Kama uwekezaji ndio huu tumekwisha

KELVIN GASPER

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,066
454
Dada wa kichina muwekezaji/muajiriwa akimuhudumia mteja saloon ya blue palace sinza mapambano.Wabongo tuko mbali hata kupaka rangi kucha tunawekeza.
 

Attachments

  • Saloon_mchina.JPG
    Saloon_mchina.JPG
    16.1 KB · Views: 222
Rejao

Most of your comments are cynical....even to issues that matter most. At times I fail to understand what kind of a person you are? Huwa sikuelewi kama ni utanzania au ndo mizaa kwenye mambo muhimu...comment yako imeniuma nikaona nikuulize
Tunajifunza kutoka wao...hawa wanakuwa mentor wetu!
 
Dada wa kichina muwekezaji/muajiriwa akimuhudumia mteja saloon ya blue palace sinza mapambano.Wabongo tuko mbali hata kupaka rangi kucha tunawekeza.

jana nilikua jangwani sea breeze,.the only black servants that i saw ni ma waitress, wamasai na ma baunsa.,counter alikuepo mzungu, cashier mzungu,.ndo nikashangaaaa
 
Rejao

Most of your comments are cynical....even to issues that matter most. At times I fail to understand what kind of a person you are? Huwa sikuelewi kama ni utanzania au ndo mizaa kwenye mambo muhimu...comment yako imeniuma nikaona nikuulize

Sisi watz tumezoea kuquestion vitu ambavyo tuna majibu navyo. Tunajifunza mambo mengi sana kutoka kwa wachina. Huwezi kuongelea construction na mechanics bila kuwagusa wachina, huwezi kuongelea biashara bila kuwagusa wachina. Ni muda wa sisi watz kujifunza kutoka kwao may b na sisi tunaweza kuwa na attitude kama zao za kufanya kazi kwa nguvu na kwa bidii!
 
Siyo kila king'aacho ni dhahabu, vivyo hivyo siyo kila raia wa nchi nyingine aliyepo hapa Tanzania ni mwekezaji. Kumbuka mtu kama huyu analazimika kufanya kazi yoyote halali ili apate mkate wa kila siku.
 
Wakuu Reajo na wengine, hawa wachina wametapakaa sehemu nyingi sana duniani na Afrika kwa sasa ndio kwao kwani wapo kila pembe.

Hata katika nchi zilizoendelea hawa wasichana na wavulana wa kutoka China wenye vipaji katika kutengeneza kucha, nyusi na hata kutoa ushauri wa dawa za kienyeji za kichina, ndio wanaofanya shughuli hizi.

Juzijuzi nilikuwa nyumbani Tanzania kutembea kidogo, na kuna siku nikawa napitapita kutembea maeneo ya Kariakoo. Kuna sehemu mtaa wa Narung'mbe niliona wachina wanafanya usafi na sehemu hio inaonekana panafanyika ujenzi.

Walikuwa wanafagiafagia na kutumia ndoo za maji kwa kupiga deki eneo linalozunguka jengo hilo. Lakini nikaangalia upande wa pili wa barabara na nikawapona vijana wa kitanzania wamekaa wanapiga soga na wengine wakicheza bao.

Sasa hapo pana mambo mawili, moja ni kwamba inawezekana mkandarasi anajenga jengo hilo au washirika wake wanatoka China na inawezekana waliamua kuajiri wachina wenzao.

Pili ni kwamba utandawazi kwa nchi zetu umefungua kila kitu mpaka vitabu vya sheria za kwetu ambapo serikali inalazimika kuwasikiliza hao wawekezaji ambao hudai kuwaleta raia wa kutoka nje ili waje kuwafanyia kazi zao ambazo zingeweza kufanywa na raia wenyeji.

Au ni uzembe tu katika kila kitu ambapo wageni wanakuwa huru mno katika kufanya watakacho.
 
Halafu watu wanasema hakuna kazi za kufanya, hapo ndipo nnaposhangaa mimi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom