Kama uliwahi tapeliwa njoo hapa

Kama uliwahi tapeliwa njoo hapa

mi nilitapeliwa nikiwa form 6 kwa kupewa burungutu uchwara la fedha nikiambulia elfu mbil tu toka humo na kuwaachia cm yng nokia pamoja na kad yng ya ATM nilikuwa wamekomba fedha zooote hii ilikuwa maeneo ya ubungo bus terminal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli kutapeliwa hakujawahi kwepeka hata uwe mjanja uliezaliwa katikati ya mji,utatapeliwa tu aidha kwamakusudi au bahati mbaya
Mimi Miaka ya nyuma, ubungo walishawahi niotea nikiwa na makusudi ya kutaka kuona ni jinsi gani wale vijana wanambinu kali za kugeuza simu kwenda sabuni(mfukoni)
Basi nikameet na janja mmoja akiwa na smartphone nzuri tu na ipo ON bt haina line. Akaniambia 50 me nikasema nina 20, akasema poa toa..nikampa fasta huku nikimkazia macho mfukoni asibadili gia...basi akaitoa mfuko uleule kama ilivyokua kwenye kibahasha..basi nikajua leo nimewaweza.alivyogeuka nikatoka mbio mpaka RIVERSIDE ili niikague...Loooh aisee nikakutana na sabuni aina ya KOMOA..doh
Aisee teknolojia ya wale viumbe niyahali ya juu.
Hebu tupe uzoefu wako katika kuingizwa Mitini

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli haukutapeliwa kisomi, bali ulitapeliwa kizembe kwa kumheshimu tapeli na kujifanya haujali.
Kitugani kilikufanya ukimbilie Riverside kukagua badala ya kuikagua mbele yake na kumuaibisha?
Kisa chako cha kizembezembe kinafanana na cha kwangu.
Nilitamani dawa ya meno aina ya whitedent pale Msimbazi kwa vender wa mkokoteni.
Nilipouliza bei nikatajiwa bei chini na ya dukani. Nilipoikagua nikagundua haijaambatishwa na miswaki kama ilivyo ada.
Nikahoji kwa nini, nikaelezwa miswaki ndiyo faida.
Nikasema kama nihivyo ninaghairi.
Yule jamaa akanieleza nisijali, akakokotoa miswaki miwili akaiweka ndani ya box la dawa, nikatia kwenye begi nikaondoka.
Nilipofika nyumbani nikakutana na dawa ileile isiyokuwa na miswaki, nikashangaa na kukasirika.
Nikaamua kurudi eneo lile ili nimdhalilishe, kiukweli nilizunguka sana na kwa kasi eneo lote lile la Kariakoo na viunga vyake, sikufanikiwa kumbamba.
Nilipotulia na kuanza kutafakari aina ya acrobatic aliyotumia, baadaye nilikuja kugundua alinilevya na adabu zake za bandia.
Aliniheshimu kwa kiwango cha kustaajabisha hadi nikalegeza umakini.
Hili neno "kiongozi","mkurugenzi", sijui "baba" yakipata mtamkaji mzuri waweza kutapeliwa kwa kuridhika.
Ni kwanini sikuhakiki alivyonikabidhi box kabla ya kuliweka kwenye begi?
Ni kwa sababu ya ulevi wa heshima ya kupigwa adabu za laghai kwa maneno niliyoyataja hapo juu. Maneno matupu yasiyokuwa na ukweli wa sifa husika za mteja.
 
Nimekaa nao sana hao wezi lakn sijawahi kuelewa ni mechanism gan ambayo huwa wanatumia ila nahsi kuna mazingaombwe hapo
Hao jamaaa nawakubari sana wanavyoiba
Huwa nikiwaona wanamuibia mtu nawapa hela ya soda ata buku 5
"Fadhili Madhambi" nawe ni mwizi pia.
 
Kiukweli haukutapeliwa kisomi, bali ulitapeliwa kizembe kwa kumheshimu tapeli na kujifanya haujali.
Kitugani kilikufanya ukimbilie Riverside kukagua badala ya kuikagua mbele yake na kumuaibisha?
Kisa chako cha kizembezembe kinafanana na cha kwangu.
Nilitamani dawa ya meno aina ya whitedent pale Msimbazi kwa vender wa mkokoteni.
Nilipouliza bei nikatajiwa bei chini na ya dukani. Nilipoikagua nikagundua haijaambatishwa na miswaki kama ilivyo ada.
Nikahoji kwa nini, nikaelezwa miswaki ndiyo faida.
Nikasema kama nihivyo ninaghairi.
Yule jamaa akanieleza nisijali, akakokotoa miswaki miwili akaiweka ndani ya box la dawa, nikatia kwenye begi nikaondoka.
Nilipofika nyumbani nikakutana na dawa ileile isiyokuwa na miswaki, nikashangaa na kukasirika.
Nikaamua kurudi eneo lile ili nimdhalilishe, kiukweli nilizunguka sana na kwa kasi eneo lote lile la Kariakoo na viunga vyake, sikufanikiwa kumbamba.
Nilipotulia na kuanza kutafakari aina ya acrobatic aliyotumia, baadaye nilikuja kugundua alinilevya na adabu zake za bandia.
Aliniheshimu kwa kiwango cha kustaajabisha hadi nikalegeza umakini.
Hili neno "kiongozi","mkurugenzi", sijui "baba" yakipata mtamkaji mzuri waweza kutapeliwa kwa kuridhika.
Ni kwanini sikuhakiki alivyonikabidhi box kabla ya kuliweka kwenye begi?
Ni kwa sababu ya ulevi wa heshima ya kupigwa adabu za laghai kwa maneno niliyoyataja hapo juu. Maneno matupu yasiyokuwa na ukweli wa sifa husika za mteja.
Sawa mkuu nakubali uzembe huu ndio source yakutamka neno UTAPELI LEO HII

ila nawe mzembe usiekua na calculations... hiyo pesa ya kwenda na kurudi tena kariakoo si ungenunua mswaki kwa Mangi hapo...duh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom