Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,483
- 30,155
Tunafahamu kuwa serikali yetu imekuwa "bingwa" wa kupeleka miswada kadhaa Bungeni kwa hati za dharula, swali kubwa ninalojiuliza hivi sasa ni kuwa kutokana na kilio cha mamilioni ya watanzania wanaotaka Tume huru ya uchaguzi, ni kwanini serikali hii inapata "kigugumizi" cha kupeleka muswada huo Bungeni?
Tunajua pia kuwa kwa Maelezo ya viongozi wengi wa CCM wanauona upinzani nchini, unapumulia "mashine" na wakati wowote utakufa, sasa sioni kitu kinachowazuia hao CCM wasipeleke muswada Bungeni, wa uundwaji wa Tume huru
Vile vile tunafahamu kuwa kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, uliofanyika mwishoni mwa mwaka Jana, ambapo chama hicho kikongwe barani Afrika cha CCM kilijizolea ushindi wa kishindo wa asilimia 99.9 na upinzani kwa ujumla wao waliambulia asilimia 0.1 pekee!
Ndipo hapo ninapojiuliza hivi ni kwavipi CCM iuogope sana upinzani nchini, ambao wao wenyewe wanadai kuwa unapumulia "mashine" na wakati wowote kutoka sasa watauzika rasmi?
Mwenye kujua sababu zinazowafanya hao CCM wawe na "mchecheto" mno kupeleka muswada Bungeni wa uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi, naomba atujuze