Kama una degree/ diploma na unashindwa kujiajiri wewe ni mzigo kwa Taifa

Kuna vitu vingine tuwe wwazi utaenda kulima labda kijishamba lakini shamba la ukweli uwe na mtaji wa kuandaa shamba upate mbegu bora palizi dawa na kadhalika ukitaka kujiajiri mafunzo 50 ya chini kabisa elfu kumi bado huna mtaji so kungekuwa na solution sawa ukitaka mkopo lazima muwe na vikundi mtengeneze hisa ili kuweza kukopa wakati pesa huna jamani too much
Unatakiwa uanze kidogo na shamba dogo ukipata faida unaongeza. Hata Bakhresa alianza kwa kushona viatu Kariakoo.
 
Inatakiwa graduate wazitumie elimu zao kujiajiri utakuta mtu amesomea business au kilimo bado analilia ajira! Kama sio upuuzi ni nini? Elimu yao ina faida gani sasa?
Hivi unazani ukisoma kilimo ndio ukimaliza tu unaanzisha shamba? Huyu msomi kafundishwa kilimo chenye tija ambacho ili uanzishe lazima uwe na mtaji, unajua gharama ya trecta? yaani mawazo ya watu wengine hadi unashangaa hivi unazani ukimaliza tu udaktari basi unaenda kufungua hospitali unajisahaulisha kuwa hata mkasi unauzwa
 
sasa kila mtu akijiajiri nani ataajiriwa kufanya kazi za waliojiajiri??? robots au???
 
Nachofahamu mimi Kijana niliye masiki mpenda Utajiri ni kwamba Pesa Hutafutwa kwa Pesa na sii vingine, Akili na Maarifa(Degree/Diploma) hutumika tuu katika mpangilio na Matumizi ya Hizo pesa. Vijana wana Degree ila hawana Pesa so unachokiongea ni Karibu na Matusi. Kwani ni nani Kijana aliye kati yetu ambaye hataki kumiliki mradi wake Peke yake?? hao walio-ajiriwa ni Njaa tuu imewafikisha Huko Mkuu, wangekua na Pesa nao wangemiliki Miradi yao.
 
Wanasiasa wasingekuwa wanaahidi kuzalisha ajira katika majukwaa ya kampeni...wewe mtoa mada utakuwa chama cha kijani maana ndo mawazo yenu hayo mkishachaguliwa na kushika madaraka yaan mnasahau kabisa kama mliahidi kutengeneza ajira kwa wapiga kura wenu

Pia sio kila mtu ana spirit ya kifanya biashara mfano mzuri Wassira yeye hawezi chochote zaidi ya siasa
Hahahahaa........ni kweli kabisa, ikiwa fursa zipo kibao...mbona wengi wanang'ang'ania ubunge?! Fursa si zipo nyingi bhana!
 
Darasa la saba wamejiajiri degree holder hawawezi. Hawa ni wa kutandika viboko

Cha msingi kiongoz tupe plan za ajira coz mwenyew nimemaliza O-level na nipo tu kitaa sina ajira nasubiri matokeo huku nikiangalia nini nifanye ila hadi sasa sijapata uamuzi sahihi. So kama vipi toa plan nini tufanye kuweza kujiajiri ila sio kusema tu tujiajiri. Tunashindwa broo!
 
Kwa theory kujiajiri ni rahisi na inawezekana ila ikija hali halisi ni tofauti
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri. Mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu.

Vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo.
Mzigo na wale wenye ajira miaka zaidi ya 10 alafu wanaendelea kuroga wabaki ofisin waoga wa kujiajili na sio anaetoka chuo lekebisha thread yako ili ilete maana
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri. Mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu.

Vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo.
Hivyo unavyotaka wakafanye unataka wakabahatishe. Unajua kwanini nchi yetu haiendelei, ni kwasababu ya watu kama nyie. Yaani mtu kasomea udaktari unampa wizara ya maji.

Yaani unataka wakafanye kilimo bila taaluma. Eti kuuza maji wewe ndo unaona maisha tayar wameyapatia
 
Mkuu wasomi wameshapewa msemo na wanasiasa unaitwa "mitaji iko wapi"
We ndo bwege kwel kuna watu wamejiajili na kujisomesha lkn mwisho wa siku kabla awajatimiza malengo serikali yako mara wafanyabiashara wadogo watoke mjini mara wasikae barabarani mara wakamatwe na city mgambo kujiajili sio kwa kusema jaribu huone ndo utaelewa kukopesheka ngumu acheni ujinga jmn kilimo watu tunafanya ila sasa kuuza kuna changamoto ushuru mara zao ili mpk sijui likomae asie jaribu kujiajili na kua mjasiliamali utajulikana tu maneno yake
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri. Mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu.

Vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo.
Magufuli yeye kajiajiri?
 
Back
Top Bottom