Kama uliwahi tapeliwa njoo hapa

Kama uliwahi tapeliwa njoo hapa

Hakuna mazingaombwe..iko hivi,wakati mnakubaliana kukuuzia hicho kitu kunakua na mwenzake pembeni anasikilizia na ndio huyu mwenye kanyanga...sasa wakati wewe unatoa pesa..anaweza hata kukuzuga wakati huo anapokea Kwa yule nwenzake kile kitu fake..na Mara nyingi bidhaa inakua kwake mpaka mkubaliane.
 
We haujawahi kutana na teja anakupa simu nzuri bei ya kutupa na unaichukua...?hujawahi?
Nakutana nao mara nyingi tu kkoo msimbazi ila nikiwa mwenyewe sihangaikagi nao nikiwa na na kampan at least wawili huwa tunawanyang'anya
 
Nilipewa buku na baba nikanunue Shati la shule. Nikafika mitumbani nikakuta wale jamaa wa Karata tatu.. Weka hapa unapata, hapa unakosa.
Nikaangaliaaa, nikaona kabisa kete ile pale.
Nikaweka ile buku.
Jamaa wakaanza kunipampu "Dogo ongeza hela ule zaidi"
Nikawaambia sina nyingine. Funua hapo nilipoweka hela yangu.
Kufunua chaliiiii.... Kete ikahamia mwanzo.
Daaah.. Nakumbuka niliporudi nyumbani baba alinichapa sana.
 
Kiukweli kutapeliwa hakujawahi kwepeka hata uwe mjanja uliezaliwa katikati ya mji,utatapeliwa tu aidha kwamakusudi au bahati mbaya
Mimi Miaka ya nyuma, ubungo walishawahi niotea nikiwa na makusudi ya kutaka kuona ni jinsi gani wale vijana wanambinu kali za kugeuza simu kwenda sabuni(mfukoni)
Basi nikameet na janja mmoja akiwa na smartphone nzuri tu na ipo ON bt haina line. Akaniambia 50 me nikasema nina 20, akasema poa toa..nikampa fasta huku nikimkazia macho mfukoni asibadili gia...basi akaitoa mfuko uleule kama ilivyokua kwenye kibahasha..basi nikajua leo nimewaweza.alivyogeuka nikatoka mbio mpaka RIVERSIDE ili niikague...Loooh aisee nikakutana na sabuni aina ya KOMOA..doh
Aisee teknolojia ya wale viumbe niyahali ya juu.
Hebu tupe uzoefu wako katika kuingizwa Mitini

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh utapeli huo ulotapeliwa mbona wakijinga sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sikuingizwa mkenge,lakini tulinusurika. Nakumbuka mtaa wa Congo k.koo pale,Mimi na cousin wangu tulikuwa tunatafuta simu,cousin wangu ndie aliekuwa muhitaji. Tukafika sehemu akamkuta teja anauza simu,kumuulizia akasema elfu 40,mi nikaikagua nikaikuta nzima na ni nzuri tu. Nikaishikilia Mimi, nikamwambia cousin mpe ela,akakataa akasema simu yenyewe nzuri nirudishieni mkitaka ongezeni ela,tukamuliza sh ngapi akasema apewe 60 nikaikomalia simu cousin akamuongeza ela,akaona hapa wananiweza akakataa tukachukua ela yetu tukampa simu yake tukasepa.
Ww mjanja sana so hawa walofungiwa kwenye bahasha .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mazingaombwe..iko hivi,wakati mnakubaliana kukuuzia hicho kitu kunakua na mwenzake pembeni anasikilizia na ndio huyu mwenye kanyanga...sasa wakati wewe unatoa pesa..anaweza hata kukuzuga wakati huo anapokea Kwa yule nwenzake kile kitu fake..na Mara nyingi bidhaa inakua kwake mpaka mkubaliane.
Mkuu hizi mipigo zote hazina shahidi wala nani mnakua wawili tu ...na unalizwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipewa buku na baba nikanunue Shati la shule. Nikafika mitumbani nikakuta wale jamaa wa Karata tatu.. Weka hapa unapata, hapa unakosa.
Nikaangaliaaa, nikaona kabisa kete ile pale.
Nikaweka ile buku.
Jamaa wakaanza kunipampu "Dogo ongeza hela ule zaidi"
Nikawaambia sina nyingine. Funua hapo nilipoweka hela yangu.
Kufunua chaliiiii.... Kete ikahamia mwanzo.
Daaah.. Nakumbuka niliporudi nyumbani baba alinichapa sana.
sipendi hizo mambo wala siji jaribu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom