Tochuku
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 5,283
- 8,365
Leo nmekutana na habari kuhusu Tanzania kuingia mkataba wa uchimbaji Helium, kwamba Tanzania tutapata 17% tu huku mwekezaji akipata zaidi ya 83%
Nikiangalia kiundani mkataba huu wa Helium One (Southern Rukwa, Tanzania) na Serikali ya Tanzania kuhusu uchimbaji wa helium katika eneo la Southern Rukwa una mambo kadhaa ambayo nimeyabaini
Mgawanyiko wa umiliki na faida ni 83% kwa 17%,, nikiwa na maana ya Helium One ina 83% ya hisa, huku Serikali ya Tanzania ina 17% kama "free carried interest"(hisa bila ya kuwekeza).
Free carried interest inamaanisha serikali haitakiwi kuwekeza pesa yoyote katika mradi, lakini itapata asilimia 17 ya faida.
Kwa mazingira ya sasa, 17% ni chini ya kiwango cha kawaida katika nchi nyingine za Afrika kwa mfano, Nigeria na Ghana mara nyingi wao hupata 20 hadi 30% kwa mikataba ya rasilimali za nchi.
Hatari nayoiona ikiwa bei ya heliam itapanda kimataifa, Helium One itapata faida kubwa, huku Tanzania tukibaki na sehemu ndogo. Serikali haijatakiwa kuwekeza, hivyo haina risk ya kifedha ikiwa mradi hautafanikiwa lakini kwa uhitaji mkubwa wa madini haya ni ngumu kuamin ya kua mradi hautoweza kufanikiwa, hiko kitu hakipo.
Pia kwenye uwakilishi na udhibiti wa Bodi ya Kampuni, bodi ya Songwe Helium Ltd itakuwa na wanachama 5, nikimanisha 3 wanateuliwa na Helium One na 2 wanateuliwa na Serikali ya Tanzania, Je, hii inatosha kudhibiti mradi? Jibu ni Hapana, kwa sababu Helium One itakua na kura zaidi katika maamuzi muhimu kama matumizi ya fedha, upanuzi wa mradi, na mauzo. Pia serikali hawezi kukataa maamuzi yoyote yanayoweza kudhuru maslahi ya taifa.
Upande wa malipo ya leseni na mapato ya Serikali, Helium One imelipa USD 960,000 kwa mwaka wa kwanza kama "kishika uchumba" ,,,kulinganisha na sekta nyingine, kama vile madini ya dhahabu, malipo ya leseni kwa miradi mikubwa mara nyingi huanzia USD 1-5 milioni kwa mwaka. Mkataba ulipaswa kua na masharti ya kipato cha ziada (royalty) kwa kila kiwango cha helium kinachouzwa. Pia kiwango cha malipo kinachopanda baada ya miaka kadhaa.
Tukirudi kwenye faida za kijamii na uchumi ni kua mradi unaweza kuajiri watanzania wengi, hasa katika ujenzi na uendeshaji pia miundombinu kuboreshwa kama barabara, umeme, na maji katika eneo hilo. Hatar inayoonekana ni Ikiwa kutakua hakuna mikataba madhubuti, faida hizi zinaweza kuwa kidogo sana kuliko inavyotarajiwa.
Helium ni rasilimali muhimu kwa teknolojia haswa kwenye MRI, semiconductors, space tech n.k,
Bei yake na soko lake linaweza kua kubwa na kupanda katika miaka ijayo kwa sababu ya uhitaji mkubwa na upungufu wa vyanzo vya upatikanaji wake
Hivyo kwa 17% tu, faida kubwa itaenda kwa kampuni ya kigeni.
Serikali inapaswa kuwa na "windfall tax" (ushuru wa ziada ikiwa bei itapanda zaidi ya kiwango fulani).
Kwahio kwa kuhitimisha faida chache ama ndogo sana ni kwa Serikali haijatakiwa kuwekeza (free carried interest). Pia inaweza kuleta ajira na miundombinu.
Hasara ni kua 17% ni kidogo sana kulinganisha na nchi nyingine. Pia udhibiti wa bodi ni mdogo, kampuni ina nguvu zaidi.
Pia hakuna masharti ya kutosha ya kuhakikisha faida ya muda mrefu.
Mapendekezo yangu ya kuboresha Mkataba na pia mikataba mingine ambayo inajumuisha rasilimali za nchi
Kuongeza hisa ya serikali hadi angalau 20-25%, pia weka masharti ya "windfall tax" ikiwa bei ya helium itapanda zaidi ya kiwango fulani. Ongeza uwakilishi wa serikali kwenye bodi kwa mfano, 3 wajumbe badala ya 2. Pia kuhakikisha malipo ya leseni yanapanda baada ya miaka 5. Kingine la mwisho kutengeneza mikataba inayolenga jamii ya wenyeji kwanza kama ajira za kwanza kwa wenyeji na uboreshaji wa miundombinu.
Asalaam Aleykum....