GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Inasemekana, kuna wakati Wakenya walikuwa wanakuja Tanzania, nafikiri Gairo, kununua viazi mviringo na kwenda kuvifsafisha, kuvigrade, na kuvifanyia packaging kisha kuvisafirisha kwenda sokoni Dubai.
Inasemekana, Wakenya hua wanavifuata vitunguu Tanzania, si kwa ajili ya kuviuza Kenya, bali nchi za nje hasa Dubai.
Inasemekana, hata Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite, kwa miaka ya nyuma, walikuwa wanapendelea zaidi kuuza madini yao Kenya kuliko nchini. Inaonekana kulikuwa na cha ziada walichokuwa wanakipata huko, vinginevyo, wasingejihatarisha kiasi hicho kutorosha madini mpaka Kenya.
Inasemekana, miaka ya nyuma , Kenya ilikuwa ikisafirisha Tanzanite nyingi zaidi kuliko Tanzania, nchi pekee duniani Tanzanite inakopatikana.
Inasemekana, miaka ya nyuma, Wakenya walikuwa wakifuata parachichi nchini Tanzania. Kipindi hicho, parachichi zilikuwa na bei nzuri, lakini walipoacha kufanya hivyo, wakulima wa Tanzania wakaambulia maumivu. Na hayo maparachichi, Wakenya walikuwa wakienda kuyasafirisha kwenda "ng'ambo".
Inavyoonekana, Wakenya wako vizuri zaidi kwenye biashara za "Kimataifa" kuwazidi Watanzania.
Wakenya ni "ndugu" zetu, kama wao wameweza, kwa nini sisi tushindwe?
Haitakuwa jambo jema endapo tutaamua kwenda kujifunza kwao?
Binafsi ninafikiria nimtafute Mkenya aliye vizuri kwenye hilo eneo ili nimfanye "mentor" wangu.
Tanzania tuna fursa nyingi sana. Tunachohitaji ni IDEA EXPLOSION!