Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kaka yangu Godbless Lema.

Asante kwa ulichokiandika. Inawezekana kina ukweli na inawezekana hakuna ukweli. Naomba kutosimamia kile ambacho sina hakika nacho.

Naomba kaka Lema na watanzania wenzangu tutambue kuwa kuna maadui wa nchi yetu wa ndani na wa nje. Maadui hawa kwa maslahi yao wanatamani kuona Tanzania sio kisiwa cha AMANI.

Maadui hawa wengine ni majirani zetu. Hivyo kaka Lema tunahitaji kushikamana na kuliombea Taifa letu. Inawezekana kabisa waliofanya uhaini huo kwa ndg yetu sio CCM bali ni maadui wa nchi hii na wana malengo maovu kwa Taifa hili.

Naamini sana ktk nguvu ya mshikamano wa ki Taifa. Aidha wale waombaji tuendelee kuliombea Taifa. Tunapoomba tusihukumiane wala kutuhumiana. Mkono wa Mungu unaweza kuwafikia waovu ktk nchi yetu.

Poleni kwa msiba wapendwa.

Queen Esther

Alikuwa kijana aliyeamini katika Mabadiliko, alitembea Nchi nzima kwa shida kujenga ufahamu kuhusu Ukweli, Haki na Usawa. Ameuwawa akiwa akitoka kwenye kazi za Chama chake, akavamiwa, akapigwa na baadae kufariki. Ni nani amefanya kitendo hiki?

Watu wengi mnalaumu Wanachama wa CCM kwani ndio waliofanya kazi hiyo, hapana, mnakosea. Mawazo ameuwawa na mfumo wa Serikali na Jeshi la polisi unaojali ukatili na uovu. Mauaji yataendelea sana, kwani wengi wamekishauwawa na kuumizwa bila Serikali kuchukua hatua.

Polisi wanaowajibika kwa utawala unaojali ukatili, ubaya, na uovu ni lazima watamsaidia Shetani kufanya kazi. Polisi wanaoshindwa kukamata wahalifu na na kuwajibisha wahalifu, wao ndio wanaosaidia Taifa hili kuingia Vitani, Matukio ya Green guard kuvamia na kujeruhi na hata kuua ni mengi katika Taifa hili, Wahalifu wanalindwa na sasa wana ujasiri wa kufanya wanavyotaka. Sioni siku nyingi za Amani Tanzania, magari ya kuwasha na silaha za moto zitashindwa kupambana na Umma uliojawa hasira na Uchungu, propaganda pia zitashidwa kutengeneza hali ya usalama, masikitiko yangu ni kuwa hali hii itamkuta kila Mtu aidha ni mwenye haki au ni asiye na haki. Usalama wa Nchi haujengwi na wingi wa silaha wala wingi wa Askari, Isipokuwa utawala unaojali Haki na Usawa.

Uhalifu wa namna hii katika Taifa hili unajengwa na Polisi walioshindwa kazi zao kwa kuzingatia Uadilifu na Sheria za kazi, Kamati za Siasa za Chama Tawala ndio zinatoa maelekezo ya utendaji wa Jeshi la Polisi. Kwa mfano hapa Arusha RPC ni mdau namba moja wa CCM na hivi karibuni katika vikao vyake vya kampeni ya kumsaidia mgombea Ubunge wa CCM alichokaa na Viongozi wa bodaboda alitoa maelekezo mabaya na ya uharibifu dhidi yangu, unafikiri nini? Ni lazima Vijana hawa kama watakosa Utu, wanaweza kufanya uhalifu mbaya sana kwangu, kwani anayepaswa kulinda amani ndiye anayesimamia Mipango mibaya ya uhalifu.

Mambo haya ni lazima yafike mwisho. Polisi mnapaswa kuwa na hekima sasa na mtambue kuwa hali ya Usalama Nchini haiko salama, Watoto wenu, Wazazi wenu, Wake zenu na familia zenu ziko Mitaani, Ukatili na Uonevu unapoongezeka kwa Watu wanyonge, ndivyo hivyo Watu hawa wanaanza kufikiria njia mbadala ya kujitetea, naona Binadamu wa Tanzania anaanza kuelekea huko.

Ni nani anafuata baada ya Mawazo? Ni vita ya kujilinda au kukubali kuwa Maiti kwa njia ya mapanga na vipigo? Tulitafakari jambo hili wote, kwani Utulivu huu tulionao hauna muda mrefu kutoweka na ndipo Nchi yetu itakuwa Nchi ya Ukiwa.

Moyo wangu umeumia na kuchoka sana nahitaji msaada zaidi, Ni Kijana rafiki mzuri niliyemuingiza kwenye Siasa, nilimpa Suruali, Mkanda, na Koti wakati ninampleka kumtambulisha kwa ajili ya kura za maoni kwenye Chama cha Tlp wakati huo, tuliishi wote na familia zetu zikapendana sana, hakuwahi kuwa mnafiki juu ya anachokipigania.

Mawazo umeuwawa? Kosa lako ni kuwa CHADEMA na kufanya Siasa? Mkuu wa Wilaya ya Geita atafurahi sasa, kwani alishawahi kutamani kuona maiti yako na leo ameshuhudia, Rafiki zako tunatafakari kwa kina na Uchungu mkubwa.

Ni heri Vita inayotafuta Haki na Usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha Utu wa Binadamu.

Nilikuwa nakupenda sana Mawazo.

Godbless Jonathan Lema
 
Jamani Mbona hakuna anayeeleza kisa cha yeye kuvamiwa? Yeye kama mwananchi anaweza tenda kosa kwahiyo msikimbilie kwenye nafasi yake bila kueleza mkasa mzima.

Ni akili mbovu kuyaandika hayo. Kwa hiyo nawewe ukikosea adhabu stahiki ni hii kwako ya kupigwa mashoka na mapanga??
 
YATQKUWA KAMA YA MWandishi MWANGOSI NA DR ULIMBOKA CCM HOVYO KABISA LAZIMA NCHI INAHITAJI UKOMBOZI HUU NI UHUNI
Hawa wauaji watapewa nafasi zipi serikalini? Aliyesimamia tukio la Mwangosi alipandishwa cheo kazini kwake,yule wa Dr Ulimboka naye kaula, nafasi za teuzi za Rais ziko mlangoni,naona watu wanapandisha CV zao.
 
anaye amin kuwa mawazo kauwawa na ccm anajiliwaza buree.....waliomuondoa ni polisi hakika...
lema kasema ukweli

So Polisi wameamua tu kumuua Mawazo bila sababu yoyote?
 
Tumeirekodi hii !

Ungekuwa na akili ungefikiria zaidi ya hapo ujue kinachojengeka ktk akili za watu ni nini lkn kwa sababu wewe ni zaidi ya andazi unachoelewa ni ujinga TU
 
Unajua ukawa nyie ndo wauaji wakubwa kila kukicha mlikuwa mnakamatwa na mapanga na kuvamia watu na kuwapiga mfano rafiki wa mosha mlimpiga nusura afe sasa mmeona na nyie tumewageukia sasa mmeanza kulialia si mlianzisha wenyew sasa tumeendeleza
 
Hii haikubaliki ....hii lazima ifike mwisho ....

Ndo ulichopigania kwa miezi yote ya kampeni mkuu. At last tunaanza kupata matunda. Kwa CCM inakubalika na hutasikia hata mtu mmoja amekamatwa it'll be like nothing have happened. Hongera kwa kuirudisha CCM madarakani
 
Kuna mijitu humu ilichekelea sana mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza alivyouliwa kule kisesa, sasa hayohayo eti yanalaani,

nilidhani mtampongeza kuwa kafa kishujaa, munafuga ugonjwa wenyewe sasa munaota matende, tulishasema hii biashara sijui kulinda kura sijui green guard iko siku itawatokea puani.

Leo lema kamwona mawazo hao wengine hajawaona? Au kwa kuwa hajawapa magwanda?

Kwa hiyo kama walichekelea kanyaga twende hakuna cha kufanya. Dunia hii ina Mizigoo.
 
Tunahitaji viongozi wa kisiasa wenye uwezo wa kujenga hoja na sio wenye kuijaza chuki jamii...!

Wako baadhi ya wenye dhamana ya ulinzi wa jamii wakishirikiana na wanasiasa au wafanyabiashara wa madini wanaendesha mauaji ya kikatili dhidi ya jamii mfano albino.

Hili ni tatizo msingi linalotakiwa kushughulikiwa.Nilidhani Lema unaliongelea hili.

Maoni yangu ni kuwa na utulivu na uvumilivu wa hali ya juu kama kiongozi kwani ubaya hulipwa kwa wema zaidi...!!!

Mtu kama wewe damu kama hizi zinafaa upakwe utembee nazo mpaka utakapokufa na wewe.
 
Aliyemkata kichwa mwenyekiti wa CDM Arumeru kwa chainsaw alitoroka mikononi mwa polisi na mpaka leo imebaki story,
Ni uoga upi utakaowapata makada wa CCM waache kuua wengine kwa kosa la kuuanga mkono CHADEMA?
 
?hadema zisaidieni familia na wawekeni katika kumbukumbu kwa wale ambao hama wamepata ulemavu au kifo kutokana na sababu pengine walipokuwa wanatekeleza majukumu ya itikadi zenu
 
Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya 4 ndiye wa kulaumiwa siku zote za vurugu la amani ya Tanzania kwakuwa yy ndiye muanzilishi wa mauwaji ya ndg zetu na viongozi wanaotetea haki zetu kwa kauli yake ya hadharani bungeni, wapigwe tu, yy akiwa km mtu mwenye dhamana ya uongozi wa juu serekalini amehalalisha kuuwawa kwa watu watafuta haki wasiokuwa na ulinzi km yy. Mungu atakuhukumu hukumu isiyo na huruma km kauli zako.
 
Godbless J Lema natambua kama ilivyo kwa wengi wewe pia umeguswa sana na kifo cha Alphonce Mawazo hivyo naomba nitoe pole kwako na kwa wengine wote. Lakini, kwako Lema, unapaswa kuwa makini sana mwanangu na matamko uyatoayo kwani ghalama yake unaweza ukashindwa kuilipa.
Kama madai yako yatakua na ukweli basi elewa kuwa hapo mlengwa hakuwa Mawazo nali wewe. Mawazo ilikua ni kete tu ambayo wataalam wa saikolojia ya mwanadam walijua ikichezwa ile kete tu, basi wewe utakuwa triggered na kulipuka. Ni kama draft unapewa kete, unakulwa watu wanakupiga double mpaka King (tamka kingi).
Ulihitaji sana msaada wa kusheria kabla ya kutoa madai yako. Kama siyi msimamo wa wana Arusha basi leo hii ungekua umekighalimu cha chako ila kwasababu ya msimamo wao basi wasiwasi wangu ni sijui kama utarudi bungeni, maana kauli zako ndiyo zitatumika dhidi yako katika kipindi hiki na na kama ujuavyo Arusha inahitajika kwa namna yoyote ile 'dead or alive'. Msipuuze sana nguvu ya wapinzani wenu maana wapo tayari kutumia ushauri wowote ule ili mradi ushindi upatikane.
Mbatia alimtaka mgombea wa CUF ajitoe, mimi ninashauri asijitoe, abaki kama backup. Nikirudi kwa Lema jaribu sana kuepuka kuwa too emotional ingawa kwa uliyoyaandika yamesomeka na sidhani kama yatafutika


umeongea kwa hekima nyingi sana, umesomeka vema
 
Last edited by a moderator:
Hivi Godbless Lema unapokuwa unaandika huwa unakuwa umelewa, umevuta bangi au huwa unakuwa ndotoni?

Mlipomuua Chacha Wangwe mlisingizia Ccm na Polisi. Leo mmemuua Mawazo unakurupuka tena na kulihusisha Jeshi la Polisi. Cha kushangaza hutoi sababu za kwanini polisi wanahusika zaidi kupiga porojo.

Ni polisi hawa hawa ambao mnawadhihaki kila kukicha na ambao wamewalinda kwenye mikutano yenu yote ya kampeni lakini leo mnawazushia uongo wa wazi kabisa.

Hivi kifo cha Mawazo kina uhusiano gani na kununuliwa kwa magari ya Polisi? Au unataka kutuaminisha kuwa magari hayo ndio yaliyomuua?

Lema mkeo ni mtu makini sana na ana busara na hekima ya hali ya juu hebu uwe unamuomba ushauri wakati fulani kabla hujaandika mambo haya. Kwake naamini ni fedheha kubwa sana. Badilika kaka.
 
Back
Top Bottom