Kama TAMISEMI walifahamu ualimu ngazi ya cheti unafutwa, kwanini zile ajira 13000 waliwahusisha Grade A?

Ualimu ngazi ya cheti umefutwa rasmi na walimu hao wanatakiwa kujiendeleza, Je, kulikuwa na ulazima wa kuwapa nafasi walimu wa cheti WAOMBE AJIRA wakati cheti chao kimefutwa?
View attachment 1585506
Huko ni kukurupuka! Je watakaoshindwa kujiendeleza watafukuzwa? Au ndiyo muendelezo wa kunyanyasa waalimu wazee ambao hawana uwezo wa kujiendeleza?
 
Huko ni kukurupuka! Je watakaushindwa kujiendeleza watafikuzwa? Au ndiyo muendelezo wa kunyanyasa waalimu wazee ambao hawana uwezo wa kujiendeleza?
Hawa tunajiandaa kuwala vichwa kama 'tukipita' kama tulivyo washughulikia wale vyeti feki.
 
Uwalimu ngazi ya cheti, si wale ambao advance hawakupita ?

Nauliza wana-ndugu? naomba na ufafanuzi kama sipo sahihi.
 
Ualimu ngazi ya cheti umefutwa rasmi na walimu hao wanatakiwa kujiendeleza, Je, kulikuwa na ulazima wa kuwapa nafasi walimu wa cheti WAOMBE AJIRA wakati cheti chao kimefutwa?

Kuna ajira ya wapi hapo mmechotwa tu akili mpige kura? Ccm hoyeee. Wanawajua kuwa waalimu ni wengi halafu hawafikiri nje ya box hata kama wataumizwa kiasi gani. Hii ni dharau kubwa sana kwa waalimu na kwa waTanzania wote. Kwanini wawaache waalimu miaka 4 mizima halafu waanze kujifanya wanawapenda mwaka huu wa uchaguzi. Wakiwaumiza vizuri ndio mtapata akili. Mumpe mitano tena, mtasimulia. Wamefuta Cheti, lakini mtalipwa mshahara kama wa cheti, subiri mtaona. Kila la heri.
 
Wametengeneza tatizo halafu kuna kuna mgombea urais atakuja hapo kutatua tatizo kisha ataombea kura
 
Sasa ni Mungu pekee wa kutufariji, hakika wengi tutakufa mioyo ikiwa inavilia kwa ndani!
 
Ni kwasababu hizo ajira 13,000 zilizotangazwa ni chai za kisiasa hakuna hata mtu mmoja atakayeajiriwa.
Kuajiri mtu ni mipango ya muda mrefu, kuanzia mshahara wake, malipo yake akiugua, atakae kaimu nafasi yake akiugua, malipo yake ya likizo, kuongeza ya mshahara ya kila mwaka nk.

Ukisikia ajira 13,000 zinatangazwa ghafla ni lini walikaa na kuratibu yote haya!
 
Back
Top Bottom