Je, lengo la DP world ni kuua competitors wa Bandari ya Dubai?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,731
Dubai ndio lango la Meli kubwa za ku exchange mizigo Duniani, kwamba Meli zote kubwa zina tia nanga pale zina pakua mizigo inapakiwa kwenye meli ndogo ndio sasa zinasambaa kuja Africa na kwingineko.

Na kumbuka plan ya Bandari ya Bagamoyo kama ingetekelezwa ingekuwa na uwezo wa kupokea meli sawa na zinazo pokelewa Dubai port.

Kwa mujibu wa mkataba huu Bandari ya Bagamoyo ambayo ingeweza kuwa mshindani wa Bandari ya Dubai haitawezekana tena kwa sababu hatuwezi tena endeleza Bandari ya Bagamoyo bila kibali cha DP World.

Kwa hio sasa kumbe lengo la DP world ni kuhakikisha hakuna competitors wanao weza kuja kujitokeza na wakaua Bandari ya Dubai?

Kumbuka kwa Techinolojia ya sasa inawezekana nchi kama Congo, Zambia, Malawi wakachukulia mizigo yao Msumbiji, Pia Congo ikitulia wakajenga njia za reli wanaweza chukulia mizigo yao Angola na kusambaza Congo nzima, sana sisi tukabakia na rwanda na Burundi pekee.

So hapa je ni DP world ni kuzuia Tanzania kwa siku za baadae wasije jenga Bandari yenye ushindani na Dubai?


Kuna mambo nyuma ya pazia hatuyajui.
 
Back
Top Bottom