Enzi za utoti wangu niliiuwa mtu wa Mungu sana lakini sikuwahi kumuona.
Hakuna tofauti ya maisha kipindi kile na sasahivi, tofauti ni kwamba kipindi kile nilikuwa mtu wa kanisani sikuhizi nimeacha
Hakuna hayo mambo ya kwamba ukiwa mtu wa Mungu atabadili maisha yako, utakuwa na nuru kwenye maisha yako.
Sio kweli, sasahivi ni almost atheist ila sioni kama kuna kitu nimepoteza
Kingine ni kwamba inanikera wazungu walivyotuletea dini zao, au waarabu pia
Nikiwa naabudi Mungu wa wazungu naona kama nawanyenyekea sana wazungu
Wao walileta dini ili kutawala waafrika kirahisi, wakafuta dini walizozikuta Africa na kusema Mungu wa ukweli hazipendi.
Kuna muda natamani wazungu na waarabu wasingeleta tu dini zao. Zimetuharibia mno jamii zetu