusianzishe ili kukomoana.
Wewe utoe laki 2 kirahisi rahisi tu? Unaitoa fungu gani?

Hebu Tanroads kuweni na akili, faini hata ingekua elfu 20 inatosha.

Mnazidi kuichonganisha serikali kwa wananchi jamani. Mnajenga chuki nyie mlopewa mamlaka tumieni mamlaka yenu vizuri
Halafu kwann nasema Imekaa kiuonevu yaani wao ndo wanakupangia sehem wanayosema umeingilia b arabara...mita 60 sio mchezo unayejihisi upo safe jiandae kuumia
 
Nmeingia kwe kasherehe ka ndugu yangu nikaacha kamkweche kangu nje parking ya ukumbi mbali na Barabara.

Wamekuja vijana wa TANROAD hawasikii la muadhini wala nini, wanasema nimepaki kwenye hifadhi ya barabara faini laki 200, jamani tuoneane huruma, kweli kwa uchumi huu hii fedha ni ya kutafuta mwezi nzima.

Sheria zipi? Sikatai ila zisiwe sheria za kuumizana maana badala ya kufundisha zinaleta chuki tu kati ya wananchi na haya mashirika.

Naomba waliangalie hili na kutupa mwelekezo badala ya kutengenezeana mazingira ya kuumizana.
Si walishakawatazwa hao wamerudi tena?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom