Kama una degree/ diploma na unashindwa kujiajiri wewe ni mzigo kwa Taifa

Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo
Fikiria kabla ya kubwabwaja
[HASHTAG]#ajira[/HASHTAG] zingekua rahis maprofesa na madaktar wangejilimiaga tu na wewe usingekua unashinda jf.......hujiuliz kwann madkt wengi na pfors wameajiriwa???
 
Waliosomea kazi kama ualimu, udaktari, lazima walilie ajira za serikali, wale waliotoka vyuo vya ufundi stadi wanaweza kujiajiri, Je aliesomea utawala atajiajiri vipi? Au apindue uongozi atawale? Kwa ufupi ni kwamba vyanzo vya ajira hususani viwanda vikubwa na vya kisasa hatuna.Assume wewe ni graduate mwenye degree 1/2/3 umetoka chuoni halafu unarudi kijijini kwenu kulima mihogo kama ajira ya kujiajiri.
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri. Mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu.

Vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo.
Hawataki kuchafuka,pia wana aibu sana we waache tu tutakutana nao uzeeni
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo
Fahamu hivi:
Income (kipato) = Consumption (matumizi) + Savings (akiba)
Savings (akiba) = capital (mtaji) = Investment (kujiajiri).

Huwezi kuwekeza kama huna mtaji na huwezi kuwa na mtaji kama hujapata shughuli ya kujiajiri ili ujiingizie kipato kitakochokuwezesha kimtaji.

Hata kama una taaluma bora kiasi gani, huwezi kusimama peke yako bila kujifunza kwa watangulizi wako (ajiriwa) mfano ni wanasheria na wahasibu.
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri. Mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu.

Vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo.
Unaishi dunia ya ngap ambayo unapewa shamba bure,unapewa mbegu bure,unapewa mbolea bure,na unalimiwa shamba bure kabisa bila capital.
Tuache kufikiri kama ndoto twende na reality.
 
Hapa ndipo ninapo kumbuka maarifa ya kitabu cha RICH DAD, POOR DAD.

RICH DAD, atakufundusha namna ya kutengeneza pesa kwa kuwekeza miradi mbalimbali etc.

POOR DAD, anasisitiza zaidi ufaulu mzuri darasani akiamini kwamba ukiwa na ufaulu mzuri utapata kazi nzuri na ulinzi utakuwepo (yani utaajiriwa)

Wazazi na serikali yetu imetufanya tuamini katika kuajiriwa na siyo kujiajiri.

Mawazo yetu yanahitaji strong reformation ili tuweze kwendana na kazi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia.
 
Unajiajiri wapi wakati elimu yako ilikuwa therory tu bana wewe
Inategemea kitu ulichosomea.

Kama ulisomea kitu ambacho hakiwezi kukusadia japo ujiajiri ni shida sana na hapo utakuwa huna namna nyingine tofauti na kusubiri uajiriwe na mtu mwingine ili amtengenezee kipato chake.
 
Hapa ndipo ninapo kumbuka maarifa ya kitabu cha RICH DAD, POOR DAD.

RICH DAD, atakufundusha namna ya kutengeneza pesa kwa kuwekeza miradi mbalimbali etc.

POOR DAD, anasisitiza zaidi ufaulu mzuri darasani akiamini kwamba ukiwa na ufaulu mzuri utapata kazi nzuri na ulinzi utakuwepo (yani utaajiriwa)

Wazazi na serikali yetu imetufanya tuamini katika kuajiriwa na siyo kujiajiri.

Mawazo yetu yanahitaji strong reformation ili tuweze kwendana na kazi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia.

Hats marekani Na ulaya vijana wanaomaliza vyuo wanategemea kuajiriwa! Kwenye third world mnakuja Na misemo uchwara!
 
Kuna vitu vingine tuwe wwazi utaenda kulima labda kijishamba lakini shamba la ukweli uwe na mtaji wa kuandaa shamba upate mbegu bora palizi dawa na kadhalika ukitaka kujiajiri mafunzo 50 ya chini kabisa elfu kumi bado huna mtaji so kungekuwa na solution sawa ukitaka mkopo lazima muwe na vikundi mtengeneze hisa ili kuweza kukopa wakati pesa huna jamani too much
 
Hats marekani Na ulaya vijana wanaomaliza vyuo wanategemea kuajiriwa! Kwenye third world mnakuja Na misemo uchwara!
Misemo uchwara iko wapi kwenye hiyo comment yangu Mkuu?

Elimu ya Marekani, Ulaya na Tanzania vinafanana?
 
wasira ni mzembe tu.. mtu ukiitumia akili yako vizuri maisha yanakwenda...

binafsi ni graduate na nimejiajiri.. na maisha yanakwenda tu..

maana ajira zipo chache sana hatuwezi kupata wote...

karibu kiwandani kwangu upate huduma

kwa kibiashara kidogo tu nalipa kodi, kama usafiri naendesha, na maisha yanakwenda tena bila deni na mtu.

na marafiki walioajiriwa daily wananikopa pesa...

mpaka nashindwa zitamani ajira zao tena

Laki si pesa wewe mwenyewe unatetea ccm ili kupata kicheo ili kupunguza njaa ya tumbo lako, na ukute umeajiriwa mshahara hata million moja haufiki, ila ukiwa JF wawaambia wenzako wajiajiri unafikiri kuna mtu anayependa hyo hali. Wasira mwenyewe kakaa serikalini tangia enzi za nyerere lakini ameshindwa kujiajiri. Anza wewe kuonyesha mfano
 
Mtu unajiajiri bla mtaji?
Sasa ukikaa nyumbani mtaji utaupata,chakarika tafuta pesa au ndio mpaka mpate post serikali mnasubiria ,tafuta mishe jiweke huku unasubiria post ..

Ttz wabongo hawana long plan
 
Kujiajiri ni jambo jema sana ila mitaji ndo shida mm nadhani serikali iangalie namna ya kubadili policy turusiwe kukopa kupitia vyeti vyetu vya elimu.
 
Ni kweli upo sawa kwa kiasi fulani lakini fikiria haya:
1. Graduates wengi wamepewa elimu inayowafanya matarajio yao makubwa kwenye kuajiriwa kuliko kujiajiri.

2. Kazi unazotaja ambazo ni fursa, tayari zina watu. Kwa mfano kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara na nyinginezo.
Inakuwa ni vigumu baba yako kakusomesha kwa jembe la mkono baada ya ku graduate unarudi kung'angania jembe na baba yako.

3. Taasisi za fedha hazikopeshi wanaoanza biashara na kama hawana mitaji ndo basi.

4. Urasimu katika uanzishwaji na usajili wa biashara mpya.

5. Bidhaa nyingi zinazotumiwa kuzalishwa nje ya nchi jambo ambalo linatengeneza fursa chache za ajira.

6.Matumizi mabaya ya rasilimali za nchi ambazo zinasababisha wachache kufaidika.

7. Hali za kiuchumi zisizotabirika. Hapa utaona kuna wengine walijiajiri vizuri tu, ila kutokana na hali ya uchumi hata wao wamekuwa tegemezi kwa walioajiriwa.

8. Siyo kila mmoja anaweza kujiajiri. Hii ikitokea hakutakuwa na mwajiriwa na hivo litazuka tatizo lingine.
umeongea ukweli sana lakini tambua nchi nyingi zinazoendelea lazima iwe na wazalisha ajira wengi kuliko wategemea ajira
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri. Mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu.

Vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo.
Umeona hao mizigo ila mkuu wa mkoa mwenye phd na akatubu kwa Kujikomba kwa raisi hujamuona.

Profesa anayeng'ang'ana na madaraka hujamuona kama mzigo.

Serikali inayoshindwa kupanga, kutekeleza na kusimamia sera zake za ajira na za vijana ambazo zingewezesha kujiajiri huioni kama mzigo.

Kweli kabisa mizigo ya nchi hii umeona wahitimu tu?
 
Nashangaa sana kijana graduate una degree au diploma unashindwa kujiajiri wakati Tanzania fursa zipo nyingi sana za kujiajiri mashamba vijijini yamejaa hayana walimaji , biashara za kufanya zipo kila kona kuna watu wanaishi kwa kuuza maji tu vijana amkeni acheni kuzurura na vibahasha kutafuta kazi ambazo hazipo
Umejiajiri kwenye sekta gani?
 
Back
Top Bottom