Kama vile naanza kukata tamaa na CHADEMA

Kama vile naanza kukata tamaa na CHADEMA

Una uhakika wewe ni
Mwanachadema?Je post zako zilizopita hapa JF zinaweza kuku-define?

CHADEMA siyo Combat tu,Ile ni falsafa.Ungekua mwanachadema wa kweli
ungetafuta ukweli kwa tafiti badala ya kukurupuka.Hizi sio sifa za
wanachadema

Kuwa makini na uwe mkweli

Mkuu, vijana wa Lumumba hao, hawaishi vioja... Kinana amekuja kivingine...
 
Unakata tamaa na CDM?lini ulikata tamaa na ccm?mafisadi hayawezi kutiwa moyo na CDM
 
Hakuna hata mmoja alieweza kushauri kitu cha maana, hili ndio tatizo la gwanda humu jf, inaweza kuwa jamaa hakielewi chama chenu vizuri na alistahili kufahamishwa lakini badala ya kumpa muongozo mnaenda kumshambulia, kweli umri ni hekima. Yote aliyo jenga mbowe nyie kenge mnavunja. Muanzisha mada bora ubaki ccm,cdm wamejaa wahuni,mfano umeuona.
 
Hivi hapa Jf kukoje, kama na mimi nikitaka kuweka ujinga wangu hapa nafanyaje, hebu nisaidieni jamani
 
ww mtoa mada utakua umekula hii kitu

images

Hiyo kitu ikiwa hivyo kwa wabena ni mboga sema yeye kala ile iliyokauka kwa kuvundikwa
 
Mwanzoni nilikuwa na matumaini makubwa sana na CHADEMA, hadi kufikia mwaka 2010 nikawapigia kura akiwepo Mnyika ilihali nikiwa bado na kadi ya CCM. Nilifikiri mwaka huu labda ningejiunga kabisa CHADEMA na kuifanya iwe na kura yangu ya kudumu.

Kadri siku zinavyoenda naanza kuwaona si HACEDAM si CCM, wote ni wale wale - tena tunaweza kuwaita ni wao na sisi ni sisi. CHADEMA hakina tofauti tena na CCM, na tena inaelekea kubaya zaidi.

Ndani ya CHADEMA huwezi kukwepa mambo ya ufisadi, yapo. Mambo ya ugaidi, udini na ukanda nao unaonekana kushamiri.

Nimechoshwa zaidi na mipango ya matukio ya kuwafanyizia watu (Zitto kulishwa sumu, Msack sijui, Kibanda naye sijui..) haya yote nayaona kama sio mema na yanaanza kuniaminisha kuwa hata Wangwe mtani wangu haikuwa hivi hivi tu! Kumekuwa na kujaribu kujikosha kwingi, sijui Saanane, sijui Zitto, sijui Mnyika, wote hawa wamekuwa sawa na Mwigulu, Ze Mutu na Nape kwa sababu sijaona cha maana wanasema humu JF zaidi ya kujitetea tetea tu kila mara.

Dr Slaa naye akiibuka ndiyo huwa ananichanganya kabisa, ingawa yeye ana kaunafuu fulani. Siku hizi hata ile gwanda yangu ninasita kuivaa, sababu naanza kuhusishwa na ugaidi hata kama sijawahi kuufanya, juzi juzi niliwaona CHADEMA pale Ubungo Plaza wamevaa magwanda nilishtuka kidogo nikimbie, sijui kwa nini nimeanza kupata hofu na magwanda haya.

Chris Lukosi at work.... We kata tamaa tena ukate na kifo kabisa. CDM HAIWEZI KUWA SAWA SAWA NA ccm KWA SABABU
1. Mafisadi wote wapo CCM lakini hakuna anayewataja... CDM iliwataja
2. Wauza twiga wa nchi hii au watoa zawadi ya twiga wapo CCM
3. Meremeta wapo CCM
4. Kagoda wapo CCM
5. Wale wa kujiuzia Kiwira Coal Mine kwa bei cheeeee wapo CCM
6. Watesaji na wauwaji wa wananchi wapo CCM
7. Haya wa kuotoa leseni ya namtumbo uranium wapo CCM
8. EPA wapo CCM
9. Dowans Wapo CCM
10. IPTL wapo CCM
11. Wanaotoa misamaha ya kodi, wanaokubali mirahaba midogo ya kwenye madini wapo CCM
12. .....
 
Hivi ccm itawaweka watu katika ajira ya kuchafua CDM hadi lini?

Ninyi mnaopangwa mfanye mambo ya hila na uchochezi wa uwongo kama huu, mnaweza kukumbuka kwamba kila nafsi itaonja mauti?

Mnajua kwamba kufa ni mara moja na baada ya kufa ni hukumu?

Mnafahamu kwamba Mungu ni Mungu mtakatifu na mwenye haki?

Mnajua kwamba kwamba siku ukifa, huendi na jk wala mwigulu maana nao wanahesabu zao za kutoa mbele za Mungu?

Mmewahi kujiuliza siku mtakayokufa ambayo haijulilkani mtamwambia nini Mungu kuhusu hizi dhambi mnazozifanya makusudi za kuumiza watu wengine kwa hila?

Mnajua kwamba Mungu hupatiliza wana uovu wa wazazi wao naam hata kizazi cha tatu na cha nne; na kwamba kwa dhambi hizi mnatengeneza laana kwa vizazi vyenu?

MKITAMBUA HILO, MTAJUTIA MAOVU YENU NA KUTUBU DHAMBI HIZO NA KUZIACHA. ANAYETAKA UMSINGIZIE MTU, UMNG'OE MENO, KUCHA NA MACHO AMA UMUUE KWA HILA, MWAMBIE AKAFANYE MWENYEWE. UTAJIPONYA NAFSI YAKO NA GHADHABU YA MUNGU NA UTAOKOA VIZAZI VYAKO NA LAANA ZA KURITHI.

TUBUNI SASA MKAGHAIRI HIZI TABIA ZENU ZA KUSHINDA MTANDAONI MNASINGIZIA WATU UWONGO HUKU MKUJUA.

TAFUTENI KAZI ZA KUJIPATIA KIPATO KWA NJIA HALALI BADALA YA FEDHA ZA LUMUMBA ZILIZOJAA DAMU.

NINAWAONYA KWA KUWA NAWAPENDA. MSIDHANI KWA KUATHIRI WATU KWA HILA ZENU MTAMSHAWISHI MUNGU KWAMBA HAMKUJUA, MLITUMWA AMA MLILAZIMISHWA. MWOGOPENI MUNGU ALIYE NA UWEZO JUU YA MWILI NA ROHO.

The finest warning ever!...advice at its best.
 
Watanzania tuilinde nchi yetu kwa kukemea vitendo vya kiharamia na kigaidi.

Ni kweli kabisa mkuu,kama vile alivyofanyiwa Dk Ulimboka,Daudi Mwangosi,Kibanda etc.
 
Ccm ni ccm na chadema ni chadema, kwa maana kwamba chadema ni magaidi na ccm ni magamba
 
Mwanzoni nilikuwa na matumaini makubwa sana na CHADEMA, hadi kufikia mwaka 2010 nikawapigia kura akiwepo Mnyika ilihali nikiwa bado na kadi ya CCM. Nilifikiri mwaka huu labda ningejiunga kabisa CHADEMA na kuifanya iwe na kura yangu ya kudumu.

Kadri siku zinavyoenda naanza kuwaona si HACEDAM si CCM, wote ni wale wale - tena tunaweza kuwaita ni wao na sisi ni sisi. CHADEMA hakina tofauti tena na CCM, na tena inaelekea kubaya zaidi.

Ndani ya CHADEMA huwezi kukwepa mambo ya ufisadi, yapo. Mambo ya ugaidi, udini na ukanda nao unaonekana kushamiri.

Nimechoshwa zaidi na mipango ya matukio ya kuwafanyizia watu (Zitto kulishwa sumu, Msack sijui, Kibanda naye sijui..) haya yote nayaona kama sio mema na yanaanza kuniaminisha kuwa hata Wangwe mtani wangu haikuwa hivi hivi tu! Kumekuwa na kujaribu kujikosha kwingi, sijui Saanane, sijui Zitto, sijui Mnyika, wote hawa wamekuwa sawa na Mwigulu, Ze Mutu na Nape kwa sababu sijaona cha maana wanasema humu JF zaidi ya kujitetea tetea tu kila mara.

Dr Slaa naye akiibuka ndiyo huwa ananichanganya kabisa, ingawa yeye ana kaunafuu fulani. Siku hizi hata ile gwanda yangu ninasita kuivaa, sababu naanza kuhusishwa na ugaidi hata kama sijawahi kuufanya, juzi juzi niliwaona CHADEMA pale Ubungo Plaza wamevaa magwanda nilishtuka kidogo nikimbie, sijui kwa nini nimeanza kupata hofu na magwanda haya.

we ni takataka.......silly
 
Back
Top Bottom