Kama Wakenya wanalalamika kuhusu DP World, kuna haja ya Tanzania kuendelea nao?

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,396
12,979
Kuna video nimeiona Wakenya wanalalamika kuwa serikali yao pia imesaini mkataba kisiri na DP World kucontrol bandari zote za Kenya. Kama hii ni kweli, hivi kweli kuna sababu yeyote ya kuendelea na hawa watu? Haiwezekani wachukue bandari zetu zote pamoja na za majirani zetu halafu tuwaamini kuwa ni wawekezaji wenye nia njema!

Kwa jinsi inavyoonekana UAE wanajua kuwa mafuta yao yatakwisha muda siyo mrefu. Hivyo sasa wameamua kuwekeza kwenye sector mbalimbali ikiwemo Usafiri wa anga (Etihad na Dubai Airline), kwenye bandari (DPW), Michezo (Machester City, New Yolk City, Melbourne City, Yokaham, Bumbai City nk), Utalii (dubai City), Crypto hub (Dubai) nk. Kwa jinsi inavyoonekana UAE wako desperate kuwekeza sasa, kwa ajili ya kizazi chao cha baadaye.

Kwa uwekezaji wanaoufanya kwa sasa hasa East Africa ambapo wanataka kuchukua bandari zote Kenya (Mombasa, Lamu nk), Tanzania na Mozambique hautakuwa uwekezaji wa faida kwa nchi husika, bali watakuwa wanajaribu kutake control ili huko mbeleni tusiwape shida kibiashara, yaani tusiwe washindani wao. Strategically, bandari yetu inaweza kuwa mshindani mkubwa sana wa DP World huko mbeleni. Sasa wao wameliona hilo leo wakati sisi hatuoni na wanajaribu kutuzuia kwa njia ya uwekezaji.

Kama kweli DP World ni wawekezaji wakubwa na wana nia njema, kwanini mpaka sasa hawajaweza kuziendeleza bandari za Beira (Mozambique), Durban and Angola kwa kiasi kikubwa au kwa technology kubwa kama ilivyo kwao Dubai? Hapo ndipo utaona kuwa strategy yao au malengo yao ni kucontrol zaidi ili kuhakikisha kuwa Dubai ports zinaendelea kuwa main ports na sisi tunakuwa tegemezi kwao.

Wanachokitaka Kenya na sisi tunakitaka. Wanachokitaka Mozambique na sisi tunakitaka. Wanachokitaka RSA na sisi tunakutaka pia na wenzetu wanakitaka. Sasa hapa unafikiri DP World watawezaje kuturidhisha wote kwa pamoja? Hii ni kama vile ndoa ya wake watatu.

Wenzetu ni makini sana katika uchunguzi kwa mambo yenye faida kwao. Pengine wamegundua udhaifu wa kiongozi wetu mkuu.
Anaweza kuwa hachukui rushwa, lakini washauri wake anaowaamini ni walarushwa wakuu hapo ndipo DPW wanapitia huko.
Tumekwisha hivyo tuchukue hatua haraka
 
Kila ulichosema kiko based on "assumptions"..

Hakuna facts bado wala evidence
Kwa Tanganyika kuna facts, Samia alifunga safari akaenda kuhongwa na waarabu picha yake ikawekwa Burj Khalifa, akatoa bure bandari zetu zote milele, mkataba wa hovyo kuthibitisha hilo upo.

Kuongozwa na mwanamke sio tatizo, tatizo awe hana akili na asiyetaka kusikia kile anachoambiwa.
 
Kuna crip nimeiona Wakenya wanalalamika kuwa serikali yao pia imesaini mkataba kisiri na DWP kucontrol bandari zote za ri DPW watawezaje kuturidhisha wote kwa pamoja...!!? Hii ni kama vile ndoa ya wake watatu.
Huko kenya wamejichanganya sana kitaumana soon,mambo ya kulimishana hakuna kule.
 
Kila ulichosema kiko based on "assumptions"..

Hakuna facts bado wala evidence
Kununua Club za mipira ni assumption ...!!?

Kuwekeza kwenye utalii na Real Estate Dubai ni assumption...!!?

Kuwekeza kwenye Usafiri wa anga ni Assumption...!!?

Kama wanavyowekeza kwenye Mpira, usafiri wa anga, Utalii na Real Estate ..... ndiyo vivyo hivyo wanawekeza kwenye bandari.

Ni STRATEGY!!!
 
Kuna video nimeiona Wakenya wanalalamika kuwa serikali yao pia imesaini mkataba kisiri na DP World kucontrol bandari zote za Kenya. Kama hii ni kweli, hivi kweli kuna sababu yeyote ya kuendelea na hawa watu? Haiwezekani wachukue bandari zetu zote pamoja na za majirani zetu halafu tuwaamini kuwa ni wawekezaji wenye nia njema!

Kwa jinsi inavyoonekana UAE wanajua kuwa mafuta yao yatakwisha muda siyo mrefu. Hivyo sasa wameamua kuwekeza kwenye sector mbalimbali ikiwemo Usafiri wa anga (Etihad na Dubai Airline), kwenye bandari (DPW), Michezo (Machester City, New Yolk City, Melbourne City, Yokaham, Bumbai City nk), Utalii (dubai City), Crypto hub (Dubai) nk. Kwa jinsi inavyoonekana UAE wako desperate kuwekeza sasa, kwa ajili ya kizazi chao cha baadaye.

Kwa uwekezaji wanaoufanya kwa sasa hasa East Africa ambapo wanataka kuchukua bandari zote Kenya (Mombasa, Lamu nk), Tanzania na Mozambique hautakuwa uwekezaji wa faida kwa nchi husika, bali watakuwa wanajaribu kutake control ili huko mbeleni tusiwape shida kibiashara, yaani tusiwe washindani wao. Strategically, bandari yetu inaweza kuwa mshindani mkubwa sana wa DP World huko mbeleni. Sasa wao wameliona hilo leo wakati sisi hatuoni na wanajaribu kutuzuia kwa njia ya uwekezaji.

Kama kweli DP World ni wawekezaji wakubwa na wana nia njema, kwanini mpaka sasa hawajaweza kuziendeleza bandari za Beira (Mozambique), Durban and Angola kwa kiasi kikubwa au kwa technology kubwa kama ilivyo kwao Dubai? Hapo ndipo utaona kuwa strategy yao au malengo yao ni kucontrol zaidi ili kuhakikisha kuwa Dubai ports zinaendelea kuwa main ports na sisi tunakuwa tegemezi kwao.

Wanachokitaka Kenya na sisi tunakitaka. Wanachokitaka Mozambique na sisi tunakitaka. Wanachokitaka RSA na sisi tunakutaka pia na wenzetu wanakitaka. Sasa hapa unafikiri DP World watawezaje kuturidhisha wote kwa pamoja? Hii ni kama vile ndoa ya wake watatu.

Wao wamewapatia za bahari si zote kama sisi
 
Back
Top Bottom