Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 572
- 356
Zoezi la bomoa bomoa katika barabara ya Morogoro kuanzia Kimara Mwisho hadi Kiluvya limekuwa likiendelea. Hata hivyo kuna mambo kadhaa ningependa kuwashauri TANROADS na wananchi wa sehemu husika. Kwa upande wa Tanroads ninapenda kuwashauri kama ifuatavyo.
1. Wanapovunja ni vizuri wakavunja mpaka mwisho wa eneo lao yaani watu wawe nje ya mawe na wajiridhishe kuwa hayo mawe hayachezewa na wananchi kwa kuhamishwa. Nasema hivi kwasababu kuna sehemu wanavunja mpaka mwisho wa eneo lao lakini kuna maeneo wanavunja halafu wanawaacha baadhi ya wananchi hasa wafanyabiashara za baa na matofari wakiwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara wakiendelea na biashara zao au huwavunjia nusu na kuwaacha nusu wakiwa ndani ya hifadhi. Nimeona mfano Mbezi mwisho kile kiofisi cha chama cha kijani kimeachwa nusu nzima ndani ya eneo la hifadhi. Mwananchi mwingine alipoona hivyo naye kaja kujenga nyumba yake usawa na ofisi hiyo. Ofisi za chama zisiwe kinga ya kuvunja sheria zibomolewe kama ilivyofanyika pale Kimara mwisho. Tabia hii huwatia tamaa wananchi wengine ambao nao huanza kurudi ndani ya hifadhi ya barabara kwa kujenga vibanda vya biashara ambapo tanroads huja tena na kuvivunja vibanda hivyo lakini wakiwaacha wenye baa na tofari ndani. Hapa hisia zilizopo ni kuwa baadhi ya wafanyakazi wa tanroads wanahongwa na wafanya biashara hao ndio maana wanawaacha waendelee na biashara zao.
Nawashauri tanroads waache mtindo wa kuvunja nusu nusu na kuwaaacha baadhi ya watu ndani ya hifadhi kwani inawatia tamaa wengine kurudi na kujenga tena. Wapite mara kwa mara kukagua na kuwaandoa wale wote wenye vibanda na wanaofanya biashara ndani ya hifadhi ya barabara. Unaweza kushangaa kukukuta tanroads inavunja vibanda vya mbao vya wamachinga vilivyomo ndani ya hifadhi lakini inawaacha wafanyabiashara ya baa na matofari ambao wamejenga vyoo kwa tofari na vibanda vya kudumu. Huu ni ubaguzi unaopaswa kukemewa.
2. Tanroads wasafishe maeneo yaliyovunjwa kwa kuondoa mapagare na kupunguza miti na misitu kwani eneo kubwa liko wazi hivyo siyo salama sana wakati wa usiku kutokana na giza.
3. Kubwa kuliko yote ni kuwa baadhi ya sehemu walizobomoa na kuwaondoa watu kuna makaburi ambako wakazi wa maeneo hayo waliwazika wafu wao. Tanroads itoe mwongozo kuhusu makaburi hayo ambayo yameachwa mapweke na sehemu hatarishi kwani hayana uangalizi tena na itakuwaje ujenzi ukianza?
4. Ni vizuri pia wakaweka sheria sasa au fine kwa mtu atayeingia katika eneo la hifadhi na kuanza kufanya shughuli zake. Hili mimeona Tanesco wamefanikiwa kwa kuwaondoa watu wote chini ya nyaya kuu za umeme ambapo wameweka mawe na vibao vya onyo. Wao wamewaondoa hata wafanya biashara wanaofyatua tofari na shughuli zingine zozote kwani wananchi ukiwaacha kidogo tu huwa wanatabia ya kujiimarisha kama ilivyotokea barabara ya Morogoro
Kwa upande wa wananchi ushauri wangu ni kutokusubiri magereda. Ukiambiwa ondoka jipange uondoke na uhamishe vitu vyako badala ya kubishana na serikali. Serikali ni chombo cha mabavu usitegemee hata siku moja kuwa itakuonea huruma. Utashangaa kukuta maghorofa yanavunjwa halafu mwananchi mwenye nyumba ya kawaida amekomaa anasubiri gereda linye liifinyange finyange nyumba yake kumbe angeweza kuokoa bati, milango na tofari kama angevunja mwenyewe.