Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,860
- 12,293
Habari za asubuhi wanaJF wenzangu?
Ndugu zangu.. binafsi nimekuwa msikilizaji, mfuatiliaji, mtafiti na mchunguzaji wa kila kilichopo au kinachotokea katika nchi yetu. Katika kusikiliza, kufuatilia, kutafiti na kuchunguza huko, nimeweza kugundua kwamba Tanzania tuna Mungu mmoja, mwenye nguvu na wa kweli (haijalishi utofauti wa dini zetu nk)
Najua hapa kuna watu wanaotaka kujua ni kwa nini mimi nimewaza na kuamini kwamba watanzania Mungu wetu ni mmoja. Sasa naomba usome chini ili uelewe zaidi vigezo nilivyotumia kugundua hili.
1. Kupewa nchi yenye kila aina ya resources ambazo nchi zingine hazina. Kumbuka au fahamu kwamba Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa resource nyingi katika East Africa Country au inaweza kuwa ya kwanza au ya pili Africa nzima. Hapa nikiwa na maana kuwa hata hiyo Kongo tunayoambiwa kuwa ina resource nyingi, bado haifikii zile tulizonazo sisi, mfano Congo hawana mlima wenye hadhi ya huu wa kwetu (mlima Kilimanjaro)ambao ndio mlima wa pili kwa ukubwa duniani, pili Congo hawana madini haya tulionayo sisi (Tanzanite) madini ambayo yanapatina Tanzania tu, na sio nchi nyingine yoyote hapa duniani.
Hapo bado sijazungumzia bahari, mito, milima mingine, mabonde na ardhi yenye rutuba nzuri hadi kupelekea baadhi ya nchi zilizopo jirani yetu kuitamani ardhi yetu (kumbuka vita ya Idi Amini kujaribu kuivamia na kuiteka ardhi yetu, mgogoro wa Tanzania na Malawi kuhusu mipaka yetu nk.
2. Ulinzi wa nchi ambao nchi nyingi hazina. I mean baada ya kupata uhuru Tanzania tuliingia katika migogoro mbali mbali ya ndani na nje ambayo ilikuwa ina nia au lengo la kuhatarisha usalama wa nchi yetu. Lakini kwa vile nchi yetu ina ulinzi wa Mungu wetu basi nia na malengo hayo yalishindwa vibaya sana.
Mfano kulikuwa na majaribio ya kumpindua raisi Nyerere mara mbili, lkn majaribio hayo ambayo pengine baadae yangetengeneza mgogoro na mgawanyiko mkubwa wa taifa ambao pengine ungeendelea hadi sasa yalishindwa.
Idi Amini nae alipojaribu kutuvamia Mungu wetu alimuadhibu vibaya na kuionesha dunia kwamba chini ya ulinzi wake sisi hatuwezi kuvamiwa na kushindwa na mtu au nchi yoyote.
Hata kipindi cha kuwasaidia ndugu zetu wa nchi za kusini kupigania uhuru wao. Makaburu waliweza kutuma mashushu, wanajeshi nk kuvamia na kuziadhibu nchi zote zilizojaribu kuwapa hifadhi wanasiasa weusi waliokuwa wamekimbia mateso katika nchi yao, lkn makaburu hao walipojaribu kutumia mbinu hizo kwa nchi yetu walishindwa na wale mashushu wao wote tuliwagundua na kuwatia nguvuni before ya kuleta madhara makubwa nchini kwetu, hivyo hivyo wareno tuliwachapa na kumuweka Samora Machel kitini kwa kutumia nguvu na ulinzi tuliopewa na Mungu wetu.
3. Umoja wetu na mshikamano wetu. Tanzania ni moja ya nchi chache ambazo raia wake tuna Umoja, Upendo na Mshikamano wenye nguvu sana. Ukienda Burundi Kuna matabaka mawili mawili nayo ni:
a) tabaka la wahutu na watusi.
b) tabaka la waongea kiswahili na kirundi.
Tabaka "A" kutokana nchi yao haina ulinzi wa Mungu kama tulio nao sisi ndio lililotumika kuleta vita kubwa nchini kwao, vita ambayo imeacha makovu mengi ndani ya mioyo yao. Pamoja na kwamba kwa sasa wanasema yale mambo ya ukabila yameisha na nchi umekuwa kitu kimoja, lkn unaona kabisa bado hakuna kuaminiana katika ya mtusi na mhutu (hiyo itakuwa hivyo hata ipite miaka 100)
Ukienda Kenya huko licha ya nchi yao kuwa na makabila zaidi ya kumi tofauti lkn bado ukabila umetamalaki kuanzia serikalini, masokoni, madukani nk. Japo Kenyata alijaribu kutaka kuwaunganisha wakenya kupitia lugha ya kiswahili baada ya kujifunza msingi huo kutoka kwa Nyerere, lkn alishindwa kutokana na swala la ukabila kupewa kipaumbele kuliko utaifa.
Ukienda Kenya maeneo ya sokoni utakuta kila mtu anaongea lugha yake na wengine hawaelewani kabisa.
Rwanda, Uganda, Congo nk ni vilevile tu Umoja wao ni wa kuunga unga na kuizuga dunia, lkn ndani ya mioyo yao imejaa mgawanyiko wa makabila, lugha nk.
4. Nguvu ya asili. Pia tumepewa nguvu ya asili ya kuweza kuwadhibiti au kuzidhibiti njia zote zinazoweza kutumika kujaribu kutuangusha. Kama nilivyotoa mfano kuhusu msumbiji na Kaburu kushindwa, lkn pia tumepewa nguvu ya kuweza kuleta Amani hata katika nchi zingine tulizoamua kwenda kuwasaidia kama Comoro nk.
Hata juzi kati Kagame alijaribu kutingisha kibiriti, za ndani kabisa zinasema kama isingekuwa mzee Mwinyi (mzee wa amani na hekima) kuzituliza zile jazba za kijana wa msoga basi leo Rwanda ingekuwa ishaonganishwa kuwa mmoja wa mikoa ya Tanzania, maana kijana wa msoga akishirikiana na mkuu wa jeshi wa kipindi hicho ambae alikuwa na hamu ya kuikamata Kigali usiku mmoja, hivyo akawa anamshawishi mkubwa wake atoe amri akamalize mechi na ubishi wa kijinga jinga wa bwana PK.
Nchi kwetu pia tulishuhudia wale wote waliojaribu kuteteresha amani yetu kupitia dini na siasa wakishindwa vibaya kabla hata ya kuanza.
Kwa resource tulizokuwa nazo na wema tulionao toka enzi za mwl Nyerere wa kukaribisha wakimbizi, na waafrika wenzetu kutoka nchi mbali mbali kama isingekuwa ulinzi wa Mungu basi leo hii nchi ingekuwa kama Congo au Msumbiji ambazo leo hii zipo kwenye vita isiyoisha.
Demokrasia imeshaleta machafuko almost Afrika nzima, lkn kwetu hiyo haijatokea na naamini hatatokea kamwe.
Kwahiyo nashauri viongozi wa serikali, dini na siasa waendelee kutuasa watanzania tupendane na tusibaguane kwa misingi ya dini, rangi, kabila, siasa, jinsia nk. Maana sisi wote Mungu wetu ni mmoja, mwenye Nguvu na Upendo wa kweli na sisi. Yeye anaangalia mioyo yetu tu, na sio dini zetu au rangi zetu.
Mungu ibariki Tanzania.
Ibariki serikali yetu na raisi wetu.
Bariki pia bara letu na dunia yetu kwa ujumla.
Ameen 🤲