Makelele ya makanisa kwenye makazi siyo sawa kidini, wala kisheria; yadhibitiwe kama makelele mengine

T Kaiza-Boshe

Member
May 27, 2013
20
39
Makelele ya makanisa kwenye makazi yanakera na kuathiri watu wengi sehemu za mijini, hasa jiji la Dar es Salaam. Aidha makelele hayo yana athari kiafya, kijamii, na hata kiuchumi; kama ilivyo makelele mengine. Na wakati mwingine yana athari zaidi kutokana na kuendelea muda mrefu, bila kuruhusu watu wakapumzika, ama kusikilizana majumbani. Watu wengi wamelalamika, lakini inaelekea serikali inapata kigugumizi kuwawajibisha wahusika kwa dhana ya kwamba ni watumishi wa Mungu!

Hivyo tarehe 10 Mei mwaka huu mtangazaji wa Clouds FM alivyomhoji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhusu kinachoonekana kuwa ubaguzi, ama upendeleo, inapokuja suala la kuwajibisha taasisi na biashara ambazo ni kero kwa wananchi kwa kupiga makelele, lilikuwa jambo la faraja na kupongeza.

Nawapongeza Clouds kwa ujasiri, kwa maana ni jambo lililohitaji ujasiri kuliibua na kuweza kuwahoji wahusika wakuu katika kuhimiza sheria zinazotulinda dhidi ya makelele kuhusu kinachoonekana kuwa upendeleo wa waziwazi katika kuwajibisha wahusika.

Kuna sehemu za jiji la Dar es Salaam walioathiriwa sana na kero ya makelele ya makanisa mpaka basi. Wamelalamika muda mrefu na kuchoshwa na mbinu za viongozi husika. Kwa mfano, katika mtaa mmoja, kanisa lilipachikwa katikati ya makazi kwenye kiwanja kidogo na kuta zilizojengwa na matofali ya matundu; na hivyo kuweza kupitisha makelele bila kizuizi (Angalia picha). Wakazi walianza kulalamikia kanisa hilo tangu linaanza kujengwa zaidi ya miaka 15 iliyopita bila mafanikio.

Mwanzoni ilidhaniwa kuwa kwa vile kwa wakati huo Diwani wa kata liliko kanisa hilo alikuwa Meya wa Kinondoni, ingekuwa rahisi kusimamisha ujenzi huo. Cha kushangaza ujenzi haukusimamishwa; licha ya wakazi kuendelea kulalamika hadi ngazi za juu. Ujenzi ulipoisha, makelele na mitetemo ya vyombo na ngoma vikaanza. Malalamiko sasa yakaelekezwa kwenye makelele na mitetemo. Mara mbili (ninazojua mimi, kunaweza kuwa kuna zaidi) malalamiko yalimfikia Mkuu wa Wilaya wa wakati ule, na wakati mwingine Mkuu wa Mkoa. Mara zote kanisa lilikuwa linapunguza makelele na mikesha kwa muda mfupi, halafu makelele yanaendelea kama kwaida.

Wakati mmoja kiongozi, ambaye pia ndiye mwanzilishi wa kanisa hilo, alipopelekwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa na kamati yake, aliahidi kuwa kusingekuwa na makelele na ibada za usiku tena baada ya kikao hicho. Aidha, kikao kilipofungwa siku hiyo, akaomba kusali (ilhali wengi wa wajumbe wa kikao hicho, pamoja na mwenyekiti, wakiwa ni Waislamu!) na kupeana mkono na wajumbe wote kama ishara ya kudhihirisha aliyoyaahidi. Ishara hiyo kwa sasa inaweza pia kutafsiriwa kama kujipa mamlaka kisaikolojia na kuwatia hofu wanakikao na uongozi. Ni mbinu za namna hiihii zinawawezesha viongozi wa dini kufanya mambo kinyume na maadili ya kiongozi wa dini ya Kikristo. Haikuchukua muda mrefu makelele na mikesha vikarudi palepale, japokuwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa wakati huo ni karibu na kanisa hilo. Mwenendo kama huu, popote penye matatizo kama haya, inafika mahali wananchi wananyamaza kwa kukata tamaa. Kwa wale wanaojiweza, wanajenga kwingine na kuhama; kwa wasioweza kuhama inabakia kuishi na kero na athari za kudumu.

Kampeni na matamko yaliyopita kuhusu makelele hajaleta unafuu, na bado kuta za kanisa hilo zina matundu ya kupitisha makelele. Kuna kipindi serikali iliwataka viongozi wa dini walishughulikie suala la makelele wenyewe kwa pamoja, kama ilivyofanya safari hii. Hii ina maana Serikali inaamini viongozi wa dini kwa umoja wao wanaweza kurekebishana. Muda ni shahidi. Kwa kipindi chote ambacho Serikali imeshughulikia tatizo hili tungekuwa tumeishaona mabadiliko. Kuna sehemu ambako hakujakuwepo mabadiliko hadi tamko la Mei mwaka huu. Lakini nako, yapo makanisa yaliyopunguza makelele, na yako ambayo hayakupunguza. Mathalan, kwa Kawe, Dar es Salaam, safari hii walao kumekuwa na nafuu kwa wanaosali kwenye viwanja vya Tanganyika Packers; lakini kanisa lililo kwenye makazi, bado!

Majibu ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC kwenye mahojiano na Clouds yanadhihirisha kuwa kuna viongozi wa umma wanaozingatia kuwastahi viongozi wa dini kuliko baadhi yao wanavyostahili; na hivyo kwenda kinyume na wajibu wao kisheria. Ni kweli Biblia inaelekeza kuwastahi viongozi wa dini, lakini pia inawaelekeza wao mambo kadhaa ambayo viongozi wanaohusika na kujenga kwenye makazi ya wananchi na kupiga makelele hawazingatii. Isitoshe Biblia imetuangaliza kuhusu viongozi wa dini feki na manabii wa uongo. Biblia pia imetuangaliza namna ya kumtambua Mtumishi wa Mungu wa kweli. Tunaelekezwa kuwatambua kwa matendo yao na matunda ya kazi zao. Kwa uhakika viongozi wa dini wanaovunja au kuwaongoza waamini ama wafuasi wao kuvunja sheria halali za nchi na kusababisha madhila kwa wananchi wenzao, hawafanyi hivyo kwa kumfuata Yesu, wala kufuata miongozo ya Biblia Takatifu.

Kiongozi mwema wa dini ya Kikristo atazingatia yafuatayo; ambayo yanayotokana na Biblia Takatifu, ama matendo ya Yesu:

1. Amri ya kumpenda mwenzako kama unavyojipenda wewe. Kwa kuwapenda binadamu wengine, viongozi wema wa Kikristo wanajali afya za jamii na amani wanakofanyia ibada. Aidha, kwa ujumla, jamii na serikali inategemea viongozi wa dini wawe msaada katika kutunza amani, na siyo vinginevyo.

2. Yesu alivyosali. Yesu alipohitaji kusali zaidi alikwenda mlimani, ama bustanini Getsemani, mbali na makazi ya watu. Viongozi wema wa Kikristo wakitaka kusali zaidi na kukesha watakwenda mbali na makazi, na kwa vyovyote hawatawapigia wananchi makelele yanayopita viwango.

3. Namna ya kusali. Biblia inaelekeza tusisali kwa kupayukapayuka. Hii imekuwa kama kawaida ya makanisa mengi yanayoibuka miaka ya karibuni; na katika kufanya hivyo wanapiga makelele yanayokera na kuathiri afya za majirani.

4. Mahusiano ya makanisa na mamlaka za utawala wa nchi. Biblia inaelekeza kuheshimu mamlaka zilizopo. Viongozi wanapowafanya wafuasi wavunje sheria, ama kukiuka miongozo ya serikali, wanakuwa wanakwenda kinyume na miongozo ya Biblia.

Ni dhahiri kutokana na vipengele hivyo hapo juu, kwamba baadhi ya makanisa kupigia wananchi makelele siyo sawa kidini, na hivyo haikubaliki.

Mbali na kwamba makelele ya makanisa yanayokera na kuathiri jamii kutokubalika kidini, serikali ina wajibu wa Kikatiba kuhakikishia wananchi wote, wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.” Je, vyombo vya Serikali vyenye wajibu wa kuhimiza sheria dhidi ya makelele visipowajibisha makanisa yenye kupiga makelele vinazingatia hili? Kwa kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jaffo, alivyonukuliwa na gazeti Uhuru la June13, 2023, hakuna tofauti kati matakwa ya Kikatiba na kile kinacholengwa na Serikali. Kwa maana Waziri Jaffo amenukuliwa akisema kuwa, “Serikali inataka ibada zifanyike na wananchi waabudu vizuri kwa amani, huku na wengine wakiwa na haki na kuishi bila kelele na bugudha.” Hii ina maana tatizo lipo katika utendaji, ama utekelezaji wa sheria na miongozo.

Aidha, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.” Hivyo, siyo sawa Kikatiba kwa Halmashauri, ama NEMC, kutowajibisha makanisa yanayovunja sheria; maana kwa kufanya hivyo, vyombo hivyo vya serikali vinakuwa vinakiuka Katiba ya nchi kwa kuwanyima wananchi haki zao, ilhali Waziri mwenye dhamana anasema Serikali inataka haki za wananchi zilindwe.

Na Theonestina Kaiza-Boshe
Email: tkaiza@gmail.com
 
Attachments

  • 20230509_121357.jpg
    20230509_121357.jpg
    1,002.2 KB · Views: 9
  • 20230509_121412.jpg
    20230509_121412.jpg
    1.3 MB · Views: 8
Makelele ya makanisa kwenye makazi yanakera na kuathiri watu wengi sehemu za mijini, hasa jiji la Dar es Salaam. Aidha makelele hayo yana athari kiafya, kijamii, na hata kiuchumi; kama ilivyo makelele mengine. Na wakati mwingine yana athari zaidi kutokana na kuendelea muda mrefu, bila kuruhusu watu wakapumzika, ama kusikilizana majumbani. Watu wengi wamelalamika, lakini inaelekea serikali inapata kigugumizi kuwawajibisha wahusika kwa dhana ya kwamba ni watumishi wa Mungu!
Hoja ya msingi hapa ni kwamba, mipango miji waje na sura mpya, kanisa au msikiti ujengwe sehemu ambayo pamepangwa nyumba ya ibada tu, sio makazi ya watu. hivyo hivyo na bar na kumbi za harusi na kumbi za starehe.

Nilimwangalia pm anavyoongea, nikaona sihitaji kusikia tena. kwasababu wanaolengwa hapa ni wakristo. waislam huwezi kuwazuia kupiga azana pamoja na yale mafundisho yao ya ijumaa au saa saba mchana kila siku. pamoja na kwamba kama wakiamua kusema sehemu iliyopangwa kwa nyumba ya ibada pekee ndio watu wajenge, misikini mingi sana imejengwa kwenye makazi na hakuna muislam atakayekubali msikiti kuvunjwa hata kama umejengwa ikulu.

Kwa wakristo hasa walokole kwasababu ndio wanaolengwa, wao pia wamekuja na makanisa mengi sana na ya ajabu tena kwenye makazi ya watu. wao ukisema unavunja kama kuna mbadala watakubali. sasa tukae chini, tukalishe dini zote pamoja tuwaambie kuwa tumeamua kuanzia sana majengo ya ibada makazi ya watu yasiwepo, tuwapatie maeneo mbadala wakajenge huko (kwa kuwalipa fidia) ili waondoke maeneo ya watu. la sivyo, kwa wakristo wanaweza kujenga makanisa yanayozuia makeleke kutoka nje, technolojia hiyo ipo. shida ni kwenye azana ya kwenye kile kipaza sauti cha wazi kama inawezekana kutumia tech inayozuia sauti.
 
Mimi ni mkristo ila suala la makelele sijawahi kuafikiana nalo kabisa, na sio kwa dini yangu tu hata na nyingine kama ipo.

Sauti inapaswa iwe toshelevu kwa walio ndani ya ibada tena kwenye jengo husika unless kama itaamuliwa kufanyika mkutano au mhadhara uwanjani hapo sawa maana huwa na muda wake, na sio usiku kucha bali katika vipindi maalum.

Wokovu ni wetu sote ila tusiendekeze bugudha
 
Hii inanikumbusha,kuna siku tupo msikitini halafu ng`ambo ya barabara kuna kanisa wanafanya misa ya kwenda kuzika,wamefungulia sauti ya juu..
Tukawaomba wapunguze sauti hawakuelewa..

Shekhe wa msikiti akatoa amri kwamba tukachukue udhu halafu tupige "kunut" tumshtakie ALLAH,Kuwa sisi wanyonge hatuna lakufanya kwa hawa majnuun ispokua wewe ALLAH..
Kilichotea anajua mungu alichofanya kwa wale khenzeer..
 
Hoja ya msingi hapa ni kwamba, mipango miji waje na sura mpya, kanisa au msikiti ujengwe sehemu ambayo pamepangwa nyumba ya ibada tu, sio makazi ya watu. hivyo hivyo na bar na kumbi za harusi na kumbi za starehe.

Nilimwangalia pm anavyoongea, nikaona sihitaji kusikia tena. kwasababu wanaolengwa hapa ni wakristo. waislam huwezi kuwazuia kupiga azana pamoja na yale mafundisho yao ya ijumaa au saa saba mchana kila siku. pamoja na kwamba kama wakiamua kusema sehemu iliyopangwa kwa nyumba ya ibada pekee ndio watu wajenge, misikini mingi sana imejengwa kwenye makazi na hakuna muislam atakayekubali msikiti kuvunjwa hata kama umejengwa ikulu.

Kwa wakristo hasa walokole kwasababu ndio wanaolengwa, wao pia wamekuja na makanisa mengi sana na ya ajabu tena kwenye makazi ya watu. wao ukisema unavunja kama kuna mbadala watakubali. sasa tukae chini, tukalishe dini zote pamoja tuwaambie kuwa tumeamua kuanzia sana majengo ya ibada makazi ya watu yasiwepo, tuwapatie maeneo mbadala wakajenge huko (kwa kuwalipa fidia) ili waondoke maeneo ya watu. la sivyo, kwa wakristo wanaweza kujenga makanisa yanayozuia makeleke kutoka nje, technolojia hiyo ipo. shida ni kwenye azana ya kwenye kile kipaza sauti cha wazi kama inawezekana kutumia tech inayozuia sauti.
Ahsante kwa mchango wa mawazo. Katika makala hii wametajwa Wakristo kwa sababu tatu: 1) Mimi ni Mkristo, hivyo nafahamu miongozo ya Kikristo; ya Kiislamu siijui.
2) Sehemu kadhaa nilikokaa nyumba za ibada zinazopiga makelele yanayozidi viwango kisheria ni za Kikristo, hasa makanisa ya Kilokole.
3)Kwa ujumla misikiti haipigi makelele yaliyo nje ya viwango kisheria, ama kukera. Na ibada za kiislamu za kiada ni fupi. Hivyo hawavunji sheria, wala kukera na kuathiri wananchi. Kuliwahi kuwa na miadhara ya maspika ya sauti kubwa, walipokatazwa waliacha. Azana (adhana?) ni kelele, lakini ni kwa muda mfupi sana, hivyo inakidhi matakwa ya sheria.
 
Ahsante! Mtu yeyote, ama taasisi yoyote, anaweza kutenda kosa kwa kutojua, ila akijua hana budi kujirekebisha. Ila inapotokea mtu akatenda kosa akiwa anajua, ama akakaidi sheria, na asijali madhila ya kosa lake kwa wengine, inakuwa kosa kubwa sana kwa dini yoyote na jamii yoyote ile; na Mwenyezi Mungu hapendi, kwa maana hakutuelekeza hivyo. Kisheria inakuwa kosa la jinai.
 
Ahsante kwa mchango wa mawazo. Katika makala hii wametajwa Wakristo kwa sababu tatu: 1) Mimi ni Mkristo, hivyo nafahamu miongozo ya Kikristo; ya Kiislamu siijui.
2) Sehemu kadhaa nilikokaa nyumba za ibada zinazopiga makelele yanayozidi viwango kisheria ni za Kikristo, hasa makanisa ya Kilokole.
3)Kwa ujumla misikiti haipigi makelele yaliyo nje ya viwango kisheria, ama kukera. Na ibada za kiislamu za kiada ni fupi. Hivyo hawavunji sheria, wala kukera na kuathiri wananchi. Kuliwahi kuwa na miadhara ya maspika ya sauti kubwa, walipokatazwa waliacha. Azana (adhana?) ni kelele, lakini ni kwa muda mfupi sana, hivyo inakidhi matakwa ya sheria.
huelewi kitu ndugu. fahamu yafuatayo:
1. makanisa ya walokole hayana kengele, hivyo huwezi kulala usingizi ukasikia kengele inaitwa watu waje kanisani au inaamsha watu, noo. hayo ni katoliki, lutheran na wengine. mijini na vijijini.

2. imani ya kilokole, ni imani ya watu, the way wanaexpress themselves wakati wa ibada ndio imani yao inavyotaka, kuwazuia ni kuingilia imani yao, cha maana tu ni kukaa nao chini, aidha wapewe eneo huru lisilo na makazi au wajenge makanisa yenye sound proof.

3. wapinzani wengi wa ibada za walokole, sio walokole, na wengi wao ni wachawi, wazinzi na waabudu dini. hivyo walokole hawategemei hata siku moja kupendwa au kuongelewa vizuri, and they are always ready for them kwasababu wanategemea watu kama wewe utawaaccuse namna hiyo. hamna jipya.

4. misikiti inapiga sana kelele saa kumi kamili umelala, unasikia mikelele, mchana ndio kabisaa. na kwa walokole na waislam hakuna wa kumcheka mwenzake, wote wamejenga makanisa na misikiti katikati ya watu. tembea ubungo hadi magomeni, rudi hadi morrocco, rudi hadi mwenge, rurura mtaani, halafu hesabu umekuta makanisa mangapi na misikiti mingapi iliyozungukwa na nyumba za watu, utashangaa. misikiti ni mingi zaidi na makelele ya kuanzia saa kumi usiku hadi saa kumi na moja yanakera pia. ila tunavumiliana. na waislam huwezi kusema waweke sound proof wanataka kila mtu asikie kule nje ile alah wakibaru.

5. sikumuelewe Pm alipokuwa anasema nyumba za ibada zipunguze sauti, alimaanisha nini? na aliwalenga kina nani, ningeshauri awaache wengine waongee hasa ikizingatia yeye sio mgalatia. sidhani kama waislam walilengwa au wanaweza kukubali kuondoa vile vipaza sauti nje, au wakanong'ona ile alah wakibaru ya saa kumi usiku na kumi na moja. waislam mtuambie kama hilo linawezekana. na kama alilenga wakristo, tunamshauri anyamaze mara moja asituvurugie amani na mshikamano wetu.

6. mwisho, jambo hili ni la kwenda nalo kwa umakini na hekima/busara. ni kweli wapo wauza mafuta kama kina mwamposa ambao huwezi kuwatofautisha na waganga wa kienyeji wao pia wanajiita walokole, though sio walokole. hao kwa ajili ya kutafuta pesa, huamka tu asubuhi, wananunua kiwanja popote na kujenga jengo au kuweka mabati wakaita kanisa bila hata kuconsult mipango miji. hao hata wakivunjiwa tutaunga mkono. ila sio makanisa yale yaliyopata vibali vya ujenzi kisheria.

7. kanisa au msikiti wowote ambao mtu amejenga bila kufuata vibali, tunaomba serikali ikavunje hata kesho. though sina uhakika kama kuna mtu mwenye ujasiri kwenda kuvunja misikiti ya aina hiyo (kama ipo), basi kuwe na balance ili isije kuonekana baadhi ya watu fulani tu ambao huwa hawana fujo wanakubali kuvunjiwa na wengine wakigoma wanaachwa.

alamsiki.
 
Tatizo la kelele ni kubwa kuliko lilivoelezwa hapa. kama tunataka kumaliza kelele maeneo yafuatayo pia yatazamwe
-Movie studios(hizi zimezagaa kila kona na wanatumia maspika makubwa na ni kero)
-kwenye daladala
-bar
-wauza sumu ya mende
-vigodoro
-pikipiki zilizokatwa exhaust.bado
masokoni ni mwendo wa vipaza sauti tu. je tutaweza kuwadhibiti wote hao?
 
ajabu watu wakitaja kelele hapa, wanawaza tu kuwabambikiza walokole kwamba ndio wapiga kelele. wanawasahau hata bodaboda, kumbi za starehe, kumbi za harusi, bar na maeneo mengine. kumbe shida hapa ni ulokole wala sio kelele.
 
Kelele za makanisa aloo ni kero kwanini wasitumie sauti ya kawaida lazima kila mtu asikie???ujue kuna upigaji kelele usio kera ila kelele nyingine ni kutiana majaribuni tu!
 
Hoja ya msingi hapa ni kwamba, mipango miji waje na sura mpya, kanisa au msikiti ujengwe sehemu ambayo pamepangwa nyumba ya ibada tu, sio makazi ya watu. hivyo hivyo na bar na kumbi za harusi na kumbi za starehe.

Nilimwangalia pm anavyoongea, nikaona sihitaji kusikia tena. kwasababu wanaolengwa hapa ni wakristo. waislam huwezi kuwazuia kupiga azana pamoja na yale mafundisho yao ya ijumaa au saa saba mchana kila siku. pamoja na kwamba kama wakiamua kusema sehemu iliyopangwa kwa nyumba ya ibada pekee ndio watu wajenge, misikini mingi sana imejengwa kwenye makazi na hakuna muislam atakayekubali msikiti kuvunjwa hata kama umejengwa ikulu.

Kwa wakristo hasa walokole kwasababu ndio wanaolengwa, wao pia wamekuja na makanisa mengi sana na ya ajabu tena kwenye makazi ya watu. wao ukisema unavunja kama kuna mbadala watakubali. sasa tukae chini, tukalishe dini zote pamoja tuwaambie kuwa tumeamua kuanzia sana majengo ya ibada makazi ya watu yasiwepo, tuwapatie maeneo mbadala wakajenge huko (kwa kuwalipa fidia) ili waondoke maeneo ya watu. la sivyo, kwa wakristo wanaweza kujenga makanisa yanayozuia makeleke kutoka nje, technolojia hiyo ipo. shida ni kwenye azana ya kwenye kile kipaza sauti cha wazi kama inawezekana kutumia tech inayozuia sauti.
Azana inajulikana muda wake, iko kama alarm, muda mwengine unasikia sauti toka msikitini ni Ijumaa muda wa mawaidha.
Kazi ipo kwenu wakristo, kanisa utakuta lina watu kumi hawafikii ila wamefungulia muziki, tena siku ya katikati ya wiki, mtu mpaka unashangaa hawa watu kazini wanaenda saa ngapi
 
huelewi kitu ndugu. fahamu yafuatayo:
1. makanisa ya walokole hayana kengele, hivyo huwezi kulala usingizi ukasikia kengele inaitwa watu waje kanisani au inaamsha watu, noo. hayo ni katoliki, lutheran na wengine. mijini na vijijini.

2. imani ya kilokole, ni imani ya watu, the way wanaexpress themselves wakati wa ibada ndio imani yao inavyotaka, kuwazuia ni kuingilia imani yao, cha maana tu ni kukaa nao chini, aidha wapewe eneo huru lisilo na makazi au wajenge makanisa yenye sound proof.

3. wapinzani wengi wa ibada za walokole, sio walokole, na wengi wao ni wachawi, wazinzi na waabudu dini. hivyo walokole hawategemei hata siku moja kupendwa au kuongelewa vizuri, and they are always ready for them kwasababu wanategemea watu kama wewe utawaaccuse namna hiyo. hamna jipya.

4. misikiti inapiga sana kelele saa kumi kamili umelala, unasikia mikelele, mchana ndio kabisaa. na kwa walokole na waislam hakuna wa kumcheka mwenzake, wote wamejenga makanisa na misikiti katikati ya watu. tembea ubungo hadi magomeni, rudi hadi morrocco, rudi hadi mwenge, rurura mtaani, halafu hesabu umekuta makanisa mangapi na misikiti mingapi iliyozungukwa na nyumba za watu, utashangaa. misikiti ni mingi zaidi na makelele ya kuanzia saa kumi usiku hadi saa kumi na moja yanakera pia. ila tunavumiliana. na waislam huwezi kusema waweke sound proof wanataka kila mtu asikie kule nje ile alah wakibaru.

5. sikumuelewe Pm alipokuwa anasema nyumba za ibada zipunguze sauti, alimaanisha nini? na aliwalenga kina nani, ningeshauri awaache wengine waongee hasa ikizingatia yeye sio mgalatia. sidhani kama waislam walilengwa au wanaweza kukubali kuondoa vile vipaza sauti nje, au wakanong'ona ile alah wakibaru ya saa kumi usiku na kumi na moja. waislam mtuambie kama hilo linawezekana. na kama alilenga wakristo, tunamshauri anyamaze mara moja asituvurugie amani na mshikamano wetu.

6. mwisho, jambo hili ni la kwenda nalo kwa umakini na hekima/busara. ni kweli wapo wauza mafuta kama kina mwamposa ambao huwezi kuwatofautisha na waganga wa kienyeji wao pia wanajiita walokole, though sio walokole. hao kwa ajili ya kutafuta pesa, huamka tu asubuhi, wananunua kiwanja popote na kujenga jengo au kuweka mabati wakaita kanisa bila hata kuconsult mipango miji. hao hata wakivunjiwa tutaunga mkono. ila sio makanisa yale yaliyopata vibali vya ujenzi kisheria.

7. kanisa au msikiti wowote ambao mtu amejenga bila kufuata vibali, tunaomba serikali ikavunje hata kesho. though sina uhakika kama kuna mtu mwenye ujasiri kwenda kuvunja misikiti ya aina hiyo (kama ipo), basi kuwe na balance ili isije kuonekana baadhi ya watu fulani tu ambao huwa hawana fujo wanakubali kuvunjiwa na wengine wakigoma wanaachwa.

alamsiki.
Naomba ifahamike kuwa si lengo la makala kulalamikia makanisa kwa misingi ya tofauti za kidini, bali kuzungumzia tatizo ambalo linahusu baadhi ya makanisa, na wala siyo yote. Ninazungumzia tatizo, na siyo makanisa, wala imani. Makanisa nayataja kwa uhusika wake na tatizo ninalozungumzia. Nazungumza kama mwananchi, mtaalamu wa mazingira aliyesajiliwa (Certified Environmental Expert) wa siku nyingi, na pia kama mwanajamii muathirika wa makelele. Sizungumzii nadharia, nazungumzia uhalisia unaothibitika kwa vipimo vya sayansi ya afya.

Kuhusu kukaa chini kuzungumza na wahusika, hilo limefanyika. Pia NEMC imeishakuwa na vikao na viongozi wa dini mara kadhaa. Watu wanaoamua kwenda kinyume na sheria, mara nyingi hawajihusishi na juhudi za Serikali za kuelimisha jamii.

Kuhusu makanisa hayo kupimiwa maeneo, ukichunguza utangundua kuwa wakati makanisa hayo yanajenga kwenye makazi kulikuwa na schemes mbalimbali za kupima viwanja zilizokuwa zimetenga maeneo ya ibada na huduma za kijamii nje ya makazi ya wananchi. Hivyo wahusika hawajengi kwenye makazi kwa kukosa maeneo yanayofaa, bali wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Tanzania ina ardhi kubwa sana, kama tatizo ni ardhi iliyopimwa, hilo siyo sababu ya kutosha. Kuna maeneo na mashamba ambayo ukinunua leo, kesho unawezakupata mpima akakupimia ukaanza kujenga nyumba yako ya ibada ndani ya wiki mbili. Mbona viongozi wa dini wa namna hiyo hawapati shida kupata viwanja vya kujenga makasri yao ya kuishi kwa amani na familia zao?

Kuhusu kelele za ibada za Waislamu za alfajiri. Kwanza nijitambulishe kuwa mimi ni Mkristo. Kwa hiyo siwezi kuzungumxia viongozi wa Kikristo kwa kuwaona, na wala siwezi kuwazungzia Waisilamu kwa kuwapendelea; hata kama nisingekuwa na maadili ya dini na kitaaluma. Naandika taarifa na kutoa maoni kwa kuzingatia uhalisia, maadili, taaluma, na sheria. Kisheria na kiafya, makelele ya muda mfupi kama azana siyo kero yenye kusababisha athari za kiafya. Ndiyo maana yanavumilika sehemu nyingi duniani.
 
Back
Top Bottom