Kama pato lako ni chini ya milioni 3 jenga ghorofa la Kinyakyusa ukiwa na ndoto ya kujenga ghorofa kwa sasa!

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,356
5,871
Ujenzi wa sasa ni gharama,

Ukitaka ujenge haraka, jenga nyumba ndogo. Ili iishe haraka, uhamie.

Tumetembelea maeneo mengi. Nimeona, wengi waliojenga majumba makubwa, wameishia njiani.

Endapo una ndoto ya kujenga ghorofa na kipato chako NET ni chini ya milioni tatu kwa mwezi, sikushauri.

Ila kama una ona ni muhimu sana kujenga ghorofa, basi jenga ghorofa la 'nusu nyumba, nusu ghorofa'... maarufu kama 'ghorofa la kinyakyusa' kutokana na ujenzi wa aina hii kushamiri jijini Mbeya 😀😀😀

images (6).jpeg
images (5).jpeg
images (3).jpeg
images (4).jpeg
 
Mimi sio mpenzi wa ghorofa,ukizeeka tabu ,ukiumwa tabu..sitaki
Duh wabongo siwawezi kwa nongwa. Yaani ulichukie ghorofa kwa hizo sababu. Kwani ukiwa na chumba chako, sebule yako na jiko chini huko juu ukawaachia wenye uzima say watoto itakuwaje? Miji inatakiwa iwe na maghorofa ili ardhi itumike vizuri sio propaganda za umaskini kama hizi
 
Back
Top Bottom