Kama nchi tunakwama wapi kusimamia mabasi ya Mwendokasi?

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
514
973
Kuna kilio cha wananchi kila kona kuhusu mabasi ya mwendokasi. Mabasi haya yanajaza pasipo mfano. Mabasi hayatoshi. Mabasi mengi yameharibika na yako yadi na hakuna matengenezo. Watu wanachelewa kufika kazini.

Kutokana na tatizo hili wananchi wameombaa kuwa daladala isaidie mabasi ya mwendokasi kwa kupita katika njia zao. Ninajiuliza hivi Watanzania tunakwama wapi. Kila tunachopewa kukiendesha sisi tunakiharibu. Hata hiyo SGR ambayo karibuni itaanza kazi mwishoni itakuwa kama mabus ya mwendo kasi. Sijui tumelaaniwa?
 
Yaani inatia hasira sana. Hata kusimamia mabus hatuwezi. Ma bus yenyewe yana njia yake. Hayana mshindani, hayasumbuliwi na traffic wala Sumatra.

Imagine kuna wazawa hata shule hawajasoma ila wana daladala kibao wanazisimamia hazifi na zinapata faida nzuri.

Ila wasomi na ma digrii na masters hawawezi kusimamia mabus ambayo yana wateja wa kumwaga
 
Back
Top Bottom