Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Wakati mchakato wa Bunge la Katiba unaendelea, kumezidi kuibuka mijadala mikali, kuhusu serikali 3 zilizopendekezwa na Tume ya Warioba au kushikilia serikali mbili ambayo ndio sera ya chama tawala, Chama cha Mapinduzi, na tayari wachunguzi wa hesabu za uwiano wa kuwianika wamedhibitisha pasi shaka kuwa endapo uamuzi wa idadi ya serikali utapitishwa kwa kura, then serikali mbili ndio zitapita.

Japo Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, amewasisitiza wajumbe wa Bunge la Katiba, kuheshimu matakwa ya Wananchi waliopendekeza serikali 3, hivyo kazi ya Bunge la Katiba iwe ni kuboresha tuu na ku rubber stamp matakwa ya Wananchi, lakini sio kuyabadili, kuyapindua au kuyafuta kabisa ili kuilinda hadhi ya Tume yake kuwa imewasikiliza wananchi na kuleta kile wananchi walichotaka, Bunge la Katiba, likipindua, kubadili au kufuta chochote, itakuwa ni kuwadharau wananchi na kuidhalilisha kazi nzuri ya tume yake!

Mwanasheria nguli nchini, Prof. Issa Shivji, amesema Bunge la Katiba ndio kila kitu!, ndio mwanzo mwisho kabla ya kura ya maoni, hivyo kazi ya Tume ilikuwa ni kupendekeza tuu na Bunge hili lina mamlaka kamili, kukubali mapendekezo ya tume, kuboresha, kukataa, kuyafuta na kuuleta kitu kingine chochote na sheria na kanuni za Bunge la Katiba zinaruhusu.

CCM kwa upande wake imeishatoa msimamo wa kushikilia serikali mbili kama ilivyo sera yake, hivyo kuhakikisha tunapata katiba mpya ya sera ya Chama cha Mapinduzi kwa kisingizio cha kuulinda muungano, hivyo kuutumia vizuri huo mwanya wa uwiano wa kuwianika wa waungaji mkono wake ndani ya Bunge la Katiba.

Mimi nashauri hivi, kama ni kweli CCM ina nia ya dhati ya kuulinda muungano, basi iwahamasishe wajumbe wa bunge la katiba, kuunga mkono hoja mpya kabisa ya Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja!.

Najua hoja hii itapata upinzani mkali toka upande wa Zanzibar, lakini kama CCM iliweza kumshikisha adabu kwa kumuadabisha rais fulani wa Zanzibar, CCM ikaweza kuyaongeza yale mambo ya muungano kutoka 11 ya awali hadi sasa zaidi ya 20, bila kuishirikisha Zanzibar, CCM ikaweza kuvifumua vipengele muhimu sana vya makubaliano ya muungano kwa kumuengua rais wa Zanzibar asiwe Makamo wa Rais bila kuishirikisha Zanzibar, hivyo CCM inaweza kabisa kuamua twende kwenye serikali moja!, hata Zanzibar wapige kelele vipi, tukiamua tumeamua, na kukionekana dalili zozote za kutaka kuichafua hali ya hewa ya kisiasa, dawa ni kuwashikisha tuu adabu kama tulivyokwisha wahi kufanya kule nyuma walipotaka kuuchokoa Muungano wetu huu Adhimu uliosababishwa na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Hili la serikali moja ndio Muarobaini pekee wa matatizo yote kabisa ya Muungano, na ili kuepuka kumeza Zanzibar, Tunaigeuza Tanzania kuwa ni Federal Union Republic of Tanzania, yenye majimbo mawili la Bara na Zanzibar, haya majimbo yataongozwa na Magavana! Tukiona hii nayo ni ngumu, then tutakuwa hatuna jinsi, Zanzibar igeuzwe tuu kuwa Mkoa mpya wenye wilaya mbili za Pemba na Uguja! Full Stop! Mwisho wa matatizo!

Na huku ndiko kutakuwa kumuunga mkono Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere aliposema.
"CHAMA CHA MAPINDUZI kitakapobadili sera yake ya Muungano wa Serikali mbili, sera yake mpya itakuwa sera ya Muungano wa Serikali moja. Chama cha Mapinduzi chenye wanachama wenye akili, na ukweli, na ujasiri, katu hakiwezi kukubali sera ya serikali tatu, kikijua wazi wazi kwamba matokeo na shabaha ya sera hiyo ni kuiua, na kuizika Tanzania. Chama cha Mapinduzi kikiwa na msimamo huo, na wala kisiuonee haya, Tanzania itadumu." Mwalimu J. K. Nyerere, "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania," Uk. 61.

Tuchukue wosia wa Baba wa Taifa niliounukuu hapo juu kwa manufaa ya nchi yetu na vizazi vijavyo!

Nawasilisha kwa Mjadala zaidi!
Wanabodi, hii nimeikuta humu iliandikwa na Mkuu Mzee Mwanakijiji , miaka 2 iliyopita! Kumbe wakati sisi tunazungumza haya leo, wenzetu walizungumza kitambo!

quote_icon.png
By Mzee Mwanakijiji


Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!

Asante Mkuu Mzee Mwanakijiji, nadhani now it's high time tuunde a pressure group ya serikali moja!. Kama rasimu inapendekeza serikali 3!, CCM imeamua kutupilia mbali maoni ya serikali mbili!, then kama nia ni kuulinda muungano, why not serikali moja?!.

Nchi Moja,
Rais Mmoja,
Serikali Moja!.

Mungu Ibariki Tanzania!.

Paskali
 
SOS Mode, naomba nirekebishie headline halo kwenye mundane, ni muungano!, hivi vigaje vya sasa vinatuletea balaa!

Paskali
 
Point kubwa ni ya Issa Shivji, mambo mengine ya kutaka kukomoa Zanzibar ni mawazo yako na sidhani kama CCM wana mawazo kama hayo. Maelezo yako yanaonesha kabisa serikali moja ni kuwnyanyasa Wazanzibar na kwa maana hiyo haifai, jibu ni serikali mbili tu.
 
Mtoa mada tatizo lako unadhani wazbr wa 64 ni sawa na wazbr wa 2014, Nyerere alilazimisha 2 ndio umeona matatizo yake yalivyo,sasa kama na nyinyi mnataka matatizo zaidi basi lazimisheni iwe moja muone hilo balaa, zanzibar ilikuwepo na itaendelea kuwepo milele, zanzibar kwanza.
 
Serikali moja ndio italeta maana hasa ya muungano, vinginevyo ni usanii uleule wa1964; mmoja anakufa mmoja anabaki. Kwa sababu ya uroho wa madaraka, serikali tatu angalau itaonyesha nchi zimeungana. Huu wa sasa ni kiini macho tu.
 
Aisee! Serikali moja ni mzuri lakini kinguvu haiwekani kama itakavyoshindwa serikali 2 wazitakazo CCM!
...
Muda utanena!
Hakuna kisichowezekana chini ya jua! kama mwanzo tuliweza kwa nini sasa tushindwe?
Pasco
 
Una kazi kubwa sana Pasco ya kuwashawishi wazanzibar kwa hilo, na siamini kama litafanikiwa. Kumbuka hilo lilikuwa sharti moja ambalo hata muasisi wa Muungano Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na Thabit Kombo walilomfunga baba wa Taifa mwaka 1964, ya kuwa 'ukitaka tuungane na nchi kubwa kama Tanganyika, sisi hatutakubali kuwa Mkoa wa Tanzania.

Nchi yetu ya Zanzibar ambayo tuliikomboa kwa kumwaga damu katika Mapinduzi ya Januari mwaka huo huo wa 1964 lazima ibaki na Baraza la Mapinduzi na Serikali ya Mapinduzi iendelee kuwepo.' Kwa wakati ule Mwalimu aliwakubalia akifikiri ya kuwa baada ya muda hili suala la uzanzibari litapoa, hasa baada ya kuunganisha TANU na ASP na kuunda CCM, ambayo ilianzishwa kwa makusudi kabisa Zanzibar mwaka 1977.

Sasa kama miaka takriban 50 imepita, waasisi hawapo tena, na wazanzibari wa leo kama walivyokuwa waasisi wa Mapinduzi bado wamekomalia kuwa na serikali yao, na wamejizatiti sana mpaka kuandika upya Katiba yao ambayo wanatamka hadharani ya kuwa Zanzibar ni nchi, usijidanganye wala asijidanganye mtu yeyote kama itakubalika kuwa na serikali moja. Tusipoangalia kitanuka.

Walimtoa Sultani kwa mapanga, magongo na silaha mbalimbali za jadi miaka 50 iliyopita, huwaambii lolote leo hii. Mark my words.
 
Last edited by a moderator:
Asante mtoa Hoja - Pasco. Mimi nasifu namna ulivoandika mada yako. Mimi ni mpinzani mkubwa wa serikali mbili na moja pia lakini kwa namna hii, lazima nikusifie. Umeweza kuturudishia udikteta wa CCM katika duara na gumzo. Zanzibar haina khiari katika maamuzi ya mustaqbali wake.

Mpaka leo hatujaonyeshwa mkataba wa muungano wala muungano wenyewe haukuidhinishwa na bunge/wawakilishi wa Zanzibar.
"very interesting".

Tunakwenda kwenye TATU ya MKATABA.
 
Mtoa mada tafadhali mara nyengine kabla ya kuandika na kurusha hakikisha kichwani mwako mvinyo umemaliza.
 
Hapa Pasco kuhusu kuwa na serikali moja tuko pamoja kwa 100%

Ila ulichoandika hapa sikubaliani nacho.

Na Pasco wa JF

....Najua hoja hii itapata upinzani mkali toka upande wa Zanzibar, lakini kama CCM iliweza kumshikisha adabu kwa kumuadabisha rais fulani wa Zanzibar, CCM ikaweza kuyaongeza yale mambo ya muungano kutoka 11 ya awali hadi sasa zaidi ya 20, bila kuishirikisha Zanzibar, CCM ikaweza kuvifumua vipengele muhimu sana vya makubaliano ya muungano kwa kumuengua rais wa Zanzibar asiwe Makamo wa Rais bila kuishirikisha Zanzibar, hivyo CCM inaweza kabisa kuamua twende kwenye serikali moja!, hata Zanzibar wapige kelele vipi, tukiamua tumeamua, na kukionekana dalili zozote za kutaka kuichafua hali ya hewa ya kisiasa, dawa ni kuwashikisha tuu adabu kama tulivyokwisha wahi kufanya kule nyuma walipotaka kuuchokoa Muungano wetu huu Adhimu uliosababishwa na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.


Ni makosa makubwa sana ya 'kiufundi' kuilinganisha CCM na Zanzibar, CCM ni chama cha Siasa kinacho'ungwa mkono' pote Zanzibar na Tanzania Bara. Zanzibar ni "NCH"
 
Hapa Pasco kuhusu kuwa na serikali moja tuko pamoja kwa 100%

Ila ulichoandika hapa sikubaliani nacho.

Na Pasco wa JF

Najua hoja hii itapata upinzani mkali toka upande wa Zanzibar, lakini kama CCM iliweza kumshikisha adabu kwa kumuadabisha rais fulani wa Zanzibar, CCM ikaweza kuyaongeza yale mambo ya muungano kutoka 11 ya awali hadi sasa zaidi ya 20, bila kuishirikisha Zanzibar, CCM ikaweza kuvifumua vipengele muhimu sana vya makubaliano ya muungano kwa kumuengua rais wa Zanzibar asiwe Makamo wa Rais bila kuishirikisha Zanzibar, hivyo CCM inaweza kabisa kuamua twende kwenye serikali moja!, hata Zanzibar wapige kelele vipi, tukiamua tumeamua, na kukionekana dalili zozote za kutaka kuichafua hali ya hewa ya kisiasa, dawa ni kuwashikisha tuu adabu kama tulivyokwisha wahi kufanya kule nyuma walipotaka kuuchokoa Muungano wetu huu Adhimu uliosababishwa na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.


Ni makosa makubwa sana ya 'kiufundi' kuilinganisha CCM na Zanzibar, CCM ni chama cha Siasa kinacho'ungwa mkono' pote Zanzibar na Tanzania Bara. Zanzibar ni "NCH..."
Mkuu Tujitegemee, safari ya kuelekea kwenye serikali moja ndio njia pekee ya kuuimarisha muungano kwa dhati, kwa sababu nauhesabu muungano wetu kama ndoa, "mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataandamana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja!". This is a very big sacrifice!.

Ili kuimarisha kuiimarisha hiyo ndoa lazima hizi big sacrifices za kuachana na baba yake na mama yake zifanyike, na kuandamana na mkewe!. Wale wanandoa wanaendelea kukaa kwa wazazi, ndoa zao hukumbwa na matatizo!

Tanganyika na Zanzibar zilipoungani, ni Tanganyika pekee, ilitoa the biggest sacrifice, ya kuupoteza utaifa wake, ikauua kabisa for the sake of union na kuwa Tanzania!. What sacrifice did Zanzibar did?!. You can't eat your cake and have it! Kama mmemsikia vizuri Jaji Warioba, wazo la muleta serikali tatu, ili ili kuibembeleza Zanzibar ibakie kwenye muungano kufuatia katiba ya Zanzibar kuuvunja muungano kimya kimya huku bara ikinyamaza, ikimchelea mwana kulia!

Kwenye thima ya Muungano, Tanganyika iliishakufa zamani, hivyo nchi inayoitwa Tanganyika, haiwezi tena kukufufuka!, this is a very big sacrifice!, dhima hiyo ikaitambulisha Zanzibar kuwa "sii nchi" bali "ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" yenye mamlaka yake ya ndani!. Katiba ya Zanzibar ya 1984 (Toleo la 2010), linaitambulisha Zanzibar kama nchi, ndani ya JMT, ina weka mipaka yake!, bendera yake!, wimbo wake wa taifa!, na kumtambulisha rais wa Zanzibar kama Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la JKU na Vikosi vya SMZ!, uliwahi kuona wapi nchi ndani ya nchi?!.

Inaonekana kana kwamba Zanzibar inabembelezwa ibaki ndani ya muungano kwa kuiacha ifanye kila inanachotanga!, kama ni sacrifices, only Bara!, kila kitu ni Bara!, wajumbe wa tume ya kukusanya maoni 50/50!, kugharimia gharama za tume, ni bara asilimia 100!. Sasa bunge la Katiba, nalo linagharimiwa 100% na bara!.

Sasa kama nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, its about time, Zanzibar nayo, itoe sacrifice, ipoteze utaifa wake!, tende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja, tena ili kuwapunguzia machungu, wenzetu, katiba itamke rais wa kwanza, atatoka Zanzibar (awe Dr. Shein).

Nimeitaja CCM kwa sababu tukubali, tukatae, CCM ni chama dola!, kama kiliweza kuamua yale mengine!, na kama nia ya dhati ni kuimarisha muungano, sio serikali tatu!, sio serikali mbili!, ni serikali moja!

Pasco.
 
''Kama Kweli Nia ya Dhati ni Kuimarisha Muungano, Then, "Twende Kwenye Serikali Moja!".
Naomba kuungana kidog na Bw. Pasco kama ifuatavyo.

Maoni ya CCM ya kubakia na sera ya muungano ni ya kimgando na udikteta. Ninasema ni ya kimgando na uditeta kwa sababu maamuzi yaliyotolewa hayakufutia taratibu za chama kwa maana ya ushrikishwaji wa chama kuanzia ngazi za chini. CCM ilitoa waraka wake na kuusambaza kama moto wa kifuu kwenye matawi na kututaka kukubaliana na mwelezo yake na kuwarudihia mjibu siku hiyohiyo. Tukiwa ndani ya kikao tulilishwa maneno hayo, ya kwamba tukubaliane na maamuzi ya juu kuwa kuwepo na se.

Serikali mbili bila hata ya kutupa fursa ya kuka na kuusoma waaka wake kwa kina ili tweze kuelewa kilichokua kimendikwa mle.Waraka huu ulitolewa wakai wa rasimu ya kwanza. CCM kilipaswa kutafakari kwanza yaliyokwishajiri kule visiwani kwa mujibu ya katiba yake ya mwaka 2010 kwamba wao ni nchi kwa wimbo, bendera, baraza la wawakilshi na raisi wao kupewa hashima sawa na Raisi wa Miingano. Vilevile siku miaka 50 ya Zanzibar raisi wa muungano hakupata nafasi yoyote yakuzungumza. Kwa mujibu Zanzibar wa kuwa na hayo niliyoyataja hapo juu,bila kumng'unya maneno tayari muunganao mekwshaunjwa na Visiwani.

Jambo jingine ambalo CCM imeliona nfikiri wanang'ania seriali mbili kwa kutilia maanani kuwa kwa visiwani kuwa na katiba yake tayari wlishajiingiza mkenge wa kuivunja ktiba ya muungano enyewe bila yauwasiliha hoja mahali husika.

Nimejaribu kufanya utafiti kidogo kwa Baadhi ya nchi nyingine ambazo zimewishaungana k.m Urusi, Uinereza na Marekani hakuna mikataba ya maridhiano ya muungano wao ila zilipigwa. Hapa ndipo ninapobaliana na Bwana Pasco. Hivyo basi CCM wametumia upofo uliopo visiwani.
 
Back
Top Bottom