Kamanda wa Malawi aapa kulinda Ziwa Malawi

Kamanda wa Malawi aapa kulinda Ziwa Malawi

Kuna vitu hapa tunachanganya, hapa kuna mipaka miwili, kuna mpaka wa kwanza uliowekwa na wakoloni ukionyesha ziwa lote ni la Malawi, lakini baada ya vita ya kwanza mpaka wakoloni wakachora mpaka mpya ambao uliligawa ziwa katikati, bongo tukapata na Malawi wakapata, ambao mkataba huu unaenda sambamba na sheria za umoja wa kimataifa kwamba mahali ambapo kuna ziwa na kuna nchi mbili mpaka unakuwa katikati ya ziwa lile. Lakini pia baada ya vita vya pili vya dunia,Tanzania iliendelea kuwa chini ya mkoloni (muingereza) kama mwangalizi ,sio mtawala,na sharia za kuwa mwangalizi huruhusiwi kuigawa nchi au kuhamisha mpaka wa nchi kwenda nchi nyingine,lakini waingereza ama kwa kupuuza au kulibeba koloni lake wakabadili mpaka wa ziwa na kulifanya ziwa lote kuwa ni mali ya Malawi. Pia kuna mkataba wa umoja wa nchi za Africa ,ambao unadai nchi za Africa wakubali mipaka iliyowekwa na wakoloni,nahisi mkataba huu ulikuja kuepusha migogoro baina ya nchi za Africa na tulisign hili dude, sasa swali ni kwamba mkataba huu wa Africa ambao tulisign kwa upande wa Tanzania tuheshimu mpaka upi? ule wa pili ( ambao unaeleza mpaka ni katikati) au ule wa tatu ambao waingereza walipeana ziwa lote kuwa mali ya Malawi pasifokufuata sheria? nadhani Tanzania wali sign mkataba wa Africa kwa tukijua mpaka ambao tunakubaliana nao ni ule wa pili ambao unaenda sambaba na sheria za umoja wa kimataifa, pia Malawi walisign mkataba ule wakijua wao wanafuata mpaka wa kwanza ambao walipewa na waingereza kuwa ziwa lote ni mali ya Malawi, hapa ndo sintafahamu inapoanzia. Sio sahihi kusema kuwa Tanzania walisign mkataba na nchi za Africa (OAU) kuwa tumekubali ziwa lote ni mali ya Malawi, hapa itabidi tuangalie mazingira yote na uhalali wa uingereza kurudia kwa mara ya tatu kugawa ziwa lile ambapo kisheria hakutakiwa kufanya vile, kwa hiyo pande zote zina sababu za kutosha kusema mpaka uwe katikati au laa.

Serikali ya Tanzania inatakiwa kuchangamka na kufuatilia suala hili na kumaliza tatizo hili kisheria once for all , kama nikutumia vyombo vya sheria vya ndani na nje, kama nikutumia wasuluhishi wa nchi pande zote mbili ,kama nikutafuta usuluhishi katika nchi wanachama wa SADC , AU,au UN basi tufanye hivyo, tusitegemee sana mambo ya utashi au busara za Maraisi walioko madarakani kwa pande zote mbili, utashi tu hautoshi maana unamaliza tatizo kwa muda mfupi linaibuka tena,hivyo hatusolve tatizo ila tunazuga zuga na kuvunga vunga tu, tutafute suluhu kisheria na tumalizane nalo.
mchango wako utazingatiwa!
 
ZIWA LIMEJAA MAFUTA. ..TUKAE NAO CHINI TUTAFUTE MBINU AMBAYO NCHI ZOTE MBILI ZITAFAIDIKA. .KULIKO KUGOMBANA. ..HAWA WAMALAWI HOVYO KABISA. ..SISI NI WASTAARABU SANA. ..
Kukaa chini ni kuwaomba na kuwabembeleza kwa sab kisheria ziwa ni lao lote kwa mujibu wa makubaliano yaliyoazimiwa na OAU na Nyerere alisaini kuwa michoro ya wakoloni iheshimiwe
 
Ningekuwa rais wa Tanzania ningepeleka huko bataliani moja ya jeshi na meli za kivita zipige doria pembezoni mwa hilo ziwa!
 
hujui kusom
Wanajamvi hili swala la mpaka wa ziwa Nyasa kati ya TZ na Malawi tusilichukulie lelemama, kwani wenzetu wako serious zaidi ya tunavyofikiri.

Kwa lugha yao wamesema hivi: “Timba samachepa ndi mazira ake,” maana yake:

"bila kujali jinsi udogo wake, (hummingbird-ndege) yuko tayari kupambana, jino na msumari kwa ajili ya usalama na umiliki wa mayai yake".

soma zaidi hapa: https://www.nyasatimes.com/malawi-a...-protecting-lake-malawi/#sthash.EbZZlIR6.dpuf[/QUOTE
hujui kusoma kingereza
 
Tumechoka na Maneno yao, tunataka vitendo sasa, kama wapo tayari waseme, tunaweza kurusha Bomu sisi wenyewe upande wetu wa Tanzania ili tulianzishe tu, maana kuna namna nyingi ya kutangaza vita,

Sasa tunataka vitendo, hivi huyo Mutharika anajipenda kweli?
 
Achana nao wasikupe weenge..... maswala ya ulinzi wa taifa ni nyaraka nyeeti..... wanachokitangaza ni tofaut na walichonacho....

Ni state ndogo saana malawi kiuchumi.. kijeshi... kiteknolojia hadi kiakili....

Ukirudi kwenye historia... mizozo na mikwara ya malawi juu ya ilo ziwa ni muda mrefu saana anaongeaga..... action ni haba...

Uzuri ni kwamba eneo lipo kwenye mipaka. Na nina imani mipaka yoote huwa inalindwa...

Achana na the press.... kuna watu wapo kwa ajili ya amani yako... vuta gambe ponda monde.... tanzania tuko imara.
 
Hivi sehemu ya ziwa inayoingia Msumbiji nayo wanadai au ni yetu tu au sisi wanatuonaje, wakamuulize Iddi Amini awape salaam.
Eneo la ziwa wanalo lilia ni la kwetu (kaskazini mashariki), kwa kifup hawana chao mjomba.
Kwa watu wa msumbiji wenyewe huwashangaa Wamalawi wanavyo jiona kuwa wao tu ndio wenye hati miliki na ziwa hadi kulibadili jina na kuliita Ziwa Malawi.
 
Ni kweli tulisign mkataba OAU kuwa nchi zote za afrika tuheshimu mipaka ya mwisho tuliyoachiwa na wakoloni na mpk wetu wa mwisho ulikuwa unaonyesha ziwa lote la malawi km ni kosa analo Nyerere kwa kusign makubaliano yale wakati mpk uliwapa ziwa lote malawi. Nadhani Nyerere hakutaka kuonekana mkorofi ukizingatia alikuwa mwanaukombozi mpenda amani. Kinacjotakiwa ni kuwabembeleza tu tukienda mahakama yoyote tunashindwa ndio maana maongezi na malawi yameimarika hasa kuanzia kipindi cha mkapa lkn mambo hayakukamilika baada ya bakili muluzi kutoka madarakani. Baadae mazungumzo yakaendelea lkn hayakuzaa matunda mpk waingereza walipogundua mafuta kuvuka nusu ya ziwa kuelekea kwetu mgogoro ukaibuka upya lkn kisheria ziwa ni lao 100%
Mmh, we nayee
 
Kama ni haki yao wapewe. Ubabe na maneno ya fedhuli hayasaidii
Wapewe nini !!??umesoma hii mada inahusuni nini !!??yaani wilaya za kyela na Nyasa zisitumie hilo ziwa ni mwendawazimu tu ndie anaweza kufikiria hivyo Banda katika uhai wake enzi hizo alijaribu hata kutaka njombe kyela na rungwe ni maeneo yake alishindwa.
 
Wanajamvi hili swala la mpaka wa ziwa Nyasa kati ya TZ na Malawi tusilichukulie lelemama, kwani wenzetu wako serious zaidi ya tunavyofikiri.

Kwa lugha yao wamesema hivi: “Timba samachepa ndi mazira ake,” maana yake:

"bila kujali jinsi udogo wake, (hummingbird-ndege) yuko tayari kupambana, jino na msumari kwa ajili ya usalama na umiliki wa mayai yake".

soma zaidi hapa: https://www.nyasatimes.com/malawi-a...-protecting-lake-malawi/#sthash.EbZZlIR6.dpuf

Kwani mbona kila mtu ana kipande chake, afterall ziwa linalindwa na Mungu
 
Magufuli hana tofauti sana na Nyerere... Wakijaribu kufanya alichofanya Idd Amin atafanya tu kama alivyofanya Nyerere. Kama wanajiamini basi waambie waje, tena waje na rafiki zao wanaowashika masikio.
 
Ingekuwa ni Kagame kichwa maji ingekuwa pengine ameshaanzisha vita au amesha waua wale viereere
 
Back
Top Bottom