Kama una uwezo huu usikimbilie Majuu!

Kama una uwezo huu usikimbilie Majuu!

Mbona vikazi vyenyewe vya kishenzi tu hutoki jasho lkn unapata mpunga wa maana!?

Kumbe bora nisepe tu... kuna jamaa kaniambia nimtafutie 4m, naingia sweden fresh adi kazi nakuwa nshataftiwa nikifika naanza mzigo tu🙂🙂..... walah mwakani mwez april nasepa.... maana hapa kazi hamna af tunaambiwa tuchape kazi
 
Katika harakati za maisha Mara nyingi kila mtu anaona bora nchi hii ama ile!ndio maana utakuta wachina wanakimbilia Tanzania na Watanzania wanakimbilia China,Wakenya wanakimbilia Tanzania na Watanzania wanakimbilia Kenya!
Ili mradi kila mtu ameona nikienda sehemu Fulani basi naweza kufanikiwa .
Lakini Leo kwa ushauri tu wa bure kama unaweza kumake 1milion tsh kwa mwenzi ukishaondoa matumizi yako na elimu yako ni ya kawaida ama huna kabisa trust me Ulaya kama hujaenda shule ni kazi bure!
USD 10 kwa saa inaonekana kubwa lakini kiuhalisia ni kupaka rangi upepo
Sio hilo tu kuna baadhi ya nchi hata kama umesoma wewe watakuona pumba tu. Kuna nchi ambayo wananchi wake ni ma-racist sana.
 
Ulaya haina kitu. Msibabaike na Ulaya watanzania. Wenyewe hivi sasa wana matatizo makubwa sana ya kiuchumi. Wananchi wao wako desperate. Europe na Amerika zimekumbwa na wimbi la watu kutaka utajiri wa haraka haraka bila kufanya kazi, matokeo yake ile spirit ya Innovation ambayo ilikuwepo katika nchi kama England karne ya 19 na 20 haipo tena. Waingereza wanapoteza kila kitu kwa Marehemu ya mahesabu pesa kwa kufungua mabanks. Hivi sasa yanawstokea puani.

Ndugu zangu watanzania nawaomba tuipende na kujivunia nchi yetu. Tusipende kuiga maisha ya wazungu. Wao wenyewe hawana mwelekeo hivi sasa. Sisi tufanye ya kwetu na tuchukue tu yale muhimu kutoka kwao.

Wazungu wamejiingiza wenyewe katika mitego ambayo hawawezi tena kujikwamua. Watakwamuliwa na mlipuko kwa sababu hayuko mtu ambaye yuko tayari kuachia anayo yafanya na faida aliyo pata.
 
Mkuu acha hizo, per day unaweza make up to 120 USD, na wanaposema wanalipa kwa lisali usidhani wanahesabiwa kwa masaa nane ina depend unapiga mchongo gani kuna wanaofanya data entry, wanaoosha vyombo, kuna wanaosafisha masehemu , mfano nakumbuka nje ya kazi yangu ya kuajiliwa nilipata kikazi cha kuwa naenda kusafisha sehem ambapo wanapaki magari, watu walikuwa wanavuta sigara wanaweka vipece vibaya , kazi hii niliifanya kila baada ya kutoka kazin kwangu, na ilikuwa 60 USD per hour nafanya 1 hour daily​
Part time job nyingine ilikuwa kusambaza business cards na kila cars 1 ni 0.5 USD, hivo nikisambaza 200 kwa siku nina 100 USD, japo nilikuwa sivisambazi ukweli nilikuwa naweka kwenye dustbin naenda kudai mpunga, hahaha wabongo tumelogwa​
Sasa inakuwaje mtu anasema si lolote si chochote... au maisha ni. Magumu huko ughaibuni kuliko Bongo
 
Hoja yako na ushauri hauna nguvu kumsaidia mtu ambaye hana ajira kwani kiufupi umezingatia mwajiliwa hapo, vipi kwa mtu kama mimi ambaye sina kazi, na mm nisiende huko mang'ambo
 
Sio hilo tu kuna baadhi ya nchi hata kama umesoma wewe watakuona pumba tu. Kuna nchi ambayo wananchi wake ni ma-racist sana.
Upo sahihi kabisa, mzungu hawezi kukuthamini mtu mweusi hata siku moja. Vinginevyo uwalambe miguu sana kwa kukubaliana na mambo yao yote ya hovyo hovyo kama ushoga
 
Sawa kabisa mwenye nacho anatamani kuwa nacho zaidi Ole wake asiye nacho, maana hata kile kidogo akiwaziacho kinaporwa na waliomtangulia kuwa nacho.Naafiki kabisa maisha ni mzunguko lakini kuna mahali ukifikia kila kitu kikasimama basi hata wazo la kwenda ughaibuni nalo litasimama pia.Ni ukweli usiopingika kuwa mwendaji yu heri kuliko mkaa bure maana huenda hata akaokota.Kwenda ughaibuni pasipo malengo ni shuruba lakini kwa yiule aendaye kwa malengo ya kutafuta yamkini hiyo bahati ikamwangukia,Hata hivyo kama akikosaaa atakuwa amejifunza kwamba alikotoka aliacha utajiri mkubwa akidhania atakakoenda atapata zaidi.....Aitwaye kutafuta asiache kuitika wito lakini asiye na mwito huo basi na aridhike na pale alipo.
 
Back
Top Bottom