Kama Wewe ni Mwanachama wa NSSF, PPF, PSPF... Soma Hapa!!!

Iselamagazi

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,922
6,009
Mfuko wa wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufilisika?

Kwamba serikali ya Tz katika muda tofauti imekopa fedha lukuki toka NSSF na kushindwa kufanya marejesho ktk mfuko husika! Mifuko mingine ya Jamii inatajwa kuwa ni: PPF, PSPF, LAPF pamoja na NHIF. Hii ni habari kulingana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ya 2010/2011. Habari hii siyo nzuri masikioni mwa wanachama husika!

Ikiwa wewe ni mwanachama ktk mojawapo ya mifuko hii, hali hii unaionaje?

Source: Mwanahalisi, ISSN: 1821- 5432, TOLEO Na. 290, 2012.
 
Mi bado sijafikia kustaaf kwa hiyo haitakua na madhara kwangu
 
Dunia nzima haifanyi utani kwenye sekta ya fedha. Wote waliofanya utani hata kama ni WAZUNGU, wameanguka. Sisi pia tunafanya utani na sekta hii nyeti. Watu wasomi lakini tuanachezea uchumi na fedha. Tuache utani jamani, TUTAUMIA.
 
Hoooo! God......!! Tunusuru nahilijanga maana naona sasa nchi inauzwa kimyakimya! Hii inakokwenda hapaeleweki,mi naona watu wamemuweka Mungu kando yatupasa kufunga na kusali sana!
 
Hivi na hawa vigogo wanaoidhinisha mikopo hiyo na kushindwa kufuatilia marejesho na ni wanachama? au! au ndiyo maana wanaongezewa miaka ya kazi
 
Dr Dau huwa anajibu kuwa mfuko una afya njema na unaweza kulipa wanachama mda wowote ndani ya miaka 25 nazidi changanyikiwa
 
haki ya kweli tutshikana!yan me nakatwa kila mwezi najua pesa zangu zipo mahali salama afu hii hii serikali ambayo inatukata kodi bila huruma inaenda kuchukua pesa zetu bila idhini yetu?????halafu sisi tukitaka kukopa kwenye hii mifuko tunakatazwa!hivi hamna uwezekano labda nikahamia PPF ya let say UK au USA hivi??manake hapa bongo wizi umezidi
 
Hizo ni tetesi uchwara!!
Taasisi hizo zina pesa ya kutosha ya kulisha tanzania nzima kwa mwaka mzima, na wastaafu wakapata pension yako kama kawaida.
Acheni kutisha wa2. Shenzi.
 
nchi ilishauzwa na chama cha CHUKUA CHAKO MAPEMA (ccm) unashangaa nini ulitaka hizo pesa aachiwe nani? ni kuchukua tu na kusepa
 
My money is still there. When I retire they will pay me since giving a loan to the government is none of my business. If they lose all the money we will take them to court!!
Mfuko wa wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufilisika?

Kwamba serikali ya Tz katika muda tofauti imekopa fedha lukuki toka NSSF na kushindwa kufanya marejesho ktk mfuko husika! Mifuko mingine ya Jamii inatajwa kuwa ni: PPF, PSPF, LAPF pamoja na NHIF. Hii ni habari kulingana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ya 2010/2011. Habari hii siyo nzuri masikioni mwa wanachama husika!

Ikiwa wewe ni mwanachama ktk mojawapo ya mifuko hii, hali hii unaionaje?

Source: Mwanahalisi, ISSN: 1821- 5432, TOLEO Na. 290, 2012.
 
Miradi ya Nssf yote tunaijua na wasipotulipa tunachukua mchinga complex tunapiga mnada!
 
Ila muda umefika serikali isichezee pesa zetu kule na waache uswahiba wao,NSSF,PPF sio reserve bank zao,waende kwenye Commercial Bank kabisa wakakope huko!!zile pesa ziwe dhamana kulipia nyumba za kununua zinazouzwa NHC,na wengine!!imetosha sasa
 
Back
Top Bottom