Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 22, 2012 08:48 NA ELIZABETH MJATTA

KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ameibuka na kusema hawezi kujiuzulu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Daud Mwangosi, aliyeuawa hivi karibuni mkoani Iringa.

Kamanda Kamuhanda alitoa msimamo huo jana alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Radio One wakati wa kipindi cha Kumepambazuka.

“Ninachofahamu mimi ni kwamba, kesi ya msingi iko mahakamani na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ameshaunda kamati ambayo inachunguza mwenendo mzima wa tukio hili na baadaye itatoa taarifa.

“Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Kamuhanda.

Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.

“Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika, haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.

“Sisi tunapokuwa kazini, tunalinda raia na mali zao na ndiyo tulilofanya na mara zote tunasisitiza utii wa sheria bila kushurutishwa.

“Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea,” alisema.

Septemba 2 mwaka huu, Mwangosi aliuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu alipokuwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Baada ya kulipuliwa na kitu hicho, mwili wake ulisambaratika vipande vipande ingawa pia askari mmoja aliyekuwa jirani naye, pia alijeruhiwa mguu.

Baada ya tukio hilo, waandishi wa habari, wanaharakati na watu mbalimbali, walilaani tukio hilo na kutoa matamko yao wakitaka Kamanda Kamuhanda ajiuzulu, kutokana na mauaji hayo.

Septemba 12 mwaka huu, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mwenye namba G2573, Pasificus Simon, alipandikizwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Iringa, kwa kosa mauaji ya marehemu Mwangosi.

Mtuhumiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo, hakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa linalomkabili haliwezi kusikilizwa katika mahakama hiyo. Hadi sasa mshitakiwa yuko mahabusu.

Jamaa ana POWER kweli... Inaonyesha JINSI asivyo na WASIWASI JUU YA KAZI YAKE.
 
kwa nini waandishi wa habari huwa mnawaauliza hawa mnaowauliza maswali mwongozo? kwa nini usimuulize ni makosa gani ambayo yanapaswa mtu akawajibika kama alivyosema kuna makosa ya kuwajibika?
 
ukisikiliza kwa makini kauli yake utagundua jinsi serikali ilivyokosa uhalali wa kuongoza.
yaani mpaka hapo haoni kosa na hawezi kujiuzulu hata kama polisi wake wakiua maelfu machoni pake.
MPELEKEENI TAARIFA KUWA TUNAMSUBIRI URAIANI.
 
Jamaa ana POWER kweli... Inaonyesha JINSI asivyo na WASIWASI JUU YA KAZI YAKE.

Hivi huyu jamaa atumia akili gani?

Anapata wapi ujasiri wa kuongea upuuzi kama huu?

"Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea,"

Hapa ana maana kuwa watu wasipotii sheria adhabu yao ni kuuawa??
 
Walimuuliza anayekosa kutii sheria bila shuruti huuwawa kwa kutumia kifungu kipi cha sheria?

Kama hawakumuuliza, basi naieleweke leo kuwa waandishi wa habari ndio tatizo Pasco waambie wenzio.
 
Last edited by a moderator:
JUMAMOSI, SEPTEMBA 22, 2012 08:48 NA ELIZABETH MJATTA

KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ameibuka na kusema hawezi kujiuzulu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Daud Mwangosi, aliyeuawa hivi karibuni mkoani Iringa.

Kamanda Kamuhanda alitoa msimamo huo jana alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Radio One wakati wa kipindi cha Kumepambazuka.

"Ninachofahamu mimi ni kwamba, kesi ya msingi iko mahakamani na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ameshaunda kamati ambayo inachunguza mwenendo mzima wa tukio hili na baadaye itatoa taarifa.

"Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa
kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti," alisema Kamanda Kamuhanda.

Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.

"Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika,
haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.

"Sisi tunapokuwa kazini, tunalinda raia na mali zao na ndiyo tulilofanya na mara zote tunasisitiza utii wa sheria bila kushurutishwa.

"Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea," alisema.

Septemba 2 mwaka huu, Mwangosi aliuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu alipokuwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Baada ya kulipuliwa na kitu hicho, mwili wake ulisambaratika vipande vipande ingawa pia askari mmoja aliyekuwa jirani naye, pia alijeruhiwa mguu.

Baada ya tukio hilo, waandishi wa habari, wanaharakati na watu mbalimbali, walilaani tukio hilo na kutoa matamko yao wakitaka Kamanda Kamuhanda ajiuzulu, kutokana na mauaji hayo.

Septemba 12 mwaka huu, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mwenye namba G2573, Pasificus Simon, alipandikizwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Iringa, kwa kosa mauaji ya marehemu Mwangosi.

Mtuhumiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo, hakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa linalomkabili haliwezi kusikilizwa katika mahakama hiyo. Hadi sasa mshitakiwa yuko mahabusu.

Is that a new phrase for "murder"?
Siku aliyouawa marehemu Mwangosi kulikuwa na maandamano?? I thought ilikuwa ni ufunguzi wa tawi la CHADEMA....... Anyway hapo RPC anajaribu kutuambia ule mkusanyiko wa CHADEMA ndo ulifanya yale mauaji au?
Is he trying to say kwamba marehemu Mwangosi alikataa kutii sheria ndo polisi wakaamua kufanya walichofanya?Hio ni sahihi??
Ushauri wa bure kwa RPC huyu........ Kadri anavyozidi kuongea anazidi kutia hasira watu kwa maneno yake...... Akae kimya tuu, itakuwa ni busara zaidi asijifanye jeuri
Kweli nimeamini power corrupts, and absolute power corrupts absolutely!!!

Naona majibu yake ni yale yale kama kauli ya Hiza Tambwe ilivyokuwa. Kwa nn watu hawaandamani kushinikiza watu kama hawa kujiuzulu?? Yaani mnataka ajiuzulu mwenyewe?? Huo si utamaduni wa wetu, inabdi awekewe pressure kwa maandamano.
 
Nasikia uchungu ningekuwa mimi ndo ananijibu hivyo ningekuwa mahabusu sasa hivi kwa kesi ya kumtandika ngumi ya uso na kuua RPC
 
Nazani damu ya Mwangosi imeanza zaa matunda maana mzee keshaanza changanyikiwa CDM walikuwa na mkutano wa ndani yeye anaongelea maandamano!
Kamanda ni busara kukaa kimya otherwise unaaribu
Alafu na huyu mwandishi yuko shallow na hakujiandaa kabisa au ndo uko katika harakati za kumsafisha Kamudandu?
 
Astaghafrulah laana tu lah! Yaani huyu m.... ndo anaropoka hivi, ningekuwa karibu yake wakati anajibu ningemlima kichwa cha uso na ningekuwa mahabusu
 
Ni jibu au swali la rpc kwanini wasijiuzuru walioandamana nijiuzuru mimi? Mwangosi aliandamana? Je wajibu wa polisi ni kuuwa waandamanaji? Alitakiwa ajibu sio kuleta ulevi na ubabe wa madaraka
 
ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia subordinates wake mpaka wakamfyatulia bomu mwangosi at zero distance.pia awajibike kwa mauaji yaliyofanywa na polisi huko songea.
 
Kuna kijana wangu wa kike yuko darasa la pili, ana busara maradufu kuliko huyu RPC.
 
Ni jibu au swali la rpc kwanini wasijiuzuru walioandamana nijiuzuru mimi? Mwangosi aliandamana? Je wajibu wa polisi ni kuuwa waandamanaji? Alitakiwa ajibu sio kuleta ulevi na ubabe wa madaraka

Unaweza kusoma kitu fulani hapa kama hayati Nyerere alivyosema; "ukishaonja nyama ya mtu vigumu kuacha." Mwisho wa nukuru. Nilipokuwa nasikia kauli hiyo sikujua Nyerere alikuwa anamaanisha nini kwa vile nilikuwa bado mdogo sana.

Kamuhada ameua Songea watu wanne mwaka huu, na kisha kuhamishiwa Iringa ameanza kuvuta kiti chake cha U-RPC kwa kuua Mwandishi wa habari mauaji ya kinyama yeye akishuhudia amebaki gari kando yake.

Leo anakuja kwa kujiamini na bila wasiwasi kwamba hawezi kujiuzuru alikuwa anatekeleza kazi yake.

Ukiona dalili za kuzeeka vibaya na kushia kustaafu kutokuwa na maisha ya raha na starehe huku ukiwazia tamu ulizozimwaga, basi ujue mambo kama hayo si ya umri wa sasa tunaouona, ila ni jambo alilolizoea na ndio maana anajiamini na hana wasiwasi kwa mauaji yake.

Kiongozi mwenye dhamiri ya kujali maisha ya binadamu angeona aibu na kusikitikia tukio lile linalolaaniwa na watanzania na dunia nzima na hata kuisababishia serikali kupata matatizo kwa wahisani kama Umoja wa nchi za Ulaya uliyvotolea kauli jana.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Mauwaji aliyoyafanya ni ya kisiasa,na kwahiyo majibu yake pia ni ya kisiasa.

Hata asipojiuzulu,kuna wakati atajibu tuhuma hizi za mauwaji.Nchi za wenzetu kashfa kama hii wala asingethubutu kupanua mdomo,maana angekuwa keshajiuzulu na angeogopa maneno yake yasitumike dhidi yake wakati wa mashtaka.Kwa mfano kauli kuwa watu wakikusanyika kufunguwa tawi basi wauwawe kwasababu wamevunja sheria.Kauli kwamba walifanya maandamano ni ya kisiasa,kwasababu mwanzoni alisema ni mikutano haitakiwi kwasababu ya sensa,lakini cha ajabu ccm ilikuwa na mikutano,na pia kulikuwepo na fiesta.

Only in Tanzania haya ndo yanaonekana kuwa ni ya kawaida.
 
Back
Top Bottom