Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kwa upande mmoja nakubaliana na Lema na hoja ya udhaifu wa serikali na polisi maana wangekuwa wanatenda haki nadhani angeozea jela saa hizi. La pili siku nyingi nimeandika wachaga ni Mafia na iko siku wataiingiza hii nchi kwenye machafuko makubwa kwa tamaa ya ulaji na sio kuongoza nchi. Nilimwambia Slaa hao wachaga ni Mafia yamempata ya kumpata na sasa namwambia Lowassa atake care. La tatu inawezekana wamemuua wenyewe kutengeneza matukio kwani ndio dili la hili chama
Kamanda Mawazo kauawa na Polisi na inajulikana,najiuliza hivi hawa Polisi wetu ni Watanzania?na kama ni Watanzania wanapigania nini?nasema wazi watatumaliza wote ili wabaki wenyewe,lakini kabla hawajatumaliza haki itachukua mkondo wake na ndipo Taifa langu Tanzania litainuka kutoka kwenye mavumbi,Mungu M;laze pema Kaka yangu Kamanda Mawazo!
 
umeandikwa kwa uchungu na ni kama dua la kuku

wengi wanauwawa kila siku nchi hii

tuchukue hatua na si kusema tu aple watu wetu wa karibu wanapokufa

Mimi naumia na wanaukawa wote, Lakini hapa nalaumu uongozi wa Ukawa. CCM tunaijua,Polisi tunawajua.Hawa ni damu na nyama. Watatoa taarifa kuwa Mawazo ameuawa na watu kutoka Rwanda au Burundi! Nani asiyejua hili?

Viongozi wa CCM wanawakilisha tabaka la matajiri na wanatumia mbinu zote kufanikisha.Hawalii hawamlalamikii mtu, wanapanga wanatenda. Sisi mwisho hata wake zetu watatuona wajinga, Tunaibiwa kura tunamwita Mungu,tunawekwa ndani tunamwita Mungu, Tunauawa tunamwita Mungu!

Jamani Mungu yuko Iraq huko anasaidia hali ni tete huko.Hebu hapa tujisaidie wenyewe!
Tusimsumbue Mungu kila kitu, hata mambo tunayoyaweza tunamuitia ili nini?

Mbowe unatuangusha kamanda!
 
Chacha Wangwe alikufa wapambe mlikaa kimya wala hamkutoa matamko mengi mengi. Si mwenyekiti wala katibu walioonyesha kukerwa na kifo kile. Na yule aliyekuwa anamuendesha mkampa uanachama bila hiyana. Kiukweli lawama zilizopo ni kuwa chama kilimshughulikia. Kila mtu ana mawazo hayo.

Angevamiwa na kushambuliwa kisha kuuwawa tusingenyamanza,au angekufa akiwa anahojiwa na vigogo wa chama kama Kolimba alivyokufa mbele ya meza akihijiwa na vigogo wa CCM tusingenyamaza,tungepaza sauti mpaka Mbingu ya saba wangesikia.Lakini Chacha Wangwe(RIP)alipoteza maisha kwa ajali ya gari,policcm walichunguza chanzo cha ajali,kesi ilipelekwa mahakama za CCM na uamuzi ulitolewa.Zilaumu MAHAKAMA zako kwa kushindwa kuhusisha ajali hiyo na mambo ya siasa kama unavyotaka kutuaminisha,pumbavu.
 
Pamoja na kwamba nimesikitishwa na kifo cha kikatili cha ndugu Mawazo lakini sikubaliani na hii tabia ya kupeana tuhuma. Wananchi wengi tunahisi huenda kifo cha mawazo kimesababishwa na mgogoro wa dhulma humo humo ndani ya CHADEMA; Wengine wanasema huenda ni migogoro binafsi kati yake na jamaa zake. CHADEMA mnasema kifo chake kimepelekewa na green guard kumvamia marehemu na wengine mnasema polisi ndio wamemuua. Sasa tushike lipi!?

Aidha, mbona kifo cha Chacha Wangwe hatukuona watu kuguswa hivi!? Wakati kilijaa giza zito na hadi leo haieleweki nini kimemuua Chacha Wangwe. Ndugu Lema kama unajua kuhusu Wangwe tugusie kidogo. Huenda ikatoa mwanga wa kujua kuhusu kifo cha Mawazo. Natazama kwa jicho la tatu tu.

RIP Mawazo

yani katika watu ambao wa hovyo ni wewe we una uhakika gani unayo yasema jamani jamani tuache siasa za kipumbavu kwenye mambo ya msingi lumumba sijui wanakupa nini hadi unaandika ujinga huu ipo siku tutachoka bora mtuue wote mbaki lumumba peke enu ili mtawale vizuri yani bongo ukiwa mpizani ni shida da.
 
Afande mkoa wa Geita:

kuna tukio la mauaji KTR/IR/1186/2015, lililotokea leo tarehe 14/11/2015 baada ya ALPHONCE S/O MAWAZO, miaka 39, msukuma, mkulima mkazi wa Geita na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita pia katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa mgombea ubunge jimbo la Busanda, alishambuliwa kwa silaha za jadi na watu wanaosadikiwa kuwa zaidi ya kumi kati yao mmoja ametambuliwa kwa jina moja la MABEGA, wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CCM.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa CHADEMA walikuwa na mkutano wao wa ndani katika mtaa wa Ludete A kata ya Ludete katika mji mdogo wa Katoro na CCM pia walikuwa na mkutano na ndani katika ofisi ya CCM, mtaa wa Njiapanda kata ya Ludete, vyama vyote viwili vilikuwa vinaandaa na kuwaapisha mawakala wao kwa ajili ya uchaguzi wa diwani ambao utafanyika kesho tarehe 15/11/2015 katika kata ya Ludete.

Wakati mkutano wa chadema ukiendelea majira ya 12:35 hrs mwanachama mmoja wa CHADEMA alitoa taarifa kuwa nje ya ukumbi kuna watu wanaosadikiwa kuwa wanachama CCM wanarekodi mkutano wao. Baada ya taarifa hiyo wajumbe wote walitoka nje ya ukumbi wakakutana na kundi la hilo nje ya ukumbi. Watu hao waliwashambulia kwa silaha butu 1. ELIZABERT D/O PASCHAL, miaka 43, msukuma, mkulima wa Katoro ameumia kisogoni 2. BAHATI S/O MICHAEL, miaka 38, mzinza, mkulima mkazi wa Katoro, amejeruhiwa kichwani. Wametibiwa kituo cha afya Katoro, wameruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. Kutokana tukio hilo wajumbe wote wa CHADEMA walitawanyika.

Marehemu alitoweka katika eneo hilo katika mazingira ambayo hata wenzake wameshindwa kuyaelezea. Muda mfupi alionekana akipigwa katika umbali unaokadiliwa kuwa nusu kilometa kutoka ukumbi ulipokuwa unafanyika mkutano wao na watu kumi walioshuka kwenye gari aina ya Land Cruiser ambayo namba zake bado hazijafahamika. Baada ya tukio hilo gari hilo lilielekea barabara ya Geita mjini.

Majeruhi alifariki majira ya saa16:00 hrs wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya Geita.

Upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaemdelea kuwatafuta watuhumiwa.

Duh eeh Mungu uturehemu, jeshi la polisu lichukue hatua stahiki kwa wote waliohusika na kitendo hiki.
 
Kwa upande mmoja nakubaliana na Lema na hoja ya udhaifu wa serikali na polisi maana wangekuwa wanatenda haki nadhani angeozea jela saa hizi. La pili siku nyingi nimeandika wachaga ni Mafia na iko siku wataiingiza hii nchi kwenye machafuko makubwa kwa tamaa ya ulaji na sio kuongoza nchi. Nilimwambia Slaa hao wachaga ni Mafia yamempata ya kumpata na sasa namwambia Lowassa atake care. La tatu inawezekana wamemuua wenyewe kutengeneza matukio kwani ndio dili la hili chama

CC: OLESAIDIMU wenzako hao
 
Last edited by a moderator:
Polisi wawe wa kwanza kulipotiwa the hague upendeleo wao ndo unaoleta haya
 
Hivi unawezaje kuchukua madaraka kutoka kwa watawala wa nchi za africa kwa wepesi namna hiyo.

Naona unarudi kwenye sense ,sasa kumbe niliposema viongozi wa ukawa watoe tamko kieleweke ,hukuelewa nini ??
 
kwa watu waliosoma physics watajua ni law of motion by Isaac Newton.
Natoa pole kwa watanzania wote waliopatwa na majanga na mabalaa adi kupoteza maisha.
hoja yangu:::
mh Lema ndio alikuwa role model wa kamanda mawazo. Lema kwa kauli zake anajenga uadui wa kutisha ili apate cheap popularity. ametoa madai mazito kuwa polisi Arusha walitaka kumuua. haingii akilini polisi wapo kisheria kulinda amani na usalama wa RAIA.
sasa kauli hizi za Lema za chuki,vitisho,kebehi,dharau,jeuri kwa jeshi la polisi anajua impact yake? mfano Lema akavamiwa na majambazi hatuombei asilani, je kwa kauli hizi kuna askari atakae kimbilia eneo la tukio kusaidia?
conclusion
EVERY ACTION HAS EQUAL AND OPPOSITE REACTION. LEMA ACHA SIFA ZA KIJINGA KWA KAULI ZAKO IT WIL COST U ONE DAY! MARK MY WORD.

Lema hana akili ya kuelewa hayo unayo andika ! mark my words !
 
Mawazo umeuwawa ? Kosa lako ni kuwa Chadema na kufanya Siasa ? Mkuu wa Wilaya ya Geita atafurahi sasa , kwani alishawahi kutamani kuona maiti yako na leo ameshuhudia ,Rafiki zako tunatafakari kwa kina na Uchungu mkubwa .

Ni heri Vita inayotafuta Haki na Usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha Utu wa Binadamu.

Nilikuwa nakupenda sana Mawazo .

Godbless Jonathan Lema

maji siku zote hujitenga na mafuta kama uongo unavyojitenga na ukweli.Dhuluma zina mwisho, Usiijali Mheshimiwa LEMA hata kama watakuwa wamefariki siku ya ukombozi tutafukua na kuchoma moto mifupa ya waovu hawa!
 
Hama kitu hapo usijidanganye.

Yawezekana uko sahihi lakini mwenyekiti wa chama, aliyekuwa mgombea, anasemekana alikuwa ni moja ya engine za chama kanda ya ziwa. . . .,. .

Mazingira ya hilo tukio na hizo sifa hapo juu mbona vinakataana sana??!!!
Watu wa aina yake wanalindwa na taasisi zao??!!
Wanapewa ABC za nyakati na mienendo yao??!!

Au wakishapotea kama hivi ndio wanasifiwa na mambo meengi hutajwa juu yao??!!!
 
Hebu weka hoja kama kichwa kina mawasiliano na unayoyafanya. . .

Hiyo ndiyo mizigo kama wewe, temana nayo rudi kwa topic.

Kwanini mmeamua hivi au mnakula nyama za watu ktk awamu hii ya 5?
 
kila ajuaye Mungu, aombe kwa Lugha yake,
Taifa lina uchungu,limetokwa mwana wake.
kauawa kwa marungu,kwa mapanga na mateke,
nenda kamanda MAWAZO.

Ilikuwa ni Kalenga, kwenye ngome ya Mkwawa
kwenye ule mtananga, uchaguzi kurudiwa,
hoja ulizifinyanga, kwa lugha yako muruwa,
Tutakukumbuka!

wametoa roho yako, mabazazi hapa kazi,
wana sifa mbwa koko,ama za paka majizi,
na zinakuzwa waliko,na makada viongozi,
Damu yako inawalilia.

Polisi siyo wepesi, kwenye hiki chama chao,
wao na wao watesi, kwa uchwao na uchao,
hawanayo hiyo kasi,daima ni ukachao
Yana mwisho.

Imekuwa ada yao, hao wana wa kijani,
si wangindo si wayao,wana roho za majini,
usikae mbele yao,kwani hawana imani,
wana deko la wazazi.
 
Back
Top Bottom