Kamanda Mambosasa na Jeshi la Polisi wasaidieni wananchi wa Kitunda Nyantila katika wimbi hili la uporaji

Coster2

Senior Member
Apr 28, 2019
168
218
Inasikitisha sana kuona watanzania wenzetu wakiishi maisha ya hofu kana kwamba hawapo nchini mwao, kule Kitunda kuna sehemu inaitwa Nyantila ambapo maduka zaidi ya 20 yamebomolewa na kuibiwa siku tatu zilizopita.

Na yakaporwa tena jana, vijana wanapora adharani na wanaogopwa, watu wanakabwa saa 2 usiku, wafanya biashara wanalazimika kufunga biashara mapema kuogopa hayo makundi ya uporaji, kuna sehemu inaitwa Sabato na sehemu inaitwa Pentagoni wananchi wanaishi kwa hofu sana.

Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua kuwasaidia wananchi wa yale maeneo.juzi watu nane wameporwa simu na pesa , tunaomba mamlaka husika msaidie kuhusu hili, tension ya yale maeneo ni kubwa sana, hofu ipo juu sana.
 
Waporaji wanafahamika ila wanaogopwa. Seriously this is not serious.

Hivyo vipanya road kwanini vinawasumbua sana hapo Daslam? Mnashindwa kujipanga hapo mtaani wanaume mkawafuata mkawatia adabu.
 
Kweli nimeamini kuishi Dar ni tatizo.. Kitunda si inajulikana kama Tarime ndogo! Leo wakurya mnakabwa mchana kweupe na vibaka! Mmekuwa wafuga kuku wa mayai sasa mmekuwa kama mabroiler😀😆😂 acheni kulialia hiyo ishu imo ndani ya uwezo wenu
 
Back
Top Bottom