Kama Serikali imepeleka miswada kadhaa kwa hati ya dharula, kwanini isipeleke wa kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi wenye maslahi mapana kwa Taifa?

Tume iliyopo sio huru kwa kuwa inateuliwa na kada wa chama kimoja kwa mujibu wa katiba iliyopo ambayo haijarekebishwa iandane na mfumo wa vyama vingi.
 
Yani mimi ni mpinzani kabisa lakini nasikitika kuona kuwa walio na uwezo wakutamka kuwa tunaenda barabarani kuidai tume huru kuanzia kesho wako kimya

Wanasubiria kubambikiziwa kesi tu
Nashauri waliamshe dude ili mkuu akitaka kupiga risasi apige watakaobaki wabaki ili kizazi kijacho kinufaike na uhuru wa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Yap hiii ndo solution mengine porojo
 
Nyinyi maccm ndiyo kila kukicha mnasema kuwa upinzani nchini imejifia wenyewe.......

Sasa ni kwanini mnashikwa na "mchecheto" wa kupeleka muswada Bungeni wa uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi?
Wanafahamu ukweli kuwa Tume ikiwa huru, October 28, saa 2 asbh wanageuka chama cha upinzani
 
Tume huru ni dhana tu ambayo haina uhalisia. Tume ya sasa inaundwa na binadamu, unachokiita tume huru pia itaundwa na binadamu. Kama wabunge wa chadema wamenunuliwa mchana kweupe unadhani ni wajumbe gani wa tume watakuwa na msimamo wa kupindisha matokeo?
 
Inatakiwa wapeleke ittupwe, kisha kwenye bunge la ukweli ambao ni wananchi ipigwe kelele kama yote. Kwa hili wapinzani wanachemsha.
Kwa kuwa Bunge saivi halipo, toeni hoja zinazotekelezeka. Tufanye nini kwa muda uliobaki kupata Tume huru?

Watawala wanajua kukiwa na Tume huru hawatapata kura za kutosha kuwarejea madarakani. So, ni jukumu la wapinzani na umma kwa ujumla kutafuta namna ya serikali kulazimika kufanya hivyo kwa SHURUTI
 
Unahitaji maendeleo au nia yako ni kuona Chadema inatawala.
Nia ni kuona kura za wananchi zinaheshimiwa. Tume ikiwa huru wananchi kwa hiari yao wakachagua ccm, hakuna shida. Ila kwa sasa, wapiga kura wakichagua X, Tume inatangaza Y kuwa mshindi
 
Kwa kuwa Bunge saivi halipo, toeni hoja zinazotekelezeka. Tufanye nini kwa muda uliobaki kupata Tume huru?

Watawala wanajua kukiwa na Tume huru hawatapata kura za kutosha kuwarejea madarakani. So, ni jukumu la wapinzani na umma kwa ujumla kutafuta namna ya serikali kulazimika kufanya hivyo kwa SHURUTI

Mimi nilishauri kuwa toka mwezi machi, watangaze kuwa kila jumamosi ya mwanzo au mwisho wa mwezi kuwa na maandamano ya kudai tume huru. Bahati mbaya Covid 19 ikashika kasi. Baada ya bunge kuvunjwa nikitagemea moto uendelee wa kudai tume huru, cha ajabu naona watu wanazungumzia kushiriki uchaguzi zaidi kwa sauti, kuliko hata umuhimu wa hiyo tume.
 
Back
Top Bottom