Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Alikua anawala kimasihara tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisaidie mawasiliano yake boss
wote wanatumia nguvu za giza mkuu kuna waziri mmoja rafiki yangu nilikuta kwake kawafungia waganga kama 30 hivi anawalisha kila kitu wamtengeneze mambo yake yawe mazuri na kweli amefanikiwa jiwe anamsikiliza hatari japokua jamaa ni bogus tu
 
Nakumbuka miaka flani maeneo ya Pale kunduchi mtongani kuliku na mzee flani anaitwa x alikuwa anafuga mbuzi basi siku moja mbuzi wake alipotea maeneo ya benaco kule akaanza kulia kwa kuliita jina la yule mzee x mpk wananchi wanampeleka kwa yule mzee
Hapo Kunduchi kuna ng'ombe zipo zinajifuga zenyewe na kuna siku nimetoka zangu kwenye mishe zangu saa nane kasoro ivi napishana na ng'ombe inaenda home aisee. Na hizo ng'ombe mtu hazigusi maana zinahusishwa na kusomewa albadiri kwa sababu inasemekana ziliibiwa kumbe zilipotea zenyewe kwa hiyo atakayezichukua cha moto kitampata.
 
hao mbuzi wanaojichunga huwa wabaya sana, usiwaguse, mbuzi anafunguliwa kwenye banda tu anajua mwenyewe pa kwenda, mbuzi kabla hajavuka barabara kwanza anageuka kulia na kushoto, ukiwaona waache!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilishangaa pale mtakuja hizo ng'ombe zinavuka kwenye zebra na zenyewe zinaangalia kulia na kushoto kama kuna gari au hamna.
 
Haahah,kuna kisa cha mpemba Mafia, alikua ameanika samaki wake baada ya kuwavua, ikafika mda akatoa mkeka akawa anapiga rakaa(Anaswali).Amemaliza kuswali kugeuka hamadi samaki wake wawili hawapo, akauliza kuna ntuu kachukua samaki zangu arudishee kila mtu akakakana akasema mi natoa dakika kumi tuu msiporudisha Walah! atakufa mtuu hapa na si masiharaa... Ebanaeee baaada ya dakika 10 zikaanguka kunguru mbili(hawa ndege Weusi) zimeshakaukaa zamani mdomoni wanamabaki ya samaki....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha Kama ni kweli Sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilitokea miaka ya 2000 mwanzoni. Tulikuwa tunaishi karibu na shamba la miti ya kupandwa...sasa kuna kichochoro fulani hukatiza katikati ya shamba hilo. Tukiwa nje mida ya saa mbili kasoro nikisikiliza habari za michezo kutoka RTD tulishuhudia kama kijinga cha moto kikipita katika kile kijia...mwanzo tulijua mtu..ila kwa kasi ya ajabu kikakwea mtini huku kikitoa cheche. Sikumbuki kilichoendelea maana breki ya kwanza ilikuwa uvunguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu utakua umechanganya majina ya kituo kdg sbb majina km yanaendana..
Kituo kitakua ni mkuzi.

Nimeishi kule kiasi maana mzee alikua meneja misitu pale magamba forest(hope unapajua ni katikati ya msitu, kambi ipo isolated na wanakijiji, japo huduma zote zipo) kabla hajahamishwa..

Lukozi ni Juu ya Magamba km unaenda Mtae huko na kifungiro n km unaenda mlola..
kwahio, unatoka kifungiro unaingia mkuzi, unakuja magamba coast, unaingia trade unakuja magamba sec(secomu) ndio unaelekea huko lukozi...

Na huko kuelekea Lukozi ndio kuna msitu unaitwa 'kandele ka paa' huko ndio kuna mapicha sio ya nchi hii, waulize waendesha magarii...

Na ukitokea huko mkuzi...
kimbembe kipo pale kati ya msitu kwenye daraja flan kubwa, maji yanayopita ni mengi ila yanashuka taratbu, kila upande ni giza kubwa si barabarani sio msituni maana maeneo hayo ndio msitu umefura kisawa sawa na miti ni mikubwa mirefuuu kwaio hata mwanga wa jua haupenyi...

Kwaio pana sifa ya Ukimya, giza kubwa, msitu mnene, Daraja kubwa lenye maji mengi,
You can imagine....

pale Hata walevi wakipita wanaacha kelele kwanza.. ndio utajua Pombe inaogopa nayo..
Maji yenyewe hayapigi kelele wala ndege wa polini wewe upge kelele ni nani?....
Pametokea matukio mengi sanaaa.....

Yote kwa yotee yale maeneo yana mapicha picha sanaaaa...
Huko huko mkuzi kuna mzungu mmoja maarufu sana naamini hata wewe unamfahamu, alikua anaitwa mzuka,

Kisa cha kupewa hili jina ni kwamba alikua na shamba akaambiwa popote utakapoona huu mti usiukate ni makazi ya majini/shetani..
Akapuuza siku akaukata...
Alikula bonge ya banzi, kuanzia pale akawa amepinda shingo, kichwa kimelalia upande mmoja...

Maisha yake yote yaliobaki alikua akitembea na kikapu kilichojaa mawe upande mmoja ili ku balance mwili maana ulikua umelala upande mmoja...

Pia tushawahi pita sehemu usiku miti ikalala yoteee.....
Pia mzee alishawahi salimiwa na vibwengo usiku akitoka magamba coast akipita ule uchocholo wa magamba sec...
Akavitukana sana huku anachomoka kasi ya ajabuu..
alifika nyumbn hana kiatu kimoja.....

Kuna mapicha mengi sanaa kulee....
Yale maeneo yote yalikua makazi ya wajerumanii,
nyumba nyingi km ya mkapa, ngwirizi na majumba mengi sana yamejaa...

Hata sisi kambi yetu ilijengwa na mjerumanii,
Majumba yao yamedizainiwa kiajabu sanaa....
Tumeish kwenye nyumba miaka na miakaaa,
eti tunakaribia kuhama ndio tunajua tunaishi juu..
kumbe chini kuna nyumb nyingne yenye mavyumba na hapo barazani chini kumbe ni bonge ya kisima..

Ilikua ukizunguka msituni kukuta sehemu imesakafiwa au makorokocho korokocho mengi ni kitu cha kawaidaaa..

Nimepamisss long time sanaaaa..
 
 
Hawa watu ni shida wewe,kuna kicheche moja ilitusumbua kwenye familia tangu ina miaka 16 yaani ilifika mahali tulikuwa tunaombea afe tu ili tupumzike ikakumbana na mpemba ikaolewa yaani kama haipo ilivyotulia hata kukiwa na tatizo haiji mpaka mumewe aizingue nje kwenyewe nasikia haichungulii
 
Dah ndio na Mimi nagundua sasa hivi, sijui kwanini muda sana nashindwa kutofautisha Mkuzi na Lukozi! Mzuka alishafariki miaka mingi akamuacha yule Mama, alikua na Mabinti wawili sijui wako wapi siku hizi. Walifungua hotel yao jirani na Makazi ya Mzee Mkapa! Nasikia Mzee ....... Usiku mwema
 
Kuthibitisha unakokutaka unataka kukidhi vigezo gani?

Maana naweza kuthibitisha usikubali uthibitisho wangu kwa vigezo vyako.

Nipe vigezo vyako unavyotaka nivitumie kuthibitisha, ili nijue uthibitisho wangu unakidhi vigezo.
Hata humu watu wanathibitisha kuwa uchawi upo ingawa wewe unapinga kwa vigezo vyako.

Kuthibitisha (uchawi) unakokutaka unataka kukidhi vigezo gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hii niliisikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…