Kama umezaliwa Dar na maisha bado magumu mjini toka nenda mikoani

MIRA01

JF-Expert Member
Sep 18, 2023
298
651
Jiji lina vijana wengi sana ambao kwa namna moja ama nyingine wamekulia ama kuzaliwa kabisa katika jiji la Dar es salaam na wengi wao wameishi maisha ya hadhi hapo miaka ya 90s-00s, wakazi wengi wamezaliwa sinza -kinondoni na baadaye kuamia Tabata na maeneo mengine

Wengi wao kwa sasa ni watu wazima kabisa yaani ni 20s plus na raman ya maisha ni haisomeki kabisa kwa upande wao, mbaya zaidi wapo wenye elimu ya TIA , UDSm na vyuo vingine vingi vya mjini, lakin kiukweli maisha yao ya kesho hayapo kwenye mboni za macho yao

Nimefanya utafiti mdogo pia kwa wakazi wenye maendeleo makubwa kwenye jiji la dar es salaam zaidi ya asilimia 90 bila kupepesa macho ni wageni tena wale wageni waliokuja ukubwani wakitokea mikoa kama kilimanjaro, mbeya , njombe, mwanza na mengineyo, kama unataka kuamini hilo nenda kariakoo kwenye maduka makubwa utagundua baada ya uchunguzi ya kwamba wamiliki wengi wa hayo maduka ndio wamiliki wa real estate kubwa kwa dar es salaam na pia hao hao ndio wamiliki wa majengo zaidi ya asilimia 95 ukitoa ya serikali

Kwa kijana kama ramani hazisomi kabisa na hauna kitu kabisa nenda mikoni na moja ya mkoa ambao na shauri ni pamoja na upande wa nyanda za juu kusini jumuisha kuanzia Iringa, Njombe, Songea, mbeya, songwe, sumbawanga, katavi ni moja ya mikoa ambayo mambo mengi wapo nyuma yaani namaanisha fursa nyingi ni mbichi haswa

Ukifika kwenye moja ya mikoa hiyo jifunze tamaduni zao na namna gani wanaishi na kuwa humble sana usionyeshe wewe ni watofauti ni watu wanaopenda vya kwao na wanapenda kuwapa fursa wakwao lakini wengi wao bado hawana macho yakuona fursa sasa kwa wewe mwenye elimu yako na umeishi kwenye jiji kubwa kama dar basi nirahis kuziona fursa na kuzifanyia kazi

Nimependekeza kwa kuanzia upande wa nyanda za juu kusini mwa nchi yetu kutokana na gharama nafuu pia za maisha kuwa ni chini zaidi ya maeneo yote ya Tanzania kwa hiyo chochote unachozalisha ni rahis zaidi kukutunza bila kukitumia

Jambo jingine kwa mtafutaji usitumie sana muda mwengi kuishi kwenye maeneo hayo unapopata faida ya kujitosheleza basi sogea mbele kwenye miji iliyochangamka kama Mwanza, shinyanga-Kahama, geita huko utapata changamoto zaidi ya biashara lakin utakuwa haraka tena mara mbili au zaidi ya ulichotoka nacho nyanda za juu kusini.

Ukifata mlolongo huo kwa miaka 5 hadi 10 ukajitosheleza rudi tena dar es salaam ukiwa na mtaji wa kutosha pamoja na uzoefu wa kutosha kwenye kazi zako haswa kwa mfanya biashara itamsaidia zaidi.

WASHINDAO NI WALE WANAOJARIBU NA KUANGUKA LAKINI HAWAKATI TAMAA🫶
 
Tatizo ni mzunguko wa Hela mkuu,,MIKOA mingi ya Tz Hela ni za msimu mfano kipindi Cha mavuno ndio angalau hata biashara zinaenda kikipita hicho kipindi njaa Kali Hamna Hela hata biashara nying haziendi

Labda kama unataka kuivest kwenye kilimo sawa Kwa MIKOA uliyotaja kweli panafaa.
 
Back
Top Bottom