Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

WANAODHANI HAKUNA UCHAWI , HAYAJAWAKUTA;
Miaka michache iliyopita nilikwenda RUKWA wilaya ya Nkasi nikiongozana na wenzangu tukiwa na watu Dr Livingstone Expedition waliokuwa wanafuatikia njia aliyotumia Dr Livingston toka Ujiji Kigoma hadi Zambia alipopata umauti.

Tulupofika kijiji kimoja kinaitwa Ntuchi (Nakikumbuka kwa tukio hili) tulikutana na kisa cha kustaajabisha kilichowakuta Maafisa toka Wizara ya Elimu Dsm waliokwenda kukagua shule za Sekondari Nyanda za juu na walipofika kwenye shule hiyo wakakutana na malalamiko ya Walimu juu ya vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa na wenyeji.

Maafisa wale wakawaita viongozi wa kijiji na wazee maarufu kuwakemea sana huku wakitishia kuwaondoa walimu wote endapo vitendo hivyo vitajirudia. Baada ya kumaliza kukemea jambo hilo wakiwa ofisini, walipotoka nje wakakuta gari lao halina upepo kwenye tairi zote 4, wakabaki wanashangaa. Walimuuliza dereva kimetokea nini naye akabaki anashangaa maana hajaona mtu yeyote akitoa upepo.

Walimwita fundi aangalie lakini kila alipojaribu kujaza upepo haukuingia. Walilazimika kuita baadhi ya wazee wakawaomba radhi na ghafla tairi zikawa na upepo kama awali. Waliapa kutorudi mkoa ule na sisi tukaendelea na safari yetu huku tukiwa na hofu kubwa.

Maafisa wale kama wamo humu JF watashuhudia tukio hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenkumbusha mbali nilitaka niaxe kazi ya ukaguz mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasukari bado hakajakoza mkuu kwa xai
Kuna rafiki etu mmoja walikuwa na party koko beach,sasa yeye ni mnywaji wa pombe zote.sasa akiwa coco beach akaja muhudumu àkamletea soda,jamaa akamfokea wewe mimi nimeagiza kitu fulañi na sio soda.yule mwanamke ambaye ni muhudumu àkàmsogelea na kumfungulia huku akimwàmbia utàkunywa soda.
Muda huo ni yeye ndie anayemuona muhudumu wale wenźie hawamuoni.
Baada ya muda ndugu zake wanamuona kaka yao àkiogelea kweñda kati kati ya bahari,sasa wao wanamshangaa si ameagiza kinywàji na kuogelea hajui anaogeleaje kufika kule (maji mengi) .Wakainuka na kuañz kumkimbilia huku wakimwita jina lake jamaa hakugeuka wakamwita sana hakugeuka mara àka wapotea baharini.
POLISI na familia źikamtafuta kando wa mbambao siku tatu jàmaaa hakuonekana hai wala màiti.siku ya tatu usiku ndio jamaa kaja mwenyewe anajokokota hajiwezi na kufika nchi kavu akadondoka.wàtu kumuokota muhimbili.
Alipopona ndio akatusimulia kuwà baada ya kukataa soda yule mwanamke alikasirika sana na akamchukua na kwenda nae baharini çhini kabisa kuna mwamba ambao walikuwa wàkibishana muda wote .yule mwanamke alikuwa anamwambia kuwa anampenda na jamaa alikuwa na msimamo wa kumkataa na alivutwa kutaka kuelekea chini ya mwamba zaidi ndio jamaa alijizatiti ende zaidi na wamepambana muda wote mwishowe yule mwanamke àka mwambia una bahati mizimu ta kwenu ina nguvu na imekulinda.
akaçhwa ,jamàa akawa ana hangaika kupanda ule mwamba wa mawe maana alikuwa ànaona njia ya kutoka shida ni kupanda amehangaika kupanda juu wabmwamba wa jiwe mpaka akatoka.ndio kutoka amepoteza fahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichogundua humu
Kuna watu fuata upepo, anaangalia fulani kasemaje na yeye aseme

Pili wengine bado ni watoto hawajakutana na masahibu

Tatu, kuna wengine wamekalilishwa neno CHAI,
basi kila coment wao utasikia ... Hio ni chai...

Wengine akili ya sisimizi wanahoji mtoa post eti inakuwaje kipindi hicho alikuwa anafundisha halafu miaka kadhaa mbele yuko field bila kujua Elimu haina mwisho.

Hawa nao wanajifanya kuhoji ili nawao waonekane wamo kumbe hawamo

Na mwisho, jamani uchawi upo na mimi nimeshuudia wachawi livi nikiwa mimi, dada yangu na kaka yangu (R.I.P) mida kama saa 5 usiku tukiwa tunamsindikiza dada kwenye uwanja wa mpira na visa vingine ninavyo kama hivi
Hueleweki pumba tupu weka story axa poyoyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikua zamani wakati wachaga bado walikua wanashika dini. Wale wa Magomeni mwembe chai unewaona siku hizi?
Hivi wachaga washawahi kushika dini maana kule kwao wanapiga mazongo mpaka nyama na hio ni miaka zaidi ya 25 nyuma
 
Wakuu, mimi huwa nawashangaa sana watu wanaokana uwepo wa nguvu za giza (uchawi na ushirikina). Nadhani ni kwavile hawajawahi kukumbana na ushirikina. Na Mshana Jr huwa anapata wakati mgumu sana kuwaelewesha watu kuhusu mambo hayo.

Si ajabu hata comments tuzopandisha kwenye uzi huu wengine watafikiri ni story za kunogeshea baraza, la hasha! Mimi nina visa kadhaa nilivyoshuhudia:

1.Wakati nikiishi mkoani Mwanza, alikokuwa anafanyia kazi Mzee wangu, na nikiwa na miaka 11 tu, kuna siku wazazi wangu wakiwa wamelala huku wamefunga milango na madirisha yote, walikuja kugutuka kutoka usingizini mishale ya saa 9 usiku na kukuta madirisha yote ya chumbani kwao na mlango yamefunguliwa. Na kwavile kulikuwa na mbalamwezi, waliweza kuwaona bundi 4 wamesimama katika madirisha 2 ya chumbani huku wakiwatazama wazazi wangu waliolala kitandani. Baba alivaa ujasiri wa kuwatimua, ila baada ya kuamka watu 4 ndani ya familia tuliamka tukiwa tumechanjwa chale mwili mzima. Ilibidi familia iingie 'gereji' ndo mambo yakawa shwari.

2.Mwaka 1993 tukiwa tulipanga nyumba moja kule Tandika Mabatini, Dar es Salaam. Mwenye nyumba alitupa masharti kadhaa, kubwa kabisa likiwa ni katazo la kuingia nyumbani baada ya saa 6 usiku, au kwenda chooni/bafuni baada ya masaa hayo. Tulijitahidi kutii! Siku moja, mpangaji mwenzetu mmoja alikiuka masharti akaenda msalani saa 6 na ushee, tulisikia kelele za kuomba msaada, lakini hakuna aliyethubutu kwenda kutoa msaada. Kesho yake alfajiri tulimkuta jamaa bado ameanguka chooni. Mwenye nyumba alimfokea kwa 'kuyataka mwenyewe'. Ilibidi jamaa ahame nyumba baada ya siku 4. Ilikuja kubainika kuwa, Mwenye nyumba alikuwa anafuga majini na huwa anayafungulia masaa hayo yanaingia kazini, hivyo jamaa alikumbana nayo yakamshughulikia. Sisi nasi kwa uoga ilibidi tuhame kabla kodi yetu haijaisha.

3.Muda haunitoshi kusimulia nilivyokutana na wachawi ' live' mara mbili, wakati nikiishi huko Kanda ya Ziwa.
Umenikumbusha nyumba moja hivi Tegeta mwaka flani hivi masharti ya mwenye nyumba yalikuwa kama hayo halafu yule mzee alikuwa amepangisha nyumba nzima halafu yeye anaishi chumba kimoja cha uwani karibu na choo tena chumba chake hakuna umeme.
Ikifika kuanzia saa 5 usiku huruhusiwi kwenda bafuni wala chooni na ikitokea ukapishana naye mwenye nyumba muda huo usimsalimie!
Halafu yule mzee hakuwa na mke wala mtoto wala hakuna aliyewahi kuingia ndani kwake na aliishi maisha duni sana sijui pesa za kodi alikuwa anapeleka wapi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mtakimbuka ile mvua ya mawe kahama march 2015 ngoja niwape kisa chake.

Mvua zilikuwa adimu sana basi wananzengo wakamfuata mganga mmoja alokuwa ana tuhma za kuzuia mvua
Basi watu wakamuhoji akakataa tuhuma hizo. Jamaa hawajaelewa wakampiga hadi kumuua.
Wakati anakufa alisema nakuta lkn mtaona.
Waloelewa walianza kuhama walokaza shingo wakakomaa .....
Mvua ilipoanza wakasema tumemuua yule alikuwa anazuia mvua....lkn ikaja kuzidi....na mawe juu. Iliua watu na mifugo na uharibifu mkubwa ulotokea.

Kiranga usi comment hapa
Basi kama ni hivyo issue hii ina theories nyingi.Inasemekana kuwa baada ya H/ W mpya ya Msalala kuundwa ulitokea mvutano mkali wa wapi pawe makao makuu kati ya Ntobo na Segese nadhani, ni katika pilika hizo kamati za ufundi zilihusishwa, inasemekana vijiji vyote viwili vilikuwa na kamati za ufundi, kijiji kimojawapo kilipotupiwa hilo kombora katika jitihada za kukwepa ndio yakatokea hayo maafa, lengo lilikuwa ku-puch kombora na kulituma Ziwa Victoria hili lipotelee ziwani, kutokana na umbali likawakumba watu wa Mwakata.
 
Jirani yangu kuna siku alikuwa ananisimulia alikuwa anasafiri na broo wake usiku walikuwa kwenye gari yao. Safari ilivyokuwa inachanganya mbele wakamuona mtu kwa mbali kama anasimamisha gari. Kumuangalia vizuri kumbe ni mwanamke, halafu ni mrembo tu! Dogo akamwambia bro huyu mwanamke atakuwa jini tu haiwezekani usiku huu wote asimame njiani peke yake, tumpite tu.

Brother yake akamwambia usihofu. Akasimamisha gari. Akamwambie ndio mrembo! Yule mwanamke akamwambia naombeni lift nimekwama huu usiku naelekea eneo fulani. Brother yake akamwambia yule mwanamke ingia. Safari inachanja mbuga brother yake akaanza kumwambia yule mwanamke. Inakuaje unatusumbua unasimamisha gari wakati eneo unalotaka kwenda unaouwezo wa kufika?

Yule mwanamke akajibu sielewi unachozungumza. Brother yake akamwambia yule mwanamke, usi' panic! Sisi tuliokupa lift tunajua kwamba wewe ni jini! Ndiyo tunakuuliza kwa nini umetusumbua kusimamisha gari wakati kufika eneo unalotaka uwezo huo unao wewe kama wewe?

Yule mwanamke akawaambia simamisheni gari! Majamaa wakasimamisha. Wakasikia mlango wa siti ya nyuma unafunguliwa. Kugeuka yule mwanamke hawamuoni tena! Brother yake akasema, unatusumbua wakati uwezo wa kufika unao. Wakaendelea na safari.

Nikamuuliza sa mbona huyo jini katumia style ya zamani sana? Jamaa akanijibu, majini ni wapumbavu wapumbavu tu.
jini kapatikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nataka siku moja nipige tungi niwashe na kitu Cha R alafu saa sita usiku niende pale katikati ya makaburi ya kaloleni nikae kwa kutulia
Nione nitaona Nini Manake hizi stories nazisikiag tu oh Mara majitu,mashetani,vibwengu blah blah nyingi nataka nione live alafu nikikutana nalo niliulize kwanini wanatisha na kuua watu
uende ukiwa kawaida mkuu bila kua na sapoti ya kilevi chochote ili uone live kama vipo au ni maneno tu usisahau mrejesho .
 
Back
Top Bottom