Kama unapata changamoto hizi Dar nenda mikoani

Kama unapata changamoto hizi Dar nenda mikoani

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Hiyo ndo i like..
Mikumi ya chamazi kule...

Sio kila siku mnashinda sehemu hamna kelele hiyo jau bana
Mie napenda sana Heka heka. [emoji23][emoji23][emoji23]
Vigoma, vibati, yaan full kurushana roho. Uwiiiiih
 
Vipi kuna shughuri? Niandae kabisa dela langu la kusasambua.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Unaweza kusasambua....
Utayaweza ya uswazi.....

Leo kwanza nipo free upo wapi nikuje
 
Mkuu acha visingizio ondoka achana na mambo ya kwenda kugeuka na dala dala na bado unakosa siti😀
 
Kama unapata changamoto hizi Dar nenda mikoani bado nchi hii ina ardhi kubwa sana tena yenye rutuba na fursa nyingine nyingi

1. Unaamka saa kumi kuwahi Gari
2. Unafika kwako saa nne usiku na kuendelea sababu ya changamoto za usafiri
3. Kipato chako kinaishia kwenye kodi na usafiri
4. Unaishi zaidi ya kilomita 40 kutoka eneo lako la kazia
5. Maisha yako ni joto, mbu na kugombania dala dala
6. Muhanga wa mafuriko kila mwaka

Nakuhakikishia mikoa 27 iliyibaki ukitoa Dar ndipo ulipoandikiwa kutoboa

Kumbuka kuteseka sio sifa na hakuna kombe la kuteseka

Ni mtazamo tu
Wengine wanaona sifa kuteseka mkuu! Na wa hivyo ni wengi sana!
 
Mikoani watu wabahili biashara hazitembei wanachonunua wao ni pembejeo za kilimo tu.
Ukiuza maji hawanunui, soda zitaexpire dukani, ndizi ndio kila mtu ana mgomba nyumbani, mboga za majani kila mtu anazo kwenye bustani. Hutoboi kirahisi.
Ila DSM ujanja ujanja unamake hela. Kuna kijana yuko pale Sinza, nguo anafua, gari anaosha, usafi anafanya nyumbani kwako. Kwa siku hakosi elfu 30-40
 
Back
Top Bottom