Kama mwanamke anakulalamikia haumjali kisa haumtumii ujumbe au kumpigia simu kila saa, mwambie hivi...

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Ukiwa na mwanamke asiyejiamini atataka umpigie na kumtext kila muda ili ajisikie kupendwa na aone unamjali. Mara nyingi wanawake ambao hawakupata upendo mzuri wakiwa wadogo hufanya hivo, kila muda wanataka wapetiwe wajisikie wanapendwa.

Pia ukiona mwanamke anakukera kwa kutaka muda wote umtafute na umhakikishie kuwa unamjali ujue ulimzoesha hivyo wakati unamtongoza ulikua unampa nafasi kubwa sana kiasi kwamba amezoea ile ndo hali itakayokua mkiwa wote miaka yote.

Lakini imefikia hatua kwako inakukera mana inachosha na ubaya zaidi mwanamke naye anakukera zaidi anapolalamika haumjali sababu hujamtext au hujampigia simu.

Cha kufanya ni kuongea na mwanamke jinsi anavyokufanya ujisikie na jinsi inavyokukera.

Mfano, analalamika haumjali kwa kuwa haumtumii text kama za ‘good morning’ ‘usiku mwema mpenzi’. Mpe ukweli kwamba unampenda lakini kutuma izo text kila siku inachosha, huwezi amka kila siku asubuhi na jambo la kwanza ufikirie kumtext za asubuhi, una mambo mengine ya kufikiria na unahitaji muda ummisi ili ukimtumia text ziwe na ukweli ndani yake sio kumtext kwa sababu unaogopa ataona humjali au atalalamika.

Kama ulishamzoesha kuongea naye kila siku kwenye simu kwa masaa, na sasa unaona inachosha, lakini ye analalamika anataka muongee muda wote ili aone unampenda, mwambie ukweli kwamba unampenda lakini kuongea naye masaa hayo yote inachosha/ inakera au vyovyote ujisikiavyo, una mambo mengine ya kufanya, na ungependa muongee mkiwa mmemisiana kweli kweli sio muongee kwa sababu unaogopa ataona humjali au atalalamika.

Mwanamke anayekuchunga kwenye simu, muda wote anakutafuta kwenye simu ili ahakikishe haumsaliti pia mwambie hivyo.

Ni heri uwe na mwanamke anayejiamini au kama uliyenaye hajiamini basi mshauri aende kwa wataalamu wamsaidie kuhusu hilo kuliko kuumia moyoni ili kumtuliza mwanamke asiyejiamini, mwanamke asiyejiamini atayafanya maisha yako kuwa magumu badala ya kuufanya uume wako kuwa mgumu.

Simu sio kwa ajili ya kutunza upendo, simu ni kwa ajili ya kupanga kukutana na mkuze upendo mkiwa pamoja.
Katika kundi la infinite kiumeni ndio sehemu pekee utakayojifunza na wanaume wengine ili kuwa bora na kujiamini zaidi katika mahusiano na mapenzi na mwanamke unayehitaji kujenga naye maisha.
 
Huyu umemsema ex wangu tuliachana kisa hizi mambo akaenda huko now anakuja kutoa mbusus then anarud kwa bwana yake
 
Nilishawahi kuwa na demu wa hivyo nikapiga chini maana alikuwa ananiganda Kama kupe.
 
Mapenzi ni mzigo wa marashi, unafurahia harufu tamu huku unapinda mgongo
 
Ndo kupendwa kwenyewe huko

Ngoja uumkute anayekutext au kukupigia anapotaka akupige kizinga utamkumbuka huyo anayetaka uumtumie meseji za usiku mwema mpenzi
 
Mawasiliano ndiyo kigezo Cha kwanza kuonesha Upendo kabla ya vitendo.Kama unampenda kweli na unaona anakulalamikia Kwa ajili ya kutomtext au kumpigia na kuona humpendi ni vizuri ukawa unafanya hivyo vitu maana ndyo akili yake ilivyojijenga.

Kwani ukimfanyia hayo anayosema utapungukiwa nini ndugu.Kila mtu anatafsiri Upendo Kwa mapana yake na akimpata anayemfanyia hayo mambo unayokataa kumfanyia utakuja kuandika Uzi mwingine hapa wa kumlalamikia.Kumjulia mtu hali na kumtumia text za mapenzi fupi inachukua dakika ngapi kwani ,inagharimu pesa kiasi gani?

Mapenzi ni kujaliana hebu mjali mwenzako.Mbusu , mkumbatie,ajione malkia hata hiyo papuchi ataitoa kwako kirahisi.
 
Back
Top Bottom