mnadhimu mkuu wa jf
JF-Expert Member
- Mar 19, 2017
- 759
- 287
Hadithia basi mkuuHahahaha aisee umenifanya nikumbuke nilivyotapeliwa kwa hii style
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Stori ndefu kidogo nitaifupisha kidogo... Nilikua kwenye harakati zangu mjini nikakutana na jamaa akadai ametoka machimboni ameelekezwa na mtu aje dar atapata wateja haswa Wenye vituo vya mafuta, nikamuelekeza kituo kilichopo karibu tukaagana nikaendelea na mishe mishe zangu ghafla akatokea jamaa mwingine akanisimamisha akaniuliza kistaarabu tu yule jamaa ametaka nini? Sikutaka kumjibu ila akaniwahi kusema kwamba jamaa ana mzigo wa dhahabu (kuna jina alinitajia limenitoka) akinipigia mahesabu naona hela kibao zinakuja ngoja nikomae na Mimi niondokane na umasikini tukakubaliana tunapiga cha juu halafu jamaa tunampa robo ya mauzo kwa vile alidai ameuza ana matatizo akipata hata 3M itamtosha kutatua shida zake. Yule jamaa wa Pili akampigia simu mwenzao akaja na gari tukasepa kuelekea kwa bosi njiani jamaa akasimamisha gari akaniomba nitoke tuongee kwenye maongezi na yeye anaongeza cha juu zaidi tukakubaliana tukarudi kwenye gari safari ikaendelea.. Walikuja kuniacha sinza madukani niwasubiri hapo washanipiga hela na ka smartphone kangu....
hakuna mazingaumbwe mkuu, hao jamaa wapo mbele ya duka langu la sim, kuna watu wanashindwa bei wanatapeliwa na hao jamaa nikishuhudia huku nacheka, afu hurudi dukan kwangu kuuliza aliye mtapeli,Nimekaa nao sana hao wezi lakn sijawahi kuelewa ni mechanism gan ambayo huwa wanatumia ila nahsi kuna mazingaombwe hapo
Hao jamaaa nawakubari sana wanavyoiba
Huwa nikiwaona wanamuibia mtu nawapa hela ya soda ata buku 5
Je ww unajua wanavyozi change bahasha kama sio mazingaombe n nn ?hakuna mazingaumbwe mkuu, hao jamaa wapo mbele ya duka langu la sim, kuna watu wanashindwa bei wanatapeliwa na hao jamaa nikishuhudia huku nacheka, afu hurudi dukan kwangu kuuliza aliye mtapeli,
Nawajibu jibu moja tu, RAHISI NI GHALI.
Sent From Ikulu-Magogoni street
hakuna mazingaombwe mkuu!!Je ww unajua wanavyozi change bahasha kama sio mazingaombe n nn ?
Uko poaMimi sikuingizwa mkenge,lakini tulinusurika. Nakumbuka mtaa wa Congo k.koo pale,Mimi na cousin wangu tulikuwa tunatafuta simu,cousin wangu ndie aliekuwa muhitaji. Tukafika sehemu akamkuta teja anauza simu,kumuulizia akasema elfu 40,mi nikaikagua nikaikuta nzima na ni nzuri tu. Nikaishikilia Mimi, nikamwambia cousin mpe ela,akakataa akasema simu yenyewe nzuri nirudishieni mkitaka ongezeni ela,tukamuliza sh ngapi akasema apewe 60 nikaikomalia simu cousin akamuongeza ela,akaona hapa wananiweza akakataa tukachukua ela yetu tukampa simu yake tukasepa.
Yeah yeah
Inamaana wewe sio mtanzania? Wenzako tumetapeliwa na watu waliovunja mkataba kisha inatugharimu 89B.Mii sijawahi kutapeliwa ngoja nipite kimya kimya
Haahahahahahaaaaaa.Ilinitokea hyo aiseee,aliniambia sim 25000 nikamwambia nna 10000 hapa,nikawa namsoma asibadilishe bana,akanipa ile naondoka akaniambia "GANZI KWA BARAFU JOMBA" kitu ambacho hadi leo sielewi maana yake na kwa nn aliniambia,nimefika mbele kuangalia nakuta sabuni imechongwa mfano wa sim aiseee nikajisemea jamaa mchawi nini.
Katika pita pita zangu nikakutana na yule jamaa bna,nikamshtua bana huku nacheka nikamkumbusha akasema jamaa angu kausha ni maisha tu.
Philips X2560
Mie hii ya dhahabu kidogo inipate pale Chalinze nilitoka Tanga nikashuka hapo ili nisubiri usafiri wa kwenda Moro nikakaa kwenye bench Mara akanijia Dada mmoja mrembo Tena kajifunika ushungi akanionyesha hivyo vipande viko kwenye kitube kimebandikwa karatasi imeandikwa dhahabu ina thamani ya shs mil kadhaa , kwamba hicho kichupa amekiokota baada ya kutokea ajali ambapo na yeye alikuwemo akaokota hicho kichupa hajui kusoma nimsomee nikamsomea,Akajifanya kushangaa akawa ananiomba nimsaidie kutafuta mteja au kama naweza kujichanga tuelewana nikamwambia Sina uwezo huo,bahati nzuri nikashikwa na haja wakati naulizia mahali pa kujisetiri Dada mmoja akanifuata akaniambia a Chana nae huyo tapeli.Nilivyorudi nikasema ngoja nione mwisho wake nikamfuata pale kwenye benchi tukawa tunaendelea kuongea Sasa kilichonishutua upande wa pili alikuwepo amekaa bwana mmoja kava bonge la miwani myeusi anatuangalia nikamwambia yule Dada hebu tuinuke twende pembeni kidogo Ile tunatembea nageuka nyuma namuona yule jamaa anatufata taratibu nikajikausha kwanza baada ya hatua chache nikageuka tena namuona jamaa bado yupo nikamuuliza mbona yule jamaa anatufata? Bi dada asinigeuke kwamba mimi ndo namjua huyo jamaa tunataka kumwibia nilikaza nikamwambia twende kituoni polisi kama una wasi wasi na mimi weee aliondoka bila kuaga na yule jamaa alivyoona tunabishana alishakula kona siku nyingi.
Nilipewa buku na baba nikanunue Shati la shule. Nikafika mitumbani nikakuta wale jamaa wa Karata tatu.. Weka hapa unapata, hapa unakosa.
Nikaangaliaaa, nikaona kabisa kete ile pale.
Nikaweka ile buku.
Jamaa wakaanza kunipampu "Dogo ongeza hela ule zaidi"
Nikawaambia sina nyingine. Funua hapo nilipoweka hela yangu.
Kufunua chaliiiii.... Kete ikahamia mwanzo.
Daaah.. Nakumbuka niliporudi nyumbani baba alinichapa sana.

Nilipigwa buku9 masika kwa wauza madude used.yale, redio na tv za kizamani.Nshaga tapeliwa moro masika pale! Aiseee acha tu yan ukija stuka ni too late.
Hio style alipiwa dadaangu akaachwa ubungo plaza pale analia maana simu aliopigwa ilikuwa ya rafiki yake!Ni Stori ndefu kidogo nitaifupisha kidogo... Nilikua kwenye harakati zangu mjini nikakutana na jamaa akadai ametoka machimboni ameelekezwa na mtu aje dar atapata wateja haswa Wenye vituo vya mafuta, nikamuelekeza kituo kilichopo karibu tukaagana nikaendelea na mishe mishe zangu ghafla akatokea jamaa mwingine akanisimamisha akaniuliza kistaarabu tu yule jamaa ametaka nini? Sikutaka kumjibu ila akaniwahi kusema kwamba jamaa ana mzigo wa dhahabu (kuna jina alinitajia limenitoka) akinipigia mahesabu naona hela kibao zinakuja ngoja nikomae na Mimi niondokane na umasikini tukakubaliana tunapiga cha juu halafu jamaa tunampa robo ya mauzo kwa vile alidai ameuza ana matatizo akipata hata 3M itamtosha kutatua shida zake. Yule jamaa wa Pili akampigia simu mwenzao akaja na gari tukasepa kuelekea kwa bosi njiani jamaa akasimamisha gari akaniomba nitoke tuongee kwenye maongezi na yeye anaongeza cha juu zaidi tukakubaliana tukarudi kwenye gari safari ikaendelea.. Walikuja kuniacha sinza madukani niwasubiri hapo washanipiga hela na ka smartphone kangu....
Tangu hii Siku nikaweka kichwani hakuna hela inapatikana kirahisi tu lazima uvuje jasho aisee
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahahahah