Kama MDDU Unit ya TANESCO ni Mali ya Maharage, Basi astaafishwe kwa manufaa ya Umma

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Pale TANESCO kuna tatizo, wafanyakazi wameshajikatia tamaa sababu wanaona Ofisi ya Umma imekuwa Ofisi ya Upigaji kwa Viongozi wa juu.

Maharage alipo pelekwa pale TANESCO, alianzisha mfumo wake wa kupiga hela, akaanzisha Managing Director delivery unit - MDDU. Akaweka watu wake, halafu akawaambia wahame kutoka pale Ubungo, akawapa Full Ofisi pale Kimara.

Kumbuka Rais alikuwa hajui undumilakuwili wa Maharage kwani Maharage kapelekwa TANESCO na Januari Makamba.

Makamba ndo alimpendekeza kwa Rais kwa kumpa sifa kedekede hata ambazo hana ili Rais amuone wa Maana. Kumbe nia ya Makamba ni kuweka mshikaji wake ili Madili yake yapite kirahisi tanesco.

Halafu wakamuomba Rais Samia Trilioni Shilingi zadi ya 11 kwamba wakiipata hiyo hela umeme utatengamaa, wakampa rais mpango kazi feki rais Samia akashitukia dili akakataa. Baadaye Dili likatiki wakapewa Bilioni 500. katengeneza MDDU na Erolink.

Sasa wakawa wanakatakata umeme ili kumtia presha Rais ili aone umuhimu wa kuwapa hela nyingi wanazotaka. Yaani Rais aone tatizo ni kubwa awape Matrilioni wayachakate🤣

Ukitaka kuwaona washirika wa Maharage, nenda Kimara TANESCO uliza Ofisi ya MDDU ipo wapi.

Wanatengewa hela nyingi na kupewa majukumu yasiyo kuwepo then hela wanagawana.

Maharage hata ahamishiwe Nangurukuru bado kuna 10% yake ya fedha za miradi. Lazima wampe. Si kawapa ulaji na hela zao bodi ilipolitisha? Hivyo kila mwezi zinaingia.

Rais angebomoa Cheni yote ya Nishati kianzia katibu Mkuu wao ili wapoteane. Pia wale wote waliopelekwa Tanesco na Maharage, aondoke nao.

Hivyo basi, kama kweli Maharage anahusika na wizi ndani ya TANESCO kwa kupitia hii Unit ya MDDU, basi naomba Rais amstaafishe kwa manufaa ya Umma.

TAKUKURU iingilie kati kwani si vibaya kumchunguza kiongozi. Wakikuta ana makosa awajibike kwa matumizi mabaya ya Ofisi.

Kama tunavyojua, Posta sasa hivi inashirikiana na Mwarabu wa Dubai, kapelekwa apige hela ya Mwarabu. Huwa haachi dili lolote. Safari hii Posta inauzwa Mazima🤣🤣
 
Hizi ndio habari zinazohitajika. Kuna kijana mmoja kigogo au Tanzania leak walimuongelea anaitwa Elihuruma ngowi alikuwa vodacom na mwamvita akaombewa kazi tanesco. Tanzania leaks wakahoji ajira yake haikufuata procedure nzuri zinazoeleweka ila aliajiriwa kimchongo na maharage. Naye alikiwepo huko Mddu.
 
Hapo sijaelewa kabisa yaani kesi ya nyani unaipeleka kwa ngedere
Huku unasema avunje kila kitu huko Tanesco na mtandao wake wa upigaji

Mwisho tena umejisahau unasema amepelekwa Posta kwa sababu mwarabu yuko huko na yeye haachii madili which is which?

Naona wote umewaweka group moja kuwa wanasaidiana upigaji ila kiaina na Umeme huko kelele zimekuwa nyingi sana
 
Hao wote wanajuana ni madili yao kama yule bibi angekua hausiki sasa hivi kipara ngwidu na maharage ya Mbeya wote wangekua ndani kwa kesi ya uhujumu uchumi, lakini kwakua lao ni moja ndio maana amewapa ulaji sehemu nyingine
 
Erolink na Deloitte wameletwa na Maharage kama Consultancy Firms za Upigaji tu, Jamaa hakuamini kabisa System za Ndani ila pamoja na Ilo wamepiga sana na Makamba mpaka unawaza hii Nchi ina Vyombo vya ulinzi
DG wa TISS/ Jaji Mkuu/IGP/DG wa TAKUKURU wote wanateuliwa na Rais nao wanaishi kwa upepo wa Rais, Makamba ni mtoto wa mjini akiiba mgao unafika mpk juu unategemea hawa dagaa watafanya nini?
 
Back
Top Bottom