Mtasema yoooote lakini bado tuu Amerika itabakia kuwa hivyo na Ulaya itabakia kuwa hivyo hivyo hata siku moja utoweza kulinganisha na Afrika, maana hata uwe na mipesa yako Afrika siku umeugua ndio utajua kwanini mtu anaona bora apige box la maisha Ulaya na Amerika,, hoja mbovu sana hii na mara nyingi watoa hoja hizi unakuta wameenda Ulaya wiki tatu mbili au miezi miwili wanakuja na maneno haya, ndio nyinyi mnanunua kiwanja bilion 2 Mbezi barabara vumbi tupu, maji hakuna, ukiugua ghafla mpaka upate huduma ya kwanza tayari umeshakufa, shule na vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu hakuna ,umeme wa mgao,bado hapo hapo heti ukiwa unaingiza Milion kwa mwezi Bongo utaishi kama Ulaya Mhhhhh, Viongozi wako wa nchi malaria tuu kidogo wanakimbilia Ulaya, lini uliona mwananchi wa ulaya anakuja Bongo kutibiwa, kuna vitu vingi sana kwa wenzetu ambavyo ni muhimu kwa mwanadamu wa kawaida lakini Bongo labda uwe kama Bakhresa au Mengi ndio utavipata, tusidanganyane au kukatisha watu tamaa,wache watafutaji wakajitafutie,