Chama ni watu wanaokuja kwenye chama pamoja na mawazo yao. Chama kinajengwa na wanachama. Utamu wa ngoma ingia ucheze. Wakomavu wa akili wanaangalia mambo yote, mazuri na mabaya. Wachanga wanaangalia mabaya tu pasipokuyaona mazuri. Ikiwa wewe unamawazo mazuri usikimbie chama njoo jiunge na wenzako, tutayasikia tutayapima yakikubalika tutayafanyia kazi, lakini kukimbia chama huku ukikosoa bila kubadilishana mawazo na wenzako haitajenga chochote hata mawazo yako utayanyima kutambulika.
Mwanzoni nilikuwa na matumaini makubwa sana na CHADEMA, hadi kufikia mwaka 2010 nikawapigia kura akiwepo Mnyika ilihali nikiwa bado na kadi ya CCM. Nilifikiri mwaka huu labda ningejiunga kabisa CHADEMA na kuifanya iwe na kura yangu ya kudumu.
Kadri siku zinavyoenda naanza kuwaona si HACEDAM si CCM, wote ni wale wale - tena tunaweza kuwaita ni wao na sisi ni sisi. CHADEMA hakina tofauti tena na CCM, na tena inaelekea kubaya zaidi.
Ndani ya CHADEMA huwezi kukwepa mambo ya ufisadi, yapo. Mambo ya ugaidi, udini na ukanda nao unaonekana kushamiri.
Nimechoshwa zaidi na mipango ya matukio ya kuwafanyizia watu (Zitto kulishwa sumu, Msack sijui, Kibanda naye sijui..) haya yote nayaona kama sio mema na yanaanza kuniaminisha kuwa hata Wangwe mtani wangu haikuwa hivi hivi tu! Kumekuwa na kujaribu kujikosha kwingi, sijui Saanane, sijui Zitto, sijui Mnyika, wote hawa wamekuwa sawa na Mwigulu, Ze Mutu na Nape kwa sababu sijaona cha maana wanasema humu JF zaidi ya kujitetea tetea tu kila mara.
Dr Slaa naye akiibuka ndiyo huwa ananichanganya kabisa, ingawa yeye ana kaunafuu fulani. Siku hizi hata ile gwanda yangu ninasita kuivaa, sababu naanza kuhusishwa na ugaidi hata kama sijawahi kuufanya, juzi juzi niliwaona CHADEMA pale Ubungo Plaza wamevaa magwanda nilishtuka kidogo nikimbie, sijui kwa nini nimeanza kupata hofu na magwanda haya.