Sisi watanzania tunakosea kumhukumu Kova kwa swala hili la Joshua Mkenya kuhusika na tukio la Ulimboka. Tunamuonea Kova
1. Ni utamaduni wa serikali hii kupika uongo na kudanganya wananchi kuhusu mambo mbalimbali. Hata Bunge hudanganywa
2. Ni utamaduni wa Polisi kubambika watu kesi za mauaji na uharamia.
3. Kova amekuwa mara kwa mara akiitisha mikutano na waandishi aw habari kutangaza habari za uongo za kukamatwa majambazi "sugu waliokuwa wanatafutwa muda mrefu" Anachukua silaha za ujambazi uliofanyika zamani anaonesha kana kwamba ndo kazikamata. Ili aonekane anafanya kazi yake kwa umahiri. Ujambazi unaongezeka hadi wananchi wamezoea hawalalamiki tena
4. Jeshi la Polisi kwa ujumla halipelelezi kesi bila mlalamikaji kutoa pesa na nyenzo nyingine. Nani ataliwezesha jeshi la Polisi kupeleleza tukio la Ulimboka? Je, jeshi la Polisi lina ujuzi wa kupeleleza au kutesa watu wakiri makosa?
5. Jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika na tukio la Ulimboka, mnatarajia Kova anaweza kupeleleza Msangi kama ndiye aliyemtuma Msangi?
Kwa maelezo hayo hapo juu, namsifu sana Kova kwa ubunifu aliofanya wa kutupatia mtuhumiwa Mkenya na kulihusisha kanisa. Nahisi Kova aliumoza kichwa sana na amejitahidi kutafuta namna ya kulinausua jeshi la Polisi na serikali.
Kwanini tuhangaike kutafuta kujiuliza kam Kenya kuna watu wenye tabia ya uharamia na mauaji wakati tunajua hivyo tayari, Mungiki, Mauaji baada ya Uchaguzi etc
Kwa nini tuhangaike kuhoji uadilifu wa viongozi wa dini? Kwa nini kiongozi huyo wa dini asifurahi kwamba serikali imemshukuru kwa kutoa ushirikiano?
Tunafanya makosa kumtuhumu Kova kudanganya leo wakati ndiyo utendaji wa kazi aw kawaida siku zote, penda usipende
Endelea Kamanda Kova, I salute you!