Kama Serikali imepeleka miswada kadhaa kwa hati ya dharula, kwanini isipeleke wa kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi wenye maslahi mapana kwa Taifa?

Tunafahamu kuwa serikali yetu imekuwa "bingwa" wa kupeleka miswada kadhaa Bungeni kwa hati za dharula, swali kubwa ninalojiuliza hivi sasa ni kuwa kutokana na kilio cha mamilioni ya watanzania wanaotaka Tume huru ya uchaguzi, ni kwanini serikali hii inapata "kigugumizi" cha kupeleka muswada huo Bungeni?

Tunajua pia kuwa kwa Maelezo ya viongozi wengi wa CCM wanauona upinzani nchini, unapumulia "mashine" na wakati wowote utakufa, sasa sioni kitu kinachowazuia hao CCM wasipeleke muswada Bungeni, wa uundwaji wa Tume huru

Vile vile tunafahamu kuwa kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, uliofanyika mwishoni mwa mwaka Jana, ambapo chama hicho kikongwe barani Afrika cha CCM kilijizolea ushindi wa kishindo wa asilimia 99.9 na upinzani kwa ujumla wao waliambulia asilimia 0.1 pekee!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi ni kwavipi CCM iuogope sana upinzani nchini, ambao wao wenyewe wanadai kiwa unapumulia "mashine" na wakati wowote kutoka sasa watauzika rasmi?

Mwenye kujua sababu zinazowafanya hao CCM wawe na "mchecheto" mno kupeleka muswada Bungeni wa uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi, naomba atujuze
Jibu ni rahisi mno CCM wote wamechafuka wananuka kinyesi wanaogopa kuja kushitakiwa kwa madhambi waliowatendea watanganyika
 
Alafu baada ya kuona vitisho vya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na mabeberu eti mtu anasimama na kutoa maneno matupu eti "uchaguzi wa 2020 utakua huru na haki na tutawakaribisha mabeberu waje kujionea"

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua Mkuu Daudi Mchambuzi ndipo hapo tunapotaka kuuona huo unafiki wake.............

Tunamuomba apeleke muswada wenye hati ya dharula ya uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi........

Akikataa tutarudi kwa mabeberu na kuwaambia kuwa huyu jamaa aliwapiga "changa la macho" alipowahakikishia kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki
 
Katiba mpya siyo priority kwa chama Cha a
Mapinduzi kwa Sasa wanaona Kama no jambo la kawaida ila ipo siku hizi kelele za raia zinazowalilia kuhusu katiba mpya wataelewa
 
Unajua Mkuu Daudi Mchambuzi ndipo hapo tunapotaka kuuona huo unafiki wake.............

Tunamuomba apeleke muswada wenye hati ya dharula ya uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi........

Akikataa tutarudi kwa mabeberu na kuwaambia kuwa huyu jamaa aliwapiga "changa la macho" alipowahakikishia kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki

Mkuu uko sahihi, bila wapinzani kuidai, hao mabeberu watakuwa hawana nguvu ya kuchukua hatua.
 
Iliyopo hatuiamini maana muundo wake inageuka kuitumikia ccm, na mifano hai ya tume kutokuwa huru imejidhihirisha hasa wakati wa chaguzi za marudio.

Kinachotakiwa ni utashi wa kisheria - tume iliyopo ni nzuri sana. Kama kuna shida sehemu si sababu ya tume - tatizo ni sisi wananchi.

Tume tunayo wenyewe ila sauti zetu haziwafikii tume kipindi cha uchaguzi, duniani kote hakuna nchi iliyopata tume na uhuru wa kidiplomasia kinalenale - it's force against.
 
Ndio ninachowaambia hawa wadau wenzangu wa upinzani, tuidai tume kwa nguvu zote. Hatuwezi kuendelea kushiriki chaguzi zinazonajisiwa kiwazi wazi hata baada ya miaka 25 ya mfumo wa chama kimoja.
 
Yani mimi ni mpinzani kabisa lakini nasikitika kuona kuwa walio na uwezo wakutamka kuwa tunaenda barabarani kuidai tume huru kuanzia kesho wako kimya

Wanasubiria kubambikiziwa kesi tu
Nashauri waliamshe dude ili mkuu akitaka kupiga risasi apige watakaobaki wabaki ili kizazi kijacho kinufaike na uhuru wa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio ninachowaambia hawa wadau wenzangu wa upinzani, tuidai tume kwa nguvu zote. Hatuwezi kuendelea kushiriki chaguzi zinazonajisiwa kiwazi wazi hata baada ya miaka 25 ya mfumo wa chama kimoja.
Naunga mkono hoja yako Mkuu tindo kwa asilimia 100
 
Tume huru ifanye nini - iliyopo ina shida gani?
Laiti ungeiruhusu akili yako kuwa huru kwa sekunde kumi tu, ungefuta ulichoandika! Acha kuendekeza utumwa wa kifikra! Una uhakika tume ya uchaguzi ni huru? Na Kama ni huru, ni kwa kiwango gani? Na unadhani kila kitu ni timamu kwa asilimia zote? Kama huamini hivyo Basi hata time ya uchaguzi Ina kasoro nyingi zinazohitaji maboresho na mabadiliko!
 
Siku hiyo ya kudai tume huru pamoja na katiba haitakuwa kwa mapenzi ya ccm, kwani ccm kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi. Kamwe haitakubali. Na Kama ni kweli wengi wanavihitaji(tume na katiba), kukataa ni sawa na kuwa fadhi kutawala watu ambao wanakupigia mkofi ukiwepo, uliwapa kisogo wanakung'ong'a.Weka mchakato wa kupata katiba mpya, time huru itaainishwa ndani yake.

Ukiwa single sided huwezi kuhukumu kuhusu hoja hiyo ya tume ya uchaguzi - kazi za tume ziko wazi sana, tatizo ni kuwa watendewa ni vilaza - kaka mabadiriko yoyote ya kiuchumi, kisiasa au kijamii lzm yaanzie kwenye jamii yenyewe.

Umekaa umenyoosha miguu halafu unataka mabadiriko! Umetambua challenge za tume halafu unabwekea uvunguni tena hata id yako fake! Awake
 
Siku hiyo ya kudai tume huru pamoja na katiba haitakuwa kwa mapenzi ya ccm, kwani ccm kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi. Kamwe haitakubali. Na Kama ni kweli wengi wanavihitaji(tume na katiba), kukataa ni sawa na kuwa fadhi kutawala watu ambao wanakupigia mkofi ukiwepo, uliwapa kisogo wanakung'ong'a.Weka mchakato wa kupata katiba mpya, time huru itaainishwa ndani yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Absolutely true
 
Hati za dharura ni kwenye makinikia na kuwabana wapinzani..
Kwa hiyo Mkuu FUSO siyo kwa uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi, kwa maslahi mapana kwa Taifa?

Hakika Taifa hili linaelekea shimoni na litaangamia
 
Unahitaji maendeleo au nia yako ni kuona Chadema inatawala.
Nahitaji maendeleo, lakini vile vile nikiona demokrasia ikiimarishwa nchini

Sitakuwa tayari kuona maendeleo yanayokuja kwa uminywaji wa demokrasia nchini
 
Back
Top Bottom