Kama makanisa mengi hayafati sheria za agano la kale ni kwanini wanazifata amri 10 za agano la kale

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Kuna sheria kibao ambazo ziliwekwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe moja kwa moja kwenye agano la kale.

Sheria za wanyama wa kula alituamuru tusile nzi, vinyonga, punda, mbwa, paka, pweza, popo, nguruwe, nyani, mbu, n.k.

Sheria za mavazi alituamuru tuvae mavazi ya kusitiri, wanawake wasivae suruali, n.k.

Ila cha ajabu makanisa mengi yanafuata amri 10 tu, ni kwanini nazo zisifutiliwe mbali ?

kuna mistari ya agano jipya inarejea maandiko ya agano la kale

Hata Yesu alisisitiza sana hajaja kufuta sheria zozote, Mission yake kubwa alikuja kuzifuta kafara za wanyama zilizotumika kusafisha dhambi, damu yake ndio itatumika milele kujitakasa hakuna haja ya wanyama
 
Eti wachungaji wa leo kwenye zile sheria ndogo sheria muhimu ni ile ya Malaki 3 tu.
Kama Nguruwe alikatazwa kwenye old testament lakini sasa analiwa kwanini Fungu la 10 lisiondolewe sasa?
 
Mkuu DR Mambo Jambo naomba unifundishe Kwanini nguruwe alikatazwa? Kulikuwa na sababu zipi za kukataza nguruwe?
Kuna majibu Ya literal kibiblia zaidi na kuna majibu ya Spirituality mkuu..
Kwa majibu ya haraka haraka ni ..

WALAWI 11:7

"Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu"
 
Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu"
Hapa sasa ndio huwa nataka kuelewa nafahamu wewe ni daktari pia.
Kwato, hacheui hii imekaaje embu iweke katika sababu ambazo unaweza kunielezea kama daktari.

Je ana madhara au ni najisi kwa maana ipi?
 
Back
Top Bottom