Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Daaa hata siamini,chozi lanidondoka hapa.Mawazo kweli!eee mungu tupe cha kukifanya.
 
Hii haikubaliki ....hii lazima ifike mwisho ....

Unaongea kinyume au unatukejeli? Ninyi hamna cha kuhofia mpo salama kwa msaada mlioutoa kipindi chote cha kampeni...kwa sasa Endeleeni tu na operation zinduka.
Achaneni na sisi wafu, tutaombolezeana na kuzikana wenyewe.
 
Inaumiza sana,huu ni ukatili wa kupindukia
 
Jamani geita tunaomba mambo mawili 1.polis I watwambie waliouwa ni wakinanani na wapo wali kwa maagizo ya Mani 2.ccm watwambie huko geita jambo hili ni kweli vijana wao wsmehusika? Vinginevyo ccm,polisi tunaishi nao mtaani niwakumbushe tu ccm vita ya kisiasa tukianza ni nchi nzima ukiniona Chadema halali yako nikikuona ccm sikuulizi makamanda siowakati wakulialia Hawaii ccm tunaomtaani majiranizetu kamatulivoumia sisi dhidi ya kamanda wetu mawazo na ccm wataumia mioyo Tao maradufu kwa dhambi hii torati inasema jino kwa jino

watakuanzia wewe ohoo shauri yako
 
Lema, i think kwa hili umewahi sana kutoa tamko.... Bado hujawa mbunge and anything can be done to stop you contesting

jaribu kubana pumzi kidogo tu ili upate nguvu zaidi ya kusukuma gurudumu

Ndo zake huyo ! Redio za Arusha zote zinaogopa kumpa 'live air time' maana anaweza kukutia kwenye matatizo usiyoyategemea !
Hachagui maneno, hana busara, hana subira na ni mpenda uchochezi.
Lema ana dalili zote za uhalifu !
 
Pole Kamanda Lema,M.A.P Alphonce Mawazo ,Polisi na Green Guards kuweni Makini acheni kutumika mtasababisha uvunjifu wa Amani nchini.
 
Last edited by a moderator:
Alikuwa kijana aliyeamini katika Mabadiliko , alitembea Nchi nzima kwa shida kujenga ufahamu kuhusu Ukweli ,Haki na Usawa . Ameuwawa akiwa akitoka kwenye kazi za Chama chake ,akavamiwa , akapigwa na baadae kufariki . Ni nani amefanya kitendo hiki ?

Watu wengi mnalaumu Wanachama wa ccm kwani ndio waliofanya kazi hiyo , hapana, mnakosea . Mawazo ameuwawa na mfumo wa Serikali na Jeshi la polisi unaojali ukatili na uovu . Mauaji yataendelea sana , kwani wengi wamekishauwawa na kuumizwa bila Serikali kuchukua hatua .

Polisi wanaowajibika kwa utawala unaojali ukatili ,ubaya,na uovu ni lazima watamsaidia Shetani kufanya kazi . Polisi wanaoshindwa kukamata wahalifu na na kuwajibisha wahalifu , wao ndio wanaosaidia Taifa hili kuingia Vitani, Matukio ya Green guard kuvamia na kujeruhi na hata kuua ni mengi katika Taifa hili, Wahalifu wanalindwa na sasa wana ujasiri wa kufanya wanavyotaka . Sioni siku nyingi za Amani Tanzania , magari ya kuwasha na silaha za moto zitashindwa kupambana na Umma uliojawa hasira na Uchungu, propaganda pia zitashidwa kutengeneza hali ya usalama , masikitiko yangu ni kuwa hali hii itamkuta kila Mtu aidha ni mwenye haki au ni asiye na haki. Usalama wa Nchi haujengwi na wingi wa silaha wala wingi wa Askari , Isipokuwa utawala unaojali Haki na Usawa .

Uhalifu wa namna hii katika Taifa hili unajengwa na Polisi walioshindwa kazi zao kwa kuzingatia Uadilifu na Sheria za kazi , Kamati za Siasa za Chama Tawala ndio zinatoa maelekezo ya utendaji wa Jeshi la Polisi . Kwa mfano hapa Arusha Rpc ni mdau namba moja wa ccm na hivi karibuni katika vikao vyake vya kampeni ya kumsaidia mgombea Ubunge wa ccm alichokaa na Viongozi wa boda boda alitoa maelekezo mabaya na ya uharibifu dhidi yangu , unafikiri nini ? Ni lazima Vijana hawa kama watakosa Utu , wanaweza kufanya uhalifu mbaya sana kwangu , kwani anayepaswa kulinda amani ndiye anayesimamia Mipango mibaya ya uhalifu .

Mambo haya ni lazima yafike mwisho . Polisi mnapaswa kuwa na hekima sasa na mtambue kuwa hali ya Usalama Nchini haiko salama , Watoto wenu ,Wazazi wenu , Wake zenu , na Familia zenu ziko Mitaani , Ukatili na Uonevu unapoongezeka kwa Watu wanyonge , ndivyo hivyo Watu hawa wanaanza kufikiria njia mbadala ya kujitetea , naona Binadamu wa Tanzania anaanza kuelekea huko .

Ni nani anafuata baada ya Mawazo ? Ni vita ya kujilinda au kukubali kuwa Maiti kwa njia ya mapanga na vipigo ? Tulitafakari jambo hili wote , kwani Utulivu huu tulionao hauna muda mrefu kutoweka na ndipo Nchi yetu itakuwa Nchi ya Ukiwa.

Moyo wangu umeumia na kuchoka sana nahitaji msaada zaidi , Ni Kijana rafiki mzuri niliyemuingiza kwenye Siasa , nilimpa Suruali , Mkanda, na Koti wakati ninampleka kumtambulisha kwa ajili ya kura za maoni kwenye Chama cha Tlp wakati huo , tuliishi wote na familia zetu zikapendana sana , hakuwahi kuwa mnafiki juu ya anachokipigania .

Mawazo umeuwawa ? Kosa lako ni kuwa Chadema na kufanya Siasa ? Mkuu wa Wilaya ya Geita atafurahi sasa , kwani alishawahi kutamani kuona maiti yako na leo ameshuhudia ,Rafiki zako tunatafakari kwa kina na Uchungu mkubwa .

Ni heri Vita inayotafuta Haki na Usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha Utu wa Binadamu.

Nilikuwa nakupenda sana Mawazo .

Godbless Jonathan Lema
Msituambie utumbo hapa makamanda. Mbona alivyokufa Chacha Wangwe hamkutoa macho kama haya. Mbona hamkutoa statement nyingi nyingi kama hizi. Au mlimuua nyinyi nini? Kwa hiyo mkawa mnajishuku.
 
Honestly huu uzi umenitoa machozi. Godbless J Lema umeandika kwa uchungu sana,umenikumbusha mengi na hasa haki yetu iliyoporwa kimabavu.
Nimetazama wino ambao bado upo kwenye kidole changu tokea October 25 nikashikwa na hasira sana.
Yote haya yana mwisho.....
R.I.P kamanda Mawazo.

Huo wino au kovu? Hebu kafanye Check up mama.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza wewe Lema ile kazi yako ya zamani imesababisha wanawake wengi kuwa wajane na watoto kukosa malezi ya baba. Tunakujua kuwa ulikuwa jambazi. Hivyo hatushangai kukuona una chuki na polisi wetu.
 
Chacha Wangwe alikufa wapambe mlikaa kimya wala hamkutoa matamko mengi mengi. Si mwenyekiti wala katibu walioonyesha kukerwa na kifo kile. Na yule aliyekuwa anamuendesha mkampa uanachama bila hiyana. Kiukweli lawama zilizopo ni kuwa chama kilimshughulikia. Kila mtu ana mawazo hayo.
 
Ni bahati mbaya sana kuwa na mtazamo kama wako juu ya jeshi la police,
najua hata wewe Leo hii ikitokea ukadhulumiwa haki yako kituo chako cha kwanza ni jeshi la police ili kudai haki yako.

Kwa nini ktkt hili unatutaka tushindwe kuliamini jeshi la police?

NAAMINI JESHI LA POLICE LITAFANYA KAZI YAKE VIZULI NA KWA WERED ULIOTUKUKA
NA KUWAZIBA MIDOMO WOTE WENYE MTAZAMO KAMA WAKO.
Labda huyo bwana mimi huwa sijihangaishi na polisi labda mtu yeye ndo anipeleke polisi ni wajinga sijui kwa kuwa wanatii amri nilikuwa natamani kuitumikia jwtz ila mambo yanayoendelea naona ni upuuzi. mwanadamu huwezi kuwa controled kama mashine au robot. pamoja na kupaswa kutii amri za wakubwa wao ila kuna wakati inabidi utumie utashi wako hilo ndo dhumuni la mungu kutupa ubongo fanya right decision individualy umewahi kuona kipigo ambacho polisi hushusha wakikamata watu kwenye maandamano?? huwa najiuliza hawa wanapiga wenzao hivi hebu wavae viatu ndo wangekuwa wao au ndugu zaa wangehisi vip
 
Siasa zimetupeleka kuwa watu wa chuki na visasi...hakuna kuangaliana kwa jicho la kawaida kwa mtu wa chama tawala na upinzani,na zaidi punde tutaona malipizo yasiyo na kikomo....ninaona siasa za chuki zikikomaa kwa sababu ya HAKI kuporwa
 
Tuitumie siku ya leo siku ya bwana kuliombea taifa letu ili haya makovu yanayoendelea yapate ufumbuzi kupitia vyombo vyetu vya dola.
 
wewe si unaushaidi wa Lema kuwa jambazi? kwanini asishitakiwe akafungwa? mkubwa ebu elimika kidogo!, nafikiri hata shule ya kata umefika!

Massawe ni mwizi na Jambazi , lakini hajawahi kufungwa ! kuna wale wanaitwa kaa Chonjo..........Kileo.......... wachaga tu ! itabakia hivyo
 
Back
Top Bottom