Kamanda Basileo Matei wa AR awajibishwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Basileo Matei wa AR awajibishwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 15, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  JAMBO lililomkuta Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Jumanne iliyopita, linatosha kabisa kumfukuzisha kazi Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo kwa uzembe na kutokuwajibika. Na kama angekuwa muungwana, yeye mwenyewe angeamua kuvua nembo ya Jeshi letu la Polisi na kuiweka pembeni.

  Jaji Bethuel Mmila alijikuta ameibiwa kompyuta ya kubeba (laptop) na zaidi ya yote kujikuta akielekezwa mtutu wa bunduki na jambazi nyumbani kwake ambaye alimtishia kumuua hapo hapo kama angefanya lolote.

  Habari hizi zinasikitisha kuwa hazijapata sauti ya kutosha wiki iliyopita kutoka kwa wanasiasa na viongozi wetu kana kwamba tunaishi Baghdad! Inasikitisha uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa katika ubinafsi wao na mikutano yao na hakuna hata mmoja wao aliyeshtushwa na jambo hilo. Sitashangaa hawakuwa na taarifa hizo kwani wao walikuwa wanawaza; “Nape, Nape, Nape!”

  Jaji huyo anasimulia katika gazeti moja la Kiswahili kuwa hayo yote yalitokea licha ya kuwa anatakiwa kuwa na maafisa wa Polisi kumpatia ulinzi nyumbani kwake.

  Jaji huyo amesema kuwa baada ya kuona kuwa kompyuta yake ambayo iko karibu na dirisha imetoweka na dirisha likiwa wazi. Alipotoka kuwatafuta maofisa wa polisi wawili wanaotakiwa kumpa ulinzi, hakukuwa na mtu. Alipokwenda kwenye nyumba ya msaidizi wake wa nyumbani, naye hakuwapo.

  Ni hapo ndipo alipojikuta anaambiwa na mtu aliyekuwa na silaha na aliyejificha uso kuwa; “ukithubutu kufanya lolote nitakushuti mara moja.” Mtu hyo akamuelekeza arudi ndani ya nyumba yake.

  Baada ya kujifungia chumbani, Jaji huyo alijaribu kupiga simu polisi Arusha kutoa tahadhari bila kuitikiwa na akajaribu polisi Moshi bila kuitikiwa. Inashangaza kuwa hadi hivi sasa si makamanda wa mikoa hiyo au kutoka makao makuu waliojitokeza kusema lolote na kuwahakikishia majaji wetu kuwa maisha yao yako salama.

  Kwa watu wengine kitendo hicho kinaweza kuwa ni ujambazi wa kawaida, lakini kwa mzee wenu hapa naamini kuwa ni mstari wa hatari sana unaoanza kuvukwa. Inapotokea majambazi wanafika hadi kwa majaji na kufanya ‘kweli’ na wale waliotakiwa kutoa ulinzi wanajiumauma meno hakuna kitu kingine cha kuwaamsha isipokuwa kuwawajibisha.

  Kama Lowassa aliweza kuwajibika kwa makosa yake ya kutowajibika kusimamia walio chini yake ipasavyo (si kwa sababu za kisiasa kama Waziri Mkuu alivyojaribu kutuzuga hivi juzi), basi Kamanda huyu wa Arusha pamoja na maofisa waliohusika kutoa ulinzi ni lazima wawajibishwe mara moja.

  Tukifumbia macho tukio hili na kulichukulia kama kawaida, tunafungua mlango wa hatari kubwa sana nchini. Hofu yangu si tu tukio hilo la ujambazi, lakini kilicho nyuma yake - ni kitu gani kilisukuma mtu kwenda kumpora Jaji kompyuta?

  Je, yawezekana Jaji Mmila alikuwa anasikiliza kesi fulani au kupanga kutoa hukumu juu ya mtu fulani ambaye hajafurahishwa na mwenendo wa kesi? Je, yawezekana Jaji Mmila ametumiwa kutuma ujumbe kwa majaji wengine ambao watakuwa tayari kusikiliza kesi za mafisadi nchini? Hivi kama Jaji huyo angeuawa leo hii tungesema nini; kwa nini kwa vile kanusurika hakuna kelele za kukemea kitendo hiki? Hadi mtu auawe ndio tutaamka na kuona uovu?

  Je, yawezekana kuwa mapolisi waliotakiwa kumlinda ndio walikula njama na majambaza/jambazi? Yawezekana kuwa mapolisi wenyewe ndio waliokuwa majambazi?

  Katika hili tusikubali kuvumilia uovu na kuuchekea ufisadi. Jaribio hili la kumshambulia jaji na zaidi ya yote kumuondolea ulinzi ni suala la hatari sana kwa utawala wa sheria na kwa hakika lazima likemewe na kupingwa na wapenda utawala wa sheria mahali pote.

  Hatutaki majaji wetu, mahakimu na watumishi wa sheria kuanza kuwa wahanga wa mapambano ya ufisadi.

  Naomba muungane nami kutaka Kamanda huyo atimuliwe kazi mara moja kama adhabu kali zaidi na fundisho kwa makamanda wengine kuwa kuna maeneo ambayo hayatakiwa kuchezewa hata kuzembewa kwa dakika yoyote.

  Zaidi ya yote tunatarajia Inspekta Jenerali wa Polisi atakuwa tayari kuomba radhi kwa jaji huyo na mahakama na kuwahakikishia majaji wetu kuwa uzembe uliotokea kwa Jaji Mmila hautarudiwa tena na ukitokea yeye mwenyewe atakuwa tayari kuwajibika.

  Katika mapambano haya tusikubali uovu ati kwa sababu tunaogopa ukweli; Tusikae kuangalia nchi yetu inatawaliwa kwa sheria ya mwituni ambapo mwenye nguvu mpishe. Natoa pole za dhati kwa jaji na ninaomba samahani kwa sisi waandishi na wapenda demokrasia na utawala wa sheria kutopiga kelele za kutosha kuhusu suala hili na kumezwa na mambo ya kitoto ya CCM na Nape!

  Nalaani kwa kauli nzito kabisa inayowezekana kitendo cha maofisa wa polisi kuondoka lindoni na kamanda wao kutojua nini kinaendelea. Tunataka wahusika wawajibishwe mara moja kama fundisho wa wengine wote ambao wanachukulia mahakama kama chombo cha kuchezea.
   
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Hilo kwa kweli linashangaza na nashawishika kusema kuwa huenda ni njama ilipangwa na hao polisi waliotakiwa kuwa lindoni usiku huo. Haiwezekani jaji aibiwe na anapoenda kuomba msaada kutoka kwa polisi aliyetakiwa kuwa lindoni asikute mtu wala mtumishi wake kuna mchezo mchafu hapo.

  Basilio Mathei na Mwema wote wanawajibika kwa hili. Hivi kwa mfano yule jaji angeuwawa IGP,RPC na wengine wangekaa kimya kweli au ndio kila mtu anakufa kivyake?
   
 3. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hiyo laptop lazima ilikuwa na hukumu zote muhimu. sijasikia tamko la jeshi la polisi mpaka sasa. inasikitisha sana
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Am out of words!Jaji?
  Hawa watu mbona wanasecurity hadi baa wanakokwenda kunywa?Amekuwa betrayed na walinzi wake!I think security inayokuwa assigned to such people iwe very much reviewed!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Sep 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kevo, nimebahatika kukaa na hawa waheshimiwa; wakati watumishi wengine wanaopewa walinzi wanapewa nyakati za jioni, majaji wana ulinzi wa masaa 24; sasa inapotokea walinzi wote wawili wasiwepo lindoni hadi Jaji anaibiwa, anatoka nje hakuna mtu; anaita hakuna mtu halafu anapiga simu Polisi hawapokei, kuna udhahiri wa jambo moja. Kuna mtu lazima awajibishwe. Hata kama siyo kumfukuza kazi lakini lazima mtu aoneshe kuwa kitendo hicho hakivumiliki.

  Lakini ni Tanzania, ni vigumu kumuwajibisha mtu kwa sababu ana familia yake hivyo lazima wafikirie sana. Sitoshangaa atatakiwa atoe maelezo ya kina (kama alivyosema mtu hapo juu) ili aelezee kwanini asichukuliwe hatua kali.
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mku kwa kweli mimi binafsi am abit astonished with these news maana nipo hapa AR na mahakamani ndiyo kama nyumbani kwa sababu ya my profession!I hobnob with these people on my weekends and I see there security!
  I know a few of them ambao kidogo kwa kweli security yao is not that much trained as I can Judge na kidogo wengi wao ni big mouthed so it is easier for outsiders to know the kind of lives hawa waheshimiwa wanayoyaishi!
  Sitashangaa either mlinzi wake alikuwa bribed or not into betraying huyu Mheshimiwa!
   
 7. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ....Kevo...I like you avatar....I can see bouncer mtoto anatunishia msuli geshi...Very interesting teh! teh!! tehhhh!!
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  wamewakamata wale askari waliopanguwa lingo kwa jaji siku ile. nadhani hao ndio watakuwa mbuzi wa kafara na habari itakuwa imekamilika
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wamekamatwa lini hao?
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ni ugaidi huo....Unaweza kuta kuna kesi muhimu ya kigogo.
  WARLORDS System kama ile ya Afganistan ndio inaanza hapo bongo.
  Hamuoni HIMAYA za Muungwana zinavyooteshwa kama zile za Saddam?
  Tunakoelekea si kuzuri kabisa.
  Itafikia mahali kama huna kajeshi kako bongo basi uwe mtumwa tu.
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  "Me no cry fe no dignitary inna no three piece suit
  Me no cry fe no dignitary inna no crisp Clarks boots
  But me will cry, me will cry fi de youth"

  Pengine watu wanatumia "The Robin Hood Theory" na hii ni a moment of "The chicken coming home to roost"?

  Mwanakijiji you gotta build a case kusema hii ni a coordinated act of terrorism.
   
 12. L

  Lizy JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 413
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  Mwanakijiji,

  Asante sana kwa Taarifa hii.

  Kweli hali inatisha, uhalifu unazidi siku hadi siku, mbaya sana.

  Binafsi nina haya machache katika hili suala;

  "Je, yawezekana kuwa mapolisi waliotakiwa kumlinda ndio walikula njama na majambaza/jambazi? Yawezekana kuwa mapolisi wenyewe ndio waliokuwa majambazi?"Yeah, Inawezekana kabisa. Hawa wanatakiwa watafutwe/wakamatwe na wahojiwe. Tena hawa ndio watuhumiwa namba moja kwani mazingira yanaonyesha hata kama hawakuhusika moja kwa moja, basi walisababisha tukio hili kutokea. "Failure to prevent felony", wanasheria nisahihisheni kama nimekosea.

  "Katika hili tusikubali kuvumilia uovu na kuuchekea ufisadi. Jaribio hili la kumshambulia jaji na zaidi ya yote kumuondolea ulinzi ni suala la hatari sana kwa utawala wa sheria na kwa hakika lazima likemewe na kupingwa na wapenda utawala wa sheria mahali pote".
  Judge aliondolewa ulinzi? Kwenye maelezo imeonyesha kuna Askari walitakiwa kuwepo kumnlinda hivyo amepewa ulinzi. Na kama basi RPC ana wahusika wengine waliamua kumuondolea Judge huyo ulinzi wa Polisi ambao anatakiwa kupewa kila siku, na hawakumjulisha kwamba wanaondoa ulinzi huo kwa sababu kadha wa kadha, then suala hili lichunguzwe na kukemewa vikali.

  "Naomba muungane nami kutaka Kamanda huyo atimuliwe kazi mara moja kama adhabu kali zaidi na fundisho kwa makamanda wengine kuwa kuna maeneo ambayo hayatakiwa kuchezewa hata kuzembewa kwa dakika yoyote".
  Hapana. Binafsi naona kamanda huyu asitimuliwe kazi, na badala yake awajibishwe kwa kuhakikisha wahusika katika tukio hili wanakamatwa, laptop inapatikana na sheria inachukua mkondo wake haraka iwezekanavyo. Kumtimua kazi hakutasolve tatizo hata mara moja, zaidi ya kuendekeza uzembe wakijua wataachishwa and thats all.
  Pia inapokuja suala la usalama wa raia dhidi ya uhalifu, tuzingatie kwamba maeneo yote (serikalini, kwa walalahoi, kwa matajiri na kwingineko) ni muhimu, hapatakiwi kuchezewa ama kuzembewa kwa dakika yoyote.

  "Inasikitisha uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa katika ubinafsi wao na mikutano yao na hakuna hata mmoja wao aliyeshtushwa na jambo hilo. Sitashangaa hawakuwa na taarifa hizo kwani wao walikuwa wanawaza; "Nape, Nape, Nape!"Yeah, naona Nape alichukua sehemu kubwa na wana CCM wakajikuta wanalala, wanasahau masuala mengine ya nchi likiwemo hili la ulinzi (Japo sioni CCM imeingia vipi hapa). LAKINI, Si tuna vyama vingi siku hizi jamani? Hawa vyama vingine walikuwa wapi kuliona hili? Au ni kitu kinahusiana na CCM tu? Hapa kidogo Mwakajijiji ...............,Anyway.

  "Inashangaza kuwa hadi hivi sasa si makamanda wa mikoa hiyo au kutoka makao makuu waliojitokeza kusema lolote na kuwahakikishia majaji wetu kuwa maisha yao yako salama".
  Yeah, watujulishe kwa nini waliamua kukaa kimya (kuficha siri)? Na nini kinaendelea? Pia,Hawa makamanda na huko Makao Makuu wanatakiwa kutuhakikishia wananchi wote kuwa maisha yetu yapo/yatakuwa salama.

  "Kama Lowassa aliweza kuwajibika kwa makosa yake ya kutowajibika kusimamia walio chini yake ipasavyo" No comment, though……….

  "Hofu yangu si tu tukio hilo la ujambazi, lakini kilicho nyuma yake - ni kitu gani kilisukuma mtu kwenda kumpora Jaji kompyuta"?
  Kweli kama hawakuiba kitu kingine zaidi ya Kompyuta hiyo, hata baada ya kumtishia Jaji na bunduki then kuna jambo linajificha ambapo Polisi ama chombo husika kwa ushirikiano wa Jaji wetu wanatakiwa kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo.

  Huko vituo vya Polisi nako sometimes mh! Hizo namba zao sijui ndio ubusy ama ni nini, ukipiga hazipatikani sasa sijui wanamaanisha nini kutoa namba za emergency ambazo hazipatikani si mchana wala usiku? They should do something kuhusu mawasiliano, ni mawasiliano tu yatawezesha kupata taarifa haraka na ni kwa taarifa hizo za haraka, zinaweza kuzuia uharifu kutokea, lakini kama mawasiliano ni zero, then ni sherehe kwa wahalifu.
  Kwa tukio hili;
  Kwa vile laptops hazipo salama. Mbali na kwamba zinawavutia wezi, pia kuna hili kundi lingine baya zaidi la kutaka kuiba kile tu kilichotunzwa (files) kwenye laptops hizo na siyo laptop yenyewe. Sasa basi tuliepuke vipi hili kundi la pili, tunapofanya kazi zetu, basi tusitunze files kwenye laptops hizo, na badala yake tununue external drives, cd's, flash discna kadhalika, kwa kutunzia files za kazi zetu. Tuhakikishe hatutunzi external drive/cd/flash kwenye bag tunaloweka laptop, badala yake tuzitunze sehemu tofauti ili basi ikitokea laptop kuibiwa/kupotea ama lolote lile, tunabaki na kazi zetu sehemu salama.

  Ni hayo tu.
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,580
  Likes Received: 5,762
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji hiyo wala usishtuke hivi sasa kumekuwa na mawasiliano machafu kati ya majambazi na jeshi la polisi...................................
  Nakupa mifano mingi kwanza kuna swaala la kutopokelewa simu ..wale watu hawapokei simu hasa wakijua wazee wa kazi wamepiga sehemu na kitu kinachofanyika ambacho nakilaani mpaka mwisho nikitendo cha kuondoa ma defender ya polisi dk 20 au nusu saa alafu unasikia watu wamepiga kazi hapo hapo!!!!!
  Kuna swala lingine la ukodishwaji wa silaha ;;hili swala alitakaa liishe kama polisi wataendelea kulipwa lakimoja na 20 akiwa na familia yake;haya ni matusi mazito ya nguoni kw arais....kuna wakati kituo kimoja kimekuwa kikikodisha silaha kwa majambazi wake na mpaka leo nina rafiki yukop pale anasema wala simillion wanalipwa lakitatu silaha inarudi saa tisa ....ni kile cha changombe..kwa hiyo haya mambo si ya ajabu sana br hata tukemeeje::nilisikirtika kuona mada moja ya kupongeza bw kova huku siku tano zilizopita watu wameibiwa fedha zao na kuuwawa bado inakuwa ngumu kuamini jeshi la polisi....dawa ni kuanza kujilinda mwenyewe kwanza hao manyangao baadae

  hii serikali hatari

  wezi wakiiba ukipiga polisi apokei

  motto ukiunguliwa wanakuja bila maji

  ukisoma hamna kazi

  twende wapi jamani????
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  John Mhala, Arusha
  Daily News; Tuesday,September 16, 2008 @00:02

  Habari nyingine
  Mdhamini nusura alambe miaka saba jela
  Sita washikiliwa kwa tuhuma za ujambazi
  Balozi wa Marekani afagilia kaulimbiu ya Kikwete
  Bunge kielelezo cha ukuaji wa demokrasia -Sitta
  Kizimbani kwa kula njama kuiba mamilioni NMB
  Polisi wa lindo la Jaji kushtakiwa
  Mtoto wa kigogo wa BAKWATA mbaroni
  Vijembe vyaanza Tarime
  Kiteto wampongeza Kikwete kwa uamuzi wa EPA
  Mfuko wa pembejeo wadai bilioni 6/-

  Askari Polisi wawili waliosababisha Jaji Mfawidhi Kanda ya Arusha, Bethuel Mmila, kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wiki iliyopita usiku na kuporwa televisheni ndogo na kompyuta ndogo, wanashitakiwa kijeshi.

  Katika tukio hilo lililotokea Uzunguni mjini hapa, mbali ya Jaji Mmila kuibiwa vitu hivyo, alinusurika kuuawa alipotoka nje kuomba msaada wa polisi ambao hata hivyo, hawakuwapo lindoni wakati huo na kutishiwa na bastola na majambazi hao waliokuwa na silaha wakati akirudi ndani.

  Habari kutoka Polisi mkoani Arusha zilisema kuwa hati ya mashitaka ya askari hao, makonstebo waliotambulika kwa jina moja moja ya Albanus na Godfrey, tayari imeandaliwa na kinachosubiriwa ni kufikishwa mahakama. Kwa mujibu wa taratibu za kipolisi, kufikishwa mahakamani kwa askari hao moja kwa moja kutawafanya wafukuzwe kazi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Basilio Matei alipoulizwa juu ya habari hizo za kushitakiwa kijeshi kwa askari hao, alikiri na kueleza kuwa watashtakiwa kijeshi muda wowote kuanzia sasa. Alisema askari hao wameonyesha uzembe mkubwa katika utendaji kazi wa kila siku wa Jeshi hilo katika malindo mbalimbali mkoani Arusha na kutokana na hilo, hawatakuwa na subira juu ya uzembe huo.

  Hata hivyo, awali Kamanda huyo alikuwa mgumu kutoa ushirikiano katika suala hilo na kumtaka mwandishi wa habari hizi kuacha ‘kuokota okota habari mtaani', akisema habari hizo si za ukweli kwani Jaji ni kiongozi mkubwa nchini, akiibiwa lazima polisi iwe na habari muda huohuo.

  Alipoulizwa ni kwa nini alishindwa kutoa taarifa mara alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Matei alidai hakuwa na taarifa juu ya tukio hilo kwani hupelekewa taarifa, hivyo hawezi kuwa kila mahali. Jaji Mmila alivamiwa nyumbani kwake saa 10:30 alfajiri ya Jumatano iliyopita na watu ambao hawajafahamika na wanaoaminika kuwa majambazi na kisha kufanya uporaji huo, huku akiwa na askari wanaopaswa kutoa ulinzi kwa mwanahaki huyo.

  My Take:
  Nafurahi kusikia hatua hizi kwani kwa wiki nzima walikuwa kimya hadi tulipoandika siku ya Jumapili na kuchapa mtandaoni na kutuma kwenye email mbalimbali tunafurahi kushiriki katika kuliamsha Taifa. Tukikubali kulala, mafisadi watatawala na watatula na kulala!
   
 15. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Polisi wa lindo la Jaji kushtakiwa

  Askari Polisi wawili waliosababisha Jaji Mfawidhi Kanda ya Arusha, Bethuel Mmila, kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wiki iliyopita usiku na kuporwa televisheni ndogo na kompyuta ndogo, wanashitakiwa kijeshi.

  Katika tukio hilo lililotokea Uzunguni mjini hapa, mbali ya Jaji Mmila kuibiwa vitu hivyo, alinusurika kuuawa alipotoka nje kuomba msaada wa polisi ambao hata hivyo, hawakuwapo lindoni wakati huo na kutishiwa na bastola na majambazi hao waliokuwa na silaha wakati akirudi ndani.

  Habari kutoka Polisi mkoani Arusha zilisema kuwa hati ya mashitaka ya askari hao, makonstebo waliotambulika kwa jina moja moja ya Albanus na Godfrey, tayari imeandaliwa na kinachosubiriwa ni kufikishwa mahakama. Kwa mujibu wa taratibu za kipolisi, kufikishwa mahakamani kwa askari hao moja kwa moja kutawafanya wafukuzwe kazi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Basilio Matei alipoulizwa juu ya habari hizo za kushitakiwa kijeshi kwa askari hao, alikiri na kueleza kuwa watashtakiwa kijeshi muda wowote kuanzia sasa. Alisema askari hao wameonyesha uzembe mkubwa katika utendaji kazi wa kila siku wa Jeshi hilo katika malindo mbalimbali mkoani Arusha na kutokana na hilo, hawatakuwa na subira juu ya uzembe huo.

  Hata hivyo, awali Kamanda huyo alikuwa mgumu kutoa ushirikiano katika suala hilo na kumtaka mwandishi wa habari hizi kuacha ‘kuokota okota habari mtaani’, akisema habari hizo si za ukweli kwani Jaji ni kiongozi mkubwa nchini, akiibiwa lazima polisi iwe na habari muda huohuo.

  Alipoulizwa ni kwa nini alishindwa kutoa taarifa mara alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Matei alidai hakuwa na taarifa juu ya tukio hilo kwani hupelekewa taarifa, hivyo hawezi kuwa kila mahali. Jaji Mmila alivamiwa nyumbani kwake saa 10:30 alfajiri ya Jumatano iliyopita na watu ambao hawajafahamika na wanaoaminika kuwa majambazi na kisha kufanya uporaji huo, huku akiwa na askari wanaopaswa kutoa ulinzi kwa mwanahaki huyo.
   
 16. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mengi yametokea Arusha, watu mashuhuri wameuwawa majumbani mwao na majambazi. Kila tukio linaishia kwenye assumptions, "lazima marehemu alimrusha mtu ndiyo maana aliuwawa" n.k. Ni lini hapa Arusha mtu amekamtwa na kushitakiwa kuwa ndiye aliyemuua fulani? The whole security system sucks, hata Basilio akiondoka hakutakuwa na tofauti yeyote,ujambazi utaendelea, watu watauwawa na hakuna ataekamatwa. Ataletwa RPC mwingine na mambo yataendelea hivyo hivyo. Labda ni wakati muafaka JWTZ wa take over.
   
 17. C

  Cool Girl Member

  #17
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu wa atown wameshacomplain sana juu ya huyu basilio,kwanza hajali,hajichanganyi na wadau,ujambazi ukikabaka everywhere in atown,wakati wa sullivan aliwaomba majambazi waende moshi kwa muda,mkutano ulipoisha nafikiri akawapigia waje waendelee na shughuli zao,sasa mpaka kwa jaji??hii too much au anahusika maana amepiga kimya kama vile yeye sio muhusika wa geshi ra porisi!ananiudhi mie basi tu!!!!!!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Cool girl... yaani huyu Kamanda aliwaomba majambazi wachukue likizo?
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nilivyomuelewa mie ni kuwa aliwaomba Majambazi waache Arusha ipumue kwa muda na hiyo ATHMA yao waipeleke Moshi. Sasa huko Moshi haijulikani kama walikuwa OFF au waliendelea KUTESA kwa zamu, maana ile ni Bongo yetu. Ingekuwa aibu kumbaka Michuzi saa au simu.
  Tanzania sasa ni MAFIA kweli. Hizi action nilikuwa nasikia na kusoma jinsi mtoto wa Don Corleon (Sonny) alivyocharazwa risasi sehemu ya kulipia ada ya matumizi ya barabara. Walinzi waliondolewa, kwenye kibanda wakawekwa wauwaji. Aliposimama tu na kufungua dirisha ili alipe ........ Nashindwa kujua hawa walikuwa na lengo la kubeba Laptop tu au huruma iliwaingia na kushidnwa kumaliza kazi. Kama walikuwa naye kwenye sahani tayari na kumuamurisha arudi ndani, kweli watu wana bahati zao. Halafu kituo cha Polisi Arusha na Moshi hawataki kupokea simu. Nafikiri wakushatakiwa ni wengi.
  Don Corleon alijua ni nani walihusika na aliwarudi wote hadi Mkwewe. I hope Jaji ana jamaa zake UWT ambao bila kujali upelelezi wa POLISI, wao wataingia na kufanya ki-vyao. Vinginevyo, kama ni POLISI watalishughulikia hili swala (Kesi ya nyani kwa ngedere) basi Jaji ajuwe Mahindi yamekwenda.....
   
Loading...