Mkuu mleta mada umemalizia kwa kumwambia aendelee na kazi yake unayoiita nzuri?unadhani kama anasoma hapa anaweza kuchambua na kuelewa unavyotaka aelewe?nimependa bandiko,ila huo utani wakati ishu ni hatari na maisha ya watu hatarini ni noma.Sasa hata kama tunataka kulifix jeshi la polisi,akiachwa aendelee ndo jambo la maana?Accountability is the key to the changes that we want.It is the begining...Kova amekosea and my opinion;he should resign!
Mkuu uandishi una namna nyingi, labda unajaribu kutuhabarisha pia kwamba Kova hana akili ya kutosha kuelewa hili bandiko
Hivi ubalozi wa kenya wameshamtambua huyo 'MTEKAJI' kuwa ni kweli raia wao na wana records zake za uhalifu? manake naona kitambulisho cha uraia kimetolewa 2010, Umri bado mkanganyiko 21 au 31. Kama 21 ina maana kitambulisho kilitolewa akiwa na miaka 19 sheria za kenya za vitambulisho vya uraia inasemaje? kama ni 31 je muda wote alikuwa wapi kupata kitambulisho cha uraia.
Katika hali ya kawaida Polisi au Serikali ilipaswa isikilize kilio cha wale wanaohitaji tume huru ya kuchunguza kwa vile serikali na polisi ni mojawapo ya watuhumiwa. Katika hali hii ambapo serikali imekataa kusikiliza ushauri huo usio na madhara yoyote kwa upande wao (hasa kama ni kweli wanavyodai kuwa hawakuhusika) imani kama haki itatendeka ni ndogo sana. Kutaja kuwa ni mtuhumiwa mmoja tu hadi sasa amehojiwa na mtuhumiwa mwenyewe asiwe yule aliyempigia simu Ulimboka ambaye kwa vyovyote jeshi la Polisi linamfahamu, kunalifanya Jeshi la Polisi machoni pa raia kuwa haliko makini. Hata kama waliotajwa wanaweza wasiwe wamehusika kuwahoji kulikuwa ni kwa lazima maana ni watuhumiwa. Ikiwa mbunge Nasari alihojiwa na kuachiwa kwa nini huyo aliyetajwa na Ulimboka asihojiwe. Kwa mazingira kama haya Jeshi linawalazimisha watu waamini kuwa tukio hili lina mkono wa serikali. Huu ni utamaduni mpya ambao tusingependa kuushuhudia katika nchi yetu. Mungu ibariki TanzaniaHivi kwa nini serikali ya Jk haimkamati mtuhumiwa wa kumtesa Dr Steven Ulimboka?kwa sababu Dr Ulimboka aliweza kumtambua pale alipofika wodi kutaka kumalizia kumuua Dr Ulimboka,hivi angekuwa ni mlalahoi ndo anatuhumiwa si angekuwa ameisha kamatwa na kufunguliwa mashitaka.Hivi huyu Ahmed Msangi anakinga ya kutokamatwa au analindwa na vigogo wenzake wa jeshi la pilisi na wa usalama wa taifa?au ni kutokana na udhaifu wa serikali ya mr Dhaifu?