hakuna kisichowezekana chini ya jua!, kama mwanzo tuliweza kwa nini sasa tushindwe?.
Pasco
Mwanzo gani uliweza?! Kwanza bwana Pasco, Zanzibar ni nchi au si nchi? Ukijibu tutajadili kwa nini ni serikali 1 na au kidogo 3 na si mbili(2)!
hakuna kisichowezekana chini ya jua!, kama mwanzo tuliweza kwa nini sasa tushindwe?.
Pasco
Mkuu Tujitegemee, safari ya kuelekea kwenye serikali moja ndio njia pekee ya kuuimarisha muungano kwa dhati, kwa sababu nauhesabu muungano wetu kama ndoa, "mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataandamana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja!". This is a very big sacrifice!.Hapa Pasco kuhusu kuwa na serikali moja tuko pamoja kwa 100%
Ila ulichoandika hapa sikubaliani nacho.....
Na Pasco wa JF
....Najua hoja hii itapata upinzani mkali toka upande wa Zanzibar, lakini kama CCM iliweza kumshikisha adabu kwa kumuadabisha rais fulani wa Zanzibar, CCM ikaweza kuyaongeza yale mambo ya muungano kutoka 11 ya awali hadi sasa zaidi ya 20, bila kuishirikisha Zanzibar, CCM ikaweza kuvifumua vipengele muhimu sana vya makubaliano ya muungano kwa kumuengua rais wa Zanzibar asiwe Makamo wa Rais bila kuishirikisha Zanzibar, hivyo CCM inaweza kabisa kuamua twende kwenye serikali moja!, hata Zanzibar wapige kelele vipi, tukiamua tumeamua, na kukionekana dalili zozote za kutaka kuichafua hali ya hewa ya kisiasa, dawa ni kuwashikisha tuu adabu kama tulivyokwisha wahi kufanya kule nyuma walipotaka kuuchokoa Muungano wetu huu Adhimu uliosababishwa na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964......
Ni makosa makubwa sana ya 'kiufundi' kuilinganisha CCM na Zanzibar, CCM ni chama cha Siasa kinacho'ungwa mkono' pote Zanzibar na Tanzania Bara. Zanzibar ni "NCH..."
Mkuu Chaza, Zanzibar ilikuwa nchi hadi April, 26, 1964, from there, haiku nchi tena bali sehemu ya JMT!, kama ilivyokufa Tanganyika tarehe hiyo hiyo na kuundwa JMT.Mwanzo gani uliweza?! Kwanza bwana Pasco, Zanzibar ni nchi au si nchi? Ukijibu tutajadili kwa nini ni serikali 1 na au kidogo 3 na si mbili(2)!
Mkuu Chaza, Zanzibar ilikuwa nchi hadi April, 26, 1964, from there, haiku nchi tena bali sehemu ya JMT!, kama ilivyokufa Tanganyika tarehe hiyo hiyo na kuundwa JMT.
Tanganyika ilipoteza utaifa wake na Zanzibar ilipoteza utaifa wake!. Kilichofanywa na Katiba ya Zanzibar ya 1984 toleo la 2010, ilikuwa ni kama kwenye ndoa, mke kaomba talaka ili aachwe, ukagoma, akaamua kufanya vitendo vya kupelekea kuvunjika kwa ndoa, ikiwemo kwenda nje ya ndoa!. Hivyo ilichokifanya Zanzibar ni kutokaq nje ya ndoa ili kupewa talaka!.
Bahati nzuri au mbaya, sijui tuiite Tanganyika ni mume zoba, au ndio anampenda sana mkewe!, hata baada ya kuushuhudia uzinifu huo wa mkewe, bado anampenda sana!, na kosa moja haliachi mke!, hivyo amesamehe na ndoa inaendelea, huku huyu mke akiendelea na visa hivi na vile kudai talaka yake!.
Pasco.
Mmmmh. Mkuu basi hata kukemea jambo la kuandikwa katiba kinyemela sijamsikia kiongozi yeyote mkuu wa Kitaifa akikemea jambo hilo, kwa nini? Huko si ni kulea maradhi, hayawezi kuleta madhara makubwa baadae? Wewe kaka Pasco unasimamia wapi? Unajemea au unaona ni sawa tu walichofanya Zanzibar?
Una utani na Wazanzibari?
Mtoa mada tatizo lako unadhani wazbr wa 64 ni sawa na wazbr wa 2014,nyerere alilazimisha 2 ndio umeona matatizo yake yalivyo,sasa kama na nyinyi mnataka matatizo zaidi basi lazimisheni iwe moja muone hilo balaa,zanzibar ilikuwepo na itaendelea kuwepo milele,zanzibar kwanza.
Mkuu Buchanan, asante kwa hili, na mimi nililizungumzia hapa [h=3]Kama Kweli Nia ya Dhati ni Kuimarisha Muungano, Then, Twende Kwenye Serikali Moja!"!.[/h]Pasco"CHAMA CHA MAPINDUZI kitakapobadili sera yake ya Muungano wa Serikali mbili, sera yake mpya itakuwa sera ya Muungano wa Serikali moja. Chama cha Mapinduzi chenye wanachama wenye akili, na ukweli, na ujasiri, katu hakiwezi kukubali sera ya serikali tatu, kikijua wazi wazi kwamba matokeo na shabaha ya sera hiyo ni kuiua, na kuizika Tanzania. Chama cha Mapinduzi kikiwa na msimamo huo, na wala kisiuonee haya, Tanzania itadumu." Mwalimu J. K. Nyerere, "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania," Uk. 61.
Tuchukue wosia wa Baba wa Taifa niliounukuu hapo juu kwa manufaa ya nchi yetu na vizazi vijavyo!
Nawasilisha kwa Mjadala zaidi!
​Wanabodi,
Wakati mchakato wa Bunge la Katiba unaendelea, kumezidi kuibuka mijadala mikali, kuhusu serikali 3 zilizopendekezwa na Tume ya Warioba au kushikilia serikali mbili ambayo ndio sera ya chama tawala, Chama cha Mapinduzi, na tayari wachunguzi wa hesabu za uwiano wa kuwianika wamedhibitisha pasi shaka kuwa endapo uamuzi wa idadi ya serikali utapitishwa kwa kura, then serikali mbili ndio zitapita.
Japo Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, amewasisitiza wajumbe wa Bunge la Katiba, kuheshimu matakwa ya Wananchi waliopendekeza serikali 3, hivyo kazi ya Bunge la Katiba iwe ni kuboresha tuu na ku rubber stamp matakwa ya Wananchi, lakini sio kuyabadili, kuyapindua au kuyafuta kabisa ili kuilinda hadhi ya Tume yake kuwa imewasikiliza wananchi na kuleta kile wananchi walichotaka, Bunge la Katiba, likipindua, kubadili au kufuta chochote, itakuwa ni kuwadharau wananchi na kuidhalilisha kazi nzuri ya tume yake!.
Mwanasheria nguli nchini, Prof. Issa Shivji, amesema Bunge la Katiba ndio kila kitu!, ndio mwanzo mwisho kabla ya kura ya maoni, hivyo kazi ya Tume ilikuwa ni kupendekeza tuu na Bunge hili lina mamlaka kamili, kukubali mapendekezo ya tume, kuboresha, kukataa, kuyafuta na kuuleta kitu kingine chochote na sheria na kanuni za Bunge la Katiba zinaruhusu.
CCM kwa upande wake imeishatoa msimamo wa kushikilia serikali mbili kama ilivyo sera yake, hivyo kuhakikisha tunapata katiba mpya ya sera ya Chama cha Mapinduzi kwa kisingizio cha kuulinda muungano, hivyo kuutumia vizuri huo mwanya wa uwiano wa kuwianika wa waungaji mkono wake ndani ya Bunge la Katiba.
Mimi nashauri hivi, kama ni kweli CCM ina nia ya dhati ya kuulinda muungano, basi iwahamasishe wajumbe wa bunge la katiba, kuunga mkono hoja mpya kabisa ya Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja!.
Najua hoja hii itapata upinzani mkali toka upande wa Zanzibar, lakini kama CCM iliweza kumshikisha adabu kwa kumuadabisha rais fulani wa Zanzibar, CCM ikaweza kuyaongeza yale mambo ya muungano kutoka 11 ya awali hadi sasa zaidi ya 20, bila kuishirikisha Zanzibar, CCM ikaweza kuvifumua vipengele muhimu sana vya makubaliano ya muungano kwa kumuengua rais wa Zanzibar asiwe Makamo wa Rais bila kuishirikisha Zanzibar, hivyo CCM inaweza kabisa kuamua twende kwenye serikali moja!, hata Zanzibar wapige kelele vipi, tukiamua tumeamua, na kukionekana dalili zozote za kutaka kuichafua hali ya hewa ya kisiasa, dawa ni kuwashikisha tuu adabu kama tulivyokwisha wahi kufanya kule nyuma walipotaka kuuchokoa Muungano wetu huu Adhimu uliosababishwa na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Hili la serikali moja ndio Muarobaini pekee wa matatizo yote kabisa ya Muungano, na ili kuepuka kumeza Zanzibar, Tunaigeuza Tanzania kuwa ni Federal Union Republic of Tanzania, yenye majimbo mawili la Bara na Zanzibar, haya majimbo yataongozwa na Magavana!. Tukiona hii nayo ni ngumu, then tutakuwa hatuna jinsi, Zanzibar igeuzwe tuu kuwa Mkoa mpya wenye wilaya mbili za Pemba na Uguja!. Full Stop!, Mwisho wa matatizo!.
Na huku ndiko kutakuwa kumuunga mkono Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere aliposema
Nchi Moja,
Serikali Moja,
Rais Mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania!.
Pasco.
Serikali moja ndio italeta maana hasa ya muungano, vinginevyo ni usanii uleule wa1964; mmoja anakufa mmoja anabaki. Kwa sababu ya uroho wa madaraka, serikali tatu angalau itaonyesha nchi zimeungana. Huu wa sasa ni kiini macho tu.
Una utani na Wazanzibari?