Kamanda Lema ndani ya Arumeru

Kamanda Lema ndani ya Arumeru

Mnalinda hewa? CDM hawataambulia kitu, hivyo hakuna cha kulinda hapa. Msijifiche kwa aibu matokeo yatakapotangazwa. Itakuwa zaidi ya Igunga. Mnacheza na CCM???? SUBIRINI KILIO.

Hapa umeonyesha upeo wako wa kufikiri umefikia wapi.
 
Polisi napata taabu kuwaelewa, kwani Mwakyembe hakutoa taarifa polisi akapuuzwa, tena Naibu waziri, ndiyo watamthamini Lema ambaye ni mbunge halafu ni kutoka upinzani. Sina imani na jeshi la polisi ambao kwa sasa wanawatumikia mabwana wawili yaani ccm na mafisadi. Nafuu morani kuliko hawa tunaowahudumia hata mavazi yao ya kazi.
 
Kwa nini Lema pamoja na viongozi wa Chadema wasiombe ulinzi kutoka jeshi la polisi, kwa usalama na mustakabali wa nchi yetu tujiepushe vita vya kikabila ambavyo vitatupeleka pabaya, sio vizuri kulindwa na walinzi wa jadi, tujifunze kutoka Tarime.

polisi wepi hao unawaongelea? polisi wetu hawawezi kumpa Lema ulinzi..
 
Mkuu hatuwezi kusema wote ni CDM.Ila wameru wameshaamua mbunge wao ni Joshua Nassari

Sio tena baada ya uchaguzi mje humu Jamvini muanze kusema tumeibiwa kura na Lowassa.
 
Kwa nini Lema pamoja na viongozi wa Chadema wasiombe ulinzi kutoka jeshi la polisi, kwa usalama na mustakabali wa nchi yetu tujiepushe vita vya kikabila ambavyo vitatupeleka pabaya, sio vizuri kulindwa na walinzi wa jadi, tujifunze kutoka Tarime.
Mbona somo la Tarime lilieleweka vizuri tu labda nyie hamkulielewa kinachofanyika sasa ni implementation.
 
Sio tena baada ya uchaguzi mje humu Jamvini muanze kusema tumeibiwa kura na Lowassa.

Mkuu wangu Wameru ni tofauti sana na Igunga na Uzini.nadhani umenielewa mkuu wangu
 
Hahahaha Ritz, yaani Nyani wanatishia kuvamia shamba lako la mahindi wewe unataka kwenda omba ulinzi wa ngedere!
 
CDM mnajipa matumaini kuwa mtashinda Uchaguzi Jimbo la Arumeru, angalizo baada uchaguzi tukutane humu sio mkimbie CDM kushinda Arumeru ni ngumu.
 
Ujue kuwa pia Polisi wakitumia za moto hata huko ziko za kumwaga! Nawashauri Ndg na Kaka zetu Polisi, kwa hili la Meru wasikubali kupeleka msiba makwao, wawe tu wapole watafikisha miaka mingi kidogo, ila wakijifanya akina Schwarzenegger watashangaa kitakachokuwa.
Hamkumbiki Bwana mmoja alienda kuomba uhuru wa Wameru? inaweza ikawa ndiyo sasa tunaupata:A S embarassed:
Tena kwa usalama polisi wasijaribu kufyatua hata bomu moja kwa vijana wa kimeru. Nawajua na nimeishi huko najua wanavyopenda kesi (mtabisha) lakini ndiyo hulka yao, mtu anayejua maeneo ya USA river, Maji ya Chai, Kikatiti, Mbuguni hatabisha. Dili nyingi zinazochorwa hasa za wizi, ujambazi unapangwa huko, mapango ya kufichia gari za wizi yako milima ya meru midizini. Kama ni silaha za moto huko ndiko nyumbani kwake na kwa taarifa tu polisi ndio wanaotoa hizo silaha kwa hao vijana, kama ni ubabe nawaonya vijana wa green guard wawe wapole wasifikiri vijana wa meru sawa na wa Igunga waliokuwa wanawapiga makofi na kuwapakia kwenye magari yao. Ni tahadhali tu kwagreen guard na vyombo vya dola kwa sisi tunavyolijua hili jimbo.
 
Mungu atuepushe na vita kati ya morani dhidi FFU na Green guard hasa wakati wa kampeni za uchaguzi:lol:
 
Tena kwa usalama polisi wasijaribu kufyatua hata bomu moja kwa vijana wa kimeru. Nawajua na nimeishi huko najua wanavyopenda kesi (mtabisha) lakini ndiyo hulka yao, mtu anayejua maeneo ya USA river, Maji ya Chai, Kikatiti, Mbuguni hatabisha. Dili nyingi zinazochorwa hasa za wizi, ujambazi unapangwa huko, mapango ya kufichia gari za wizi yako milima ya meru midizini. Kama ni silaha za moto huko ndiko nyumbani kwake na kwa taarifa tu polisi ndio wanaotoa hizo silaha kwa hao vijana, kama ni ubabe nawaonya vijana wa green guard wawe wapole wasifikiri vijana wa meru sawa na wa Igunga waliokuwa wanawapiga makofi na kuwapakia kwenye magari yao. Ni tahadhali tu kwagreen guard na vyombo vya dola kwa sisi tunavyolijua hili jimbo.

Tunaomba polisi wafuate sheria kuepusha msuguano na wananchi walio wengi
 
Kwa hiyo unataka kutuambia Wameru wote ni Chadema?
Kamuulize UVCCM pwani je watu wa kazikazini ni wote chadema? au muulize nape eti wachaga wote ni chadema, Ni kweli kuwa yeye hawezi kujiunga chama chenye wachaga wengi..
 
ma.gamba yanaruka na kukanyagana....igunga mlitumia mashehe hamkufaniwa...meru mkataka kuwatumia wazee wa kimila...sasa inakula kwenu dadedi...wala msitafute mchawi..nyie wenyewe ndo wachawi
 
Jaman yashafika huko; Nakumbuka wakati TENDWA amemshauri Lema kuomba msamaa watu tulimponda sana humu ndani; na kama haitoshi akaibuka bwana mmoja ambaye pia ni Kiongozi wa wameru pande zile na kusema hakuna Tamko lolote lililotoka labda ni mtu mmoja tu yeye kama yeye kaamua kufunguka na huo uzushi wake ila tu wazee hawakupenda kauli za Mh Lema alizozitoa wakat wa msiba wa Mh Sumari; sasa yamefikaje ya kuandaa PLATOON YA ULINZI hivi hamuoni kama tunaandaa mazingira ya kuraruana sime?
 
Back
Top Bottom