Kama naanza kuichoka Azam TV vile

Kama naanza kuichoka Azam TV vile

mseseve

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
511
Reaction score
89
Nilikuwa na kimuhemuhe na kiroho papo kuwa na kisimbuzi cha Azam Tv ndio, ni kutokana na jinsi walivyokuwa wanajimwambafy (kujisifia kwa ubora wa miatambo na modern technology na watangazaji manguli), tuna studio bora kama za Al-Jazeera na BBC...l

Lakini pamoja na hayo yoote naona swala la uchangamfu wa channel zao na uchanganyaji picha, bado sanaaa.. Na hata ule ubunifu wa watangazaji kupresent taarifa ili kumvutia mtazamaji haupo..

Nilitegemea utumizi wa technology kama tunavyoona BBC na Al-Jazeera wanavyofanya bt kinyume chake naona hakuna utofauti na channel zingine ambazo si Pay Tv kama Clouds Tv n.k..

Utangazaji na uwasilishaji wa habari hauko designed, uondoshaji wa habari moja kwenda nyingine bado uko local sana... Bora hata kuangalia EATV wamechangamka na wanacheza na technology vizuri.. Sijui ni kwanini hawajilinganishi na international Tv, wanabaki kuwaza kushindana na local tv za kibongo..

Jueni kuwa tunatoa hela kupata huduma zenu..
 
Sijui kwanini sijawahi na sina mpango wa kuitumia Azam, sijawahi kushawishika nao. Mi ni startimes na Dstv inatosha.
 
Channel zao za sinema za kiingereza zinaonyesha Cinema za zamani na mbaya zaidi mitangazo inapita kila baada ya dakika chache mpaka inaboa.......
 
Azma ungetaka kuwafaidi ungenunua decoder kabla ya uchaguzi
walikuwa best tv kipindi cha uchaguzi

sasa hivi toka sakata la makontena kuna kitu kimepungua
ni kama kuna kitu kimeathiri hivi tv yao....
nahisi hawataki tena kujitolea sana na habari za serikali
 
Sinema zao nazo ni zile zile kila siku.. tena ni za zamani kishenzi...hiyo chaneli wangeitoaga tu..michaneli ya kiarabu kiiibaaaooo
 
Duh, kesho nilitaka kwenda kununua kumbe ni majanga??

Sasa mnishauri kisembuzi kizuri nikipi?? Maana m nilitaka kwa ajir mpira, na ubora wa pc ninacho cha startimes yaan ni majanga,

Wadau plz ushaur
 
Mimi hoja yangu kubwa ni kwamba hawajui kucheza na technology iliyopo/iliyoinvestiwa hapo..labda hawana ma IT nguli..yaani kikubwa hakuna tofauti na local chanels tena kuna nyingine unafurahi kuangalia vipindi vyao coz vinashawishi na wafanyakazi ni wachangamfu...mfano mzuri hata ukiangalia kina kikeke bbc swahili wanaonesha kuwa wako kwenye tv ya levo zingine na hata uchanganyaji wa habari na picha uko sawa
 
Duh, kesho nilitaka kwenda kununua kumbe ni majanga??

Sasa mnishauri kisembuzi kizuri nikipi?? Maana m nilitaka kwa ajir mpira, na ubora wa pc ninacho cha startimes yaan ni majanga,

Wadau plz ushaur

Baada ya azam kuboa hakuna nyingine zaidi ya kuji Dstviisha
 
Tatizo la baadhi ya wafanya biashara na Wasomi Africa, wako tayari kuficha ukweli hata kama wanaumia, ukweli' ili kupata watanzamaji na wasikilizaji ni lazima uwe na vipindi vinavyogusa uhalisia wa maisha na matatizo ya watu, na hapo lazima uiseme serekali na wao wanaogopa kwani kuna mahali wanajua hawako sawa ktk biashara zao, ili ufanye biashara Africa lazima ukwepe kodi,ujipendekeze kwa viongozi na uchangie gharama za uchaguzi na vyama tawala kwani sheria ni mbovu na zimewekwa ili kuwafilisi watakaoisema serekali, kwa mfanya biashara halisi anayetumia faida yake ili kupata faida na biashara zake zinamakao africa hawezi kuwekeza kwenye media.
 
Azma ungetaka kuwafaidi ungenunua decoder kabla ya uchaguzi
walikuwa best tv kipindi cha uchaguzi

sasa hivi toka sakata la makontena kuna kitu kimepungua
ni kama kuna kitu kimeathiri hivi tv yao....
nahisi hawataki tena kujitolea sana na habari za serikali

Walikuwa?hapana hapana...pamoja na kuwa na mitambo bora ya urushaji matangazo, lakini bdo walikuwa wanakatikakatika na hata watangazaji walikuwa bado wageni wa technology mfano ni ile touch tv yao waliyokuwa wanaitumia kwa uchambuzi, watumiaji walikuwa wanaigusa kama hawajiamini/hawakuwa na confidence ya kutosha, na wakati mwingine utakuta anaigusa mara mbilimbili ili picha ifunguke..kiukweli wanaweza kuwa na mitambo na vifaa vizuri bt baaaaado sana...
 
Back
Top Bottom