Siku ya Mwalimu Duniani: Wizara ya Elimu yafuta rasmi mafunzo ya Ualimu wa shule ya msingi na awali ngazi ya Cheti Tanzania

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
7,289
2,000
Wakuu Salaam;

IMG_20201005_111806_012.JPG

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefuta mtaala wa ualimu wa ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi ikiwa ni hatua ya kuboresha elimu nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo, Dk Ave Maria Semakafu amesema hatua hiyo inakwenda sambamba na kufanyia kazi maoni ya wadau ambao wamekuwa wakiyatoa likiwemo kufuta mtaala huo.

“Mtaala ulioboreshwa unatoa nafasi kwa mwalimu katika mwaka wa pili wa masomo kuchagua eneo la umahiri atakalobobea tofauti na mfumo wa zamani ambao haukuwa katika muktadha huo,” amesema.

Amesema mtaala huo mpya utaanza kutumika katika mwaka wa masomo 2020/2021 na kwamba mwalimu yeyote mwenye cheti cha ualimu atakuwa na sifa ya kusomea Diploma ya Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi na vile vile atakapohitimu na kufaulu atakuwa na sifa ya kujiunga na Chuo Kikuu kupata Shahada ya Kwanza ya Ualimu kwa elimu ya awali au msingi.

“Programu itakayofundishwa itakuwa ya miaka mitatu na masomo yatafundishwa kwa lugha mbili ambazo ni Kingereza na Kiswahili kutokana na kuwepo kwa shule za English Medium nchini,” amesema.

Amesema waliosoma Astashahada (cheti) bado serikali inatambua uhitimu wa cheti katika kada ya ualimu na ipo kwenye mfumo wa utumishi na itaendelea kuwepo na hakuna mwalimu atakayefukuzwa kazi kwa kuwa yeye ni mwalimu wa ngazi ya cheti.

Kwa mujibu wa Semakafu, walimu walioko kazini watakaopenda kujiendeleza wanaweza kusoma kwa masafa kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kwa njia ya masafa, njia ambayo haitaathiri utendaji na mwisho kufanya mitihani ili kupata Stashahada.

“Kwa walimu ambao wana vyeti na hawajaweza kupata fursa ya ajira, watatakiwa kurudi vyuoni na kuweza kupata Diploma ya Ualimu,” amesema.

1601909926046.png

--


Nini maoni yako kwenye uamuzi huu?

UPDATES
Rais Magufuli atengua uamuzi huu kwa kupiga simu mubashara akiwa katika kongamano la waalimu

Zaidi kuhusu habari hii soma;
Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti
 

F11

Member
Aug 21, 2019
42
95
Uamuzi upo mkononi Mwako Tarh28="Tate Mkuu, post: 36908456, member: 535381"]
Taarifa mbaya hii kwa sisi tulio omba maombi ya ajira ya ualimu Serikalini mwezi uliopita tukitumia hivi vyeti vyetu vya Grade A.

Magufuli tuokoe baba! Tutaangamia mtaani.
[/QUOTE]
 

Babluu

Member
May 25, 2020
21
45
Mimi naona walichelewa kuboresha hilo ila Ni muda muafaka KUFANYA HIVYO.Ili kuendana na soko la dunia kwenye ajira.Nadhani siyo Mheshimiwa Rais kafanya hivyo ila Ni wakati tulionao NDIYO unahitaji hivyo .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom